Jukumu la Vyama Vyetu vya Wafanyakazi sasa ni nini hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jukumu la Vyama Vyetu vya Wafanyakazi sasa ni nini hasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 20, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo mengi yanatokea nchini ambayo yanagusa maslahi ya wafanyakazi. Mambo ambayo kuendelea kwake kunahatarisha maslahi ya wafanyakazi na mambo mengine ambayo yamesababisha ukimya na utulivu wa vyama hivyo kusimamia watawala. Vyama vya wafanyakazi kwa asili yake viliibuka ili kuzuia nguvu ya mabepari kunyonya nguvu kazi za wafanyakazi na kudai maslahi bora zaidi ya kazi n.k Lakini katika sehemu nyingi vyama vya wafanyakazi vimeendelea kuwa speed governors dhidi ya utawala unaojaribu kujinufaisha kwa migongo ya wafanyakazi na hivyo kutokana na mbinu mbalimbali vyama hivyo vimeweza kusababisha hata mabadiliko ya kisiasa na kisheria kwnye nchi mbalimbali.

  Kwa Tanzania vyama vya wafanyakazi vina historia ndefu ya kubadilisha mwelekeo wa kisiasa nchini. Sasa hivi vyama hivi vinaonekana vimekaa pembeeni na kuacha vyama vya upinzani kufanya yale ambayo yalitakiwa kufanywa na vyama vya wafanyakazi. Ni kitu gani kimetokea nchini na kusababisha hii docility ya vyama vya wafanyakazi nchini? Ni kwanini vyama vya wafanyakazi havina uthubutu wa kusimama na kudai maslahi bora ya kweli ya wananchi lakini wakati huo huo kuzuia ufujaji mkubwa wa raslimali zetu ili raslimali hizo zitumike kuinua maslahi ya wafanyakazi? Yawezekana vyama vya wafanyakazi nchini havina tena nafasi isipokuwa wakati wa kudai kima cha chini cha mishahara na siyo mambo mengine? Je bado vina umuhimu wa watu kujiunga navyo? Je vyama hivi vinaweza kuwa na nguvu ya kubadilisha maisha ya wanachama wake bila kugongana na wanasiasa?

  Michango yenu itanisaidia katika hoja yangu ya Jumatano.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu nchi inapooza uozo huo unaji manifest kwenye vitu vingi sana. Nchi inaoongozwa kwa hongo, milungula na rushwa kwa hiyo vyama vya wafanyakazi haviwezi kupona ama kujing'atua kutoka kwenye mashimo ya rushwa, milungula na hongo. Hakuna lingine zaidi ya kwamba mabepari/wawekezaji wanawatia mifukoni watendaji mablimbali wakiwamo viongozi wa vyama vya wafanyakazi kwa hiyo vyama haviwezi kutenda ambayo yantegemewa toka kwao. Mimi siwezi kujiunga na vyama hivyo.
   
 3. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Walipokuwa wakija mabwana wa soko huria wakaona chama cha wafanyakazi kinapiga kelele sana. Wakawaambia wakuwadi wao, "vunja chama cha wafanyakazi". Makuwadi wa soko huria wakavunja. Wakakagua, bado wakasikia tuvyama tuna kelele. Wakauliza, "hivi we kuwadi unaishije na kelele zote hizi hazikusumbui?". Wakaagiza tena, 'vunja zaidi, vibaki vidogo vidogo viwe na uhuru sawa na shirikisho lake'. Wakatii!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Swali ni je bado wapo watu wanajiunga na vyama vya wafanyaka? Je vina jukumu lolote leo hii?
   
 5. Kamisaa

  Kamisaa Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni vyama vya wafanyakazi kutumiwa na vyama vya siasa. Zamani wakati wa chama kimoja vilitumika na CCM; sasa hivi vinatumika na vyama vya upinzani kwa maslahi ya kisiasa badala ya kusimamia maslahi ya wafanyakazi na kuwahamasisha juu ya haki zao. Siku hizi viongozi wengi wa vyama vya wafanyakazi wameshabikia mabadiliko ya kisiasa wakidhani kuwa hayo yataleta mabadiliko ya maslahi ya wafanyakazi.
   
 6. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kupiga dili na waajiri. kwa mfano, wafanyakazi wanaweza kuwa na madai yao ya msingi na wakaona ili kupata haki yao, lazima 'kulianzisha'. inapotokea hivo, kwa viongozi wa wafanyakazi huwa ni dili. utawaona wakijibaraguza kufanya vikao na menejimenti kama sehemu ya kutafuta suluhu, lakini ukweli ni kuwa huwa wanatafuta rushwa.

  si munakumbuka ya gratian mukoba? si alirushiwa viti pale diamondi jubilii? kwani unahitaji kwenda skuli kujua kama alikuwa amepewa chake?

  ukisikia viongozi wa chama cha wafanyakazi wanatishia kuchochea mgomo, ujue wameishiwa hela. wanataka kupozwa na waajiri.

  nina mfano hai: hapa nafanya kazi mwaka jana (wakati mkurugenzi akiwa ni mwingine) mshahara ulipanda 15%. mwaka huu mkurugenzi mpya, uzalishaji ni zaidi ya mwaka jana, na faida ni zaidi ya mwaka jana, lakini tumepongezwa kwa kupewa soda moja, kipande cha kuku na 7% nyongeza ya mshahara. viongozi wapo, wafanyakazi wanataka 50%, hakuna anayewapigania.

  ngoja niishie hapa
   
 7. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  the way it seems serikali yetu hufanikiwa kuwaweka mfukoni viongozi wa vyama hivi kwa kuwafanya tabaka la wanyonyaji dhidi ya wafanyakazi. Hebu fikiria CWT mapesa yote ya makato yanaishia wapi? Na jee yule kiongozi wao aliyesema "majirani wakigombana chukua kapu ukavune ??" alimaanisha kwamba sasa matatizo ya wafanyakazi yamekwisha au alikuwa anashukuru kuwa waliokuwa wanamgombanisha na Kikwete sasa wameumbuka? Hapa hatuna uongozi, tuna tabaka jingine la wanyonyaji.
   
 8. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  the way it seems serikali yetu hufanikiwa kuwaweka mfukoni viongozi wa vyama hivi kwa kuwafanya tabaka la wanyonyaji dhidi ya wafanyakazi. Hebu fikiria CWT mapesa yote ya makato yanaishia wapi? Na jee yule kiongozi wao aliyesema "majirani wakigombana chukua kapu  ukavune ??" alimaanisha kwamba sasa matatizo ya wafanyakazi yamekwisha au alikuwa anashukuru kuwa waliokuwa wanamgombanisha na Kikwete sasa wameumbuka? Hapa hatuna uongozi, tuna tabaka jingine la wanyonyaji.
   
 9. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kuna chama,kama tuico,kilianzishwa toka enzi ya chama kimoja,na hadi sijaona lolote jipya walilowafanyia wafanyakazi hawa wa tanzania.
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,220
  Likes Received: 7,339
  Trophy Points: 280
  Imekuwa ni ajira inayolipa ukiwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi. Unaona kukurukakara za hongo wakati wa uchaguzi.
  Kazi ya kuendesha vyama vya siasa ni ngumu sana na ni kiongozi anayejiamini na aliyetayari kwa lolote ndiye anaweza kusimama, lakini ni kinyume cha matarajio hayo hapa nchini.

  Pili, viongozi wanaingia kwa rushwa na wengi hawajui maana halisi ya vyama vya wafanyakazi. Kama ulivyosema wao wanadhani kazi yao inaishia pale kima cha chini cha mshahara kinapowekwa. Wanadhani kazi yao ni kuandaa maandamano ya mei mosi. Wengine hawajui hata chimbuko la vyama vya wafanyakazi duniani.

  Kama wangelijua kazi ya Rashidi mfaume Kawawa kama kiongozi wa wafanyakazi pengine wasingekuwa walivyo. Kawawa alishiriki sana siasa na mara nyingi alikjikuta katika misuko suko na wakoloni si kwa siasa au maslahi binafsi bali kutumia wafanyakazi kuendesha migomo. Alifanya hivyo akijua ukombozi wa mfanyakazi haushii kudai mshahara bali maingiliano na wanaopanga mishahara. Hadithi hiyo ndiyo ya Morgan Tvangirai na marehemu Chiluba. Zaidi ya hapo viongozi hawajui kuwa hiyo pia ni ngazi muhimu kiutawala hasa kisiasa.

  Wanapochaguliwa mara zote huwekwa mfukoni kwa sababu dhamira yao ya uongozi haikuwa kumsaidia mfanyakazi bali maslahi binafsi.
  Inashangaza wapinzani wanaposimamia hoja za posho bila kusikia neno kutoka vyama vya wafanyakazi!! Wao wanadhani wapinzani wanawahitaji na hawajui ni symbiosis kwamba kama wangeitumia turufu vyema basi ingekuwa kwa masilahi yao zaidi kuliko wanasiasa.
   
 11. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  aaaargh! Leo tena siku yangu inaharibika hivi hivi, yani nakutana asubuhi na habari ya kitu nisichokipenda na kinachoumiza wafanyakazi ''vyama vya wafanyakazi.''
  Ubovu wa vyama vya wafanyakazi
  MAHUSIANO KATI YA VIONGOZI NA WANACHAMA mahusiano baina yao mara nyingine ni duni au hayapo kabisa na hii ni kutokana na mfumo hasahasa serikalini eti mtu unaajiriwa automatically unakatwa 2percent ili iende workers union so wale viongozi wa vyama hawawezi kuwatafta wanachama wakutane nao wawaeleze roles zao na vipi wanaweza kumsaidia mfanyakazi lkn hayo maviongozi yako tu yanakula kiyoyozi ofisini huku wafanykazi wanateseka hawajui watasaidikaje na nani awasaidie as long as wao wanapata pesa from contribution unayokatwa hawana haja ya kujua wafanyakazi. Hili lingekua solved only if wafanyakazi walipwe hela afu watoe michango wenyeywe hawa viongozi wa vyama vya wafanyakazi wangetuheshimu
  Tatizo jingine ni AINA YA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI hili nalo ni tatizo viongozi wengi wa hivyi vyama ni kama tu wabunge wengi hawako pale kwa kusaidia wafanyakazi bali kwa lengo la kuganga njaa washazfanya hizo ofisi vijiwe vya mshahara na posho huku wakilinda maslahi ya vigogo kuliko ya wafanyakazi. Viongozi wa vyama wa wafanyakazi ni MASNITCH wakubwa Mfano ni mwanzoni wa mwaka huu baada ya kupata ajira ktk halmashauri moja tulikuwa tunafuatilia stahili zetu za nauli, mizigo etc, ila sasa kukawa na mizinguo flani si unajua bongo tena, tukafight ikawa inakuwa ngumu tukaenda kwa katibu wa chama cha wafanykazi wilayani hapo tukaongea tukamwambia tatizo letu kila kitu akasema kweli huko kuna wizi tumuachie ka siku tatu atatjulisha eehh! Baada ya siku 2 wote tulioenda kwa katibu tulipokea barua kali ya onyo toka kwa mkurugenzi eti ni marufuku kwenda ofisi ya chama wala kwake kudai serikali haina hela khaaaaa! Tulichefuka na kuamua kudai kwa nguvu bila chama chetu na tuliolipwa ni wale tulioenda front bila woga ila sasa tumekuwa marked hakuna kwenda semina, kozi, field wala vikao yaani posho ndo tusahau hiivyo hatupewi chance hata ka unastahili.
  Tatizo lingine ni SHERIA Sijui sheria ya hivi vyama vikoje ila nahisi haina meno juu mwajiri, haki ya mikutano ya wafanyakazi na vikao vyao vianishwe kisheria ili mfanyakazi awe na haki ya kuhudhuria vikao bila upinzani toka kwa mwajiri.
  SIASA hili nalo ni tatizo lingine viongozi wa vyama vya wafanyakazi wengi wana malengo ya kisiasa kwa hiyo kwenye vyama vya wafanyakazi wanatafuta umaaarufu na siku zote hufanya kazi kuwaridhisha wale walioko ktk vyama vyao vya kisiasa na sio wafanyakazi.
  MATUMIZI YA RASILIMALI NA OFISI sijui ka mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali hufika huku viongozi wa vyama vya wafanyakazi wana matumizi mabaya ya ofisi na rasilimali hujiandikia vikao na semina nyiiingi kwa ajili ya posho na kukaa ktk vituo vyao kusaidia wafanyakazi ni very rare na kuhusu kodi ya majengo na vitega uchumi ambavyo vimejengwa kwa michango yetu hizo ndo wanakula na wakubwa wanaowalinda.
  Tatizo kubwa lingine ktk ufanisi wa hivyi vyama ni SISI WENYEWE WAFANYAKAZI tumekuwa ni waoga kudai haki zetu tunalalamika kwenye korido tu na ofisini mkiambiwa kuna kikao cha workers union hawaudhurii kwenye kuchagua viongozi na wawakilishi tena mnachagua watu kwa kuhongwa, kujuana au kuwa idara moja badala ya kuangalia uwezo yaaani aliyeturoga kafa. Haya mkijitokeza wachache kudai kwa ajili ya wote ndo yale ya majina yanaibuka ofisini oohh mara wanaharakati chadema, lissu sijui nini kashfa kibao.
  ALL IN ALL VYAMA VYA WAFANYAKAZI INGAWA TUNAVIGHARAMIKIA SISI HAVIKO KWA AJILI YETU WAFANYAKAZI BALI KWA WAAJIRI
   
 12. SHIGELLA

  SHIGELLA Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wafanyakazi na watanzania wengi wa Leo hawana utamaduni wakushiriki jambo na kuwawajisha wanao kwenda kinyume na melengo waliojiwekea..! wakisha kasimu madaraka kwa mtu basi wao wanabaki kuwa walalamikaji, mashabiki, watazamaji....na watetea masilahi ya kikundi fulani chenye masilahi yao wachache! Aiadha mwanachama akiwa natatizo ndio analalamika na kukashifu chama na atakapomaliza shida yake anasahau yote maozo nakuacha uozo na urasimu unaendelea kunyanyasa wengine! Wajumbe nao wapo tu kwa ajili ya posho za safari na vikao wala si kwa masilahi ya waliowachagua "YAANI UBINAFSI UNATAWALA NA NGUVU YA PAMOJA INAPOTEA". muitikio wa wafanyakazi kujiunga na vyama hivi umepungua sana, wanajiunga tu au kujikuta ni wanachama kwakuwa wanakatwa michango moja kwa moja kwenye mishahara yao.
   
 13. M

  Mindi JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,389
  Likes Received: 939
  Trophy Points: 280
  Kwanza huko nyuma, Nyerere alijaribu kuunganisha vyama vya wafanyakazi katika mfumo wa chama kimoja, pengine ili kupunguza upinzani, lakini aliwahi kunukuliwa akisema "Tanzania mtu ukigoma unamgomea nani?" kutokana na mfumo aliokuwa anaukusudia, kwamba mamlaka ni ya wananchi, nchi ni yao, kila kitu ni chao. nadhani hii haikufanikiwa, na ni moja ya mambo ambayo hata yeye angepewa "second chance", angefanya vingine. kuna mahala niliwahi kusoma mtu kaandika kwamba ukishakuwa mwajiri, utakuwa na mindset ya mwajiri. utapenda ku-maximise kazi na masaa ya kazi, na ku-minimise malipo kwa watu, ili upate faida zaidi. hata kama utawapa watu maslahi mazuri, si kwa sababu unawapenda sana, bali ni kama mtu anayemlisha kuku vizuri ili atoe mayai mengi au apate uzito mzuri apate bei nzuri na mwisho faida zaidi kwake. kadhalika ukiwa mwajiriwa, kuna mindset yake tofauti: ku-maximise malipo, na ku-minimise kazi na masaa ya kazi.

  Kama taifa, tungependa kuangalia mambo katikati, kwamba taifa linafaidika kama watu wanafanya kazi zaidi lakini pia wanakuwa na maslahi mazuri. Nyerere alikuwa na nia nzuri lakini hakupata njia muafaka ya kufikia nia yake. katika mifumo yetu ya sasa hivi, serikali au "system" ina lengo la kubana watu pumzi, kwa kuhakikisha kwamba ina-control na ku-monitor mfumo mzima wa vyama vya vyote: wafanyakazi, wanafunzi, nk. ni "system" inayokusanya fedha kutoka kwa wadau: wanafunzi (DARUSO, etc.), wafanyakazi (RAAWU, THTU, etc), nk., na kuziwasilisha kwa vyama husika. pia inatoa "ruzuku" ili "kuviwezesha kufanya kazi zake". hali hii inavifanya vyama hivi kuwa na udhaifu wa kimfumo. sheria zote zinazosimamia vyama hivi, zinatungwa na "system" kwa kutumia vyombo vinavyowajibika kwa "system". mara nyingi vyama hivi vinawajibika zaidi kwa "system".

  Kwa maana hiyo, vyama hivi si mali hasa ya wafanyakazi au "wadau", bali ni mali ya "system". inawezekana kupata kiongozi hapa na pale ambaye atapambana na mfumo huu, lakini mazingira yaliyopo hapa nchini hayana mbolea ya "kumwezesha" mtu kama huyo asitawi katika lengo lake. ni rahisi "kuvutwa shati" na kufuata mkondo. process ya kuondoka katika mfumo huo na kwenda kwenye mfumo ambao vyama vya wafanyakazi vitakuwa kweli ni vyama vya wafanyakazi, ni process ya mapambano dhidi ya "system". inahitaji hao wafanyakazi wenyewe wakae pamoja na kutafakari mustakabali wao, na kuamua kuwa na vyama vyao. tunahitaji kuzingatia yafuatayo:

  1. kujiunga kwa wingi katika vyama hivyo, na kuwatambua watu mashujaa ambao wapo tayari kupambana lolote na liwe.
  2. kuwaweka madarakani mashujaa hao, na kuwapa nguvu na mamlaka. nguvu hiyo ni umma uliowaweka madarakani. hivyo wakiitisha mgomo, unaitikiwa kwa wingi.
  3. Kurudia utaratibu wa zamani ambapo matatizo ya wanafunzi wa vyuo vikuu yaliwagusa waalimu, matatizo ya walimu yaliwagusa wanafunzi, matatizo ya walala hoi yaliwagusa wafanyakazi, wasomi na watanzania wote. kazi ya ukombozi Africa nzima ilikuwa wajibu wa kila mtanzania, kila mzalendo na kila mjamaa. basi tunaposikia wakulima wanapunjwa mazao yao, tuone kwamba hilo ni tatizo letu linalotakiwa kushughulikiwa na kila mmoja wetu. tunaposikia dhahabu yetu inatoroshwa, vyama vyote viuingane kupinga.
  4. Kuwa na dira, au itikadi inayotuunganisha watanzania wote. kwa utaratibu huu wa kila kipande cha chama kupigania maslahi yake tu, hatufiki popote. ifike mahala tukisikia kuna mtu kafukuza watu katika nyumba fulani wanakaa nje, kuwe na vyombo vingi tu vinavyohoji hilo. ikitokea kuna kiwanda kinanyanyasa wafanyakazi wake, ifikie mahala kuna chama cha walaji kitaitisha mgomo wa kugomea bidhaa za kiwanda hicho. na hata kama wanategemea kuuza nje tu, kampeni inapigwa kimataifa pia.
  5. Wadau wamiliki vyama vyao, na kuviwezesha. kwa sasa watu wanakata tamaa kwa kufikiria kwamba hata wakichangia vyama hivi, pesa yao inapotea bure. tufike mahala tutambue kwamba kila mtu peke yake hakuna mafanikio. tunatakiwa kutumia both formal and informal ways. taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria zina umuhimu wake, lakini kwa pamoja tuazimie kuhakikisha taratibu hizi zinakuwa kwa maslahi ya wengi.
  6. Kuna vyama kama UDASA, ambavyo sio Trade union, lakini ni more powerful than a trade union (RAAWU, THTU), hasa ikipata watu wenye moyo wa kupambana kama akina marehemu Prof. Chachage. sijasema waliopo hawafai.
   
 14. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wafanyakazi ni walipa kodi wakubwa sana, katika mazingura ya kawaida wanalipa zaidi ya asilimia arobaini ya mshahara. Mathalani kama PAYE ni 30% na VAT ni 18%, kwa uchache kodi hizi mbili tu zinagharimu walau 42% ya mshahara wa mfanyakazi, achilia mbali kodi nyinginezo.
  Kwa hili, ni jukumu la vyama vya wafanyakazi kuhakikisha kuwa fedha hizi za kodi zinatumika kwa maendeleo ya nchi na wananchi (provision of public services) na si vinginevyo. Namshangaa huyu Mgaya na wengineo wapo kimya angali kodi zetu zinafujwa (e.g. sitting allowances, etc).
   
 15. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,784
  Likes Received: 1,970
  Trophy Points: 280
  wafanyakazi badhi yao ni mabepari hasa hasa wale ambao ni viongozi wa vyama hivi vya wafanyakazi kwahiyo ni ngumu kwa wafanyakazi waonewa kuwa na mshikamano kutokana na kuona kuwa mwisho wa siku viongozi wao ndio wa kwanza kuwasaliti. Viongozi wa vyama hivi wangesimama angalau kwenye mafundisho ya Karl Marx na mwenzake Fredrick Engeles wafanyakazi wengi wangejiunga na kuwa na msimamo mmoja.
   
 16. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
   
 17. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Vyama vya wafanyakazi TZ ni deal na ulaji wa hao viongozi wa chama. Kama siyo kweli basi Mgaya aje atwambie ule mgomo aliokuwa anamtishia JK mwaka jana umeishia wapi??
   
Loading...