lwambof07
JF-Expert Member
- Jul 12, 2016
- 4,593
- 5,202
Habar JF
Wote tunajua kuwa suala la kulea mtoto ni jukumu la wazazi wote baba na mama, hakuna kitu kinaboa na kuchosha kama kuhakikisha mtoto yupo msafi muda wote, wakina mama hubadilisha nepi hadi huchoka na kuamua kuacha tu na kuangalia unakuta dogo nguo yake imeloa mikojo na wengine hadi inaanzia kutoa harufu.
Zishukuriwe pampasi kwa sababu hiyo mtoto akipigwa kuja kumtoa sio leo.
Wababa wengi huwa hawapendi kabisa kuwasafisha watoto wao pale wanapokuwa wameharibu mambo iwe haja kubwa au ndogo ila hasa hasa haja kubwa hii ndogo anaweza akavumilia.
Unakuta baba kashika mtoto au anacheza na mwanaye yaan dogo akishajisaidia tu utamsikia we mama fulani mwanao amejinyea huku njoo umchukue.Baba yeye anapenda kucheza na mwanaye akiwa msafi tu akishaharibu mambo kosa hilo.
Kwani baba fulani ukimsafisha utapungukiwa na nini huwezi kumsafisha mtoto wako hadi umuite mama watoto??au kumsafisha mtoto hilo ni jukumu la mama peke yake baba halimuhusu??