Juice na unga wa ngano kutoka viwanda vya Kenya vitaingia Tanzania bila vikwazo na sementi kutoka viwanda vya Tanzania vitaingia Kenya bila vikwazo

Cement ya dangote ikiwa sirari ni karibu 22000, ukivuka tu upande wa isebania Rai cement ni 11000 tu , labda kama dangote ataamua kuweka kiwanda Kenya
Unazungumzia kipindi alichobanwa kwenye uzalishaji kwa sasa akipata nafasi ya kuzalisha bila vikwazo ana uwezo wa kusambaza mzigo kwa bei nzuri
 
Ni moja ya products zinazotoka kwetu kwenda kenya na kubamba sana zikiwa huko
Japo kuna wakati ziliwahi kurudishwa na kebs pale namanga kwa kuwa quality ilikuwa mbaya. Kwa baadhi ya batches.
Vip kwasasa mkuu, watu hawavushi tena??? Na kama wanavusha kuna utaratibu gani?
 
Ukiachana na nishati, vipi kuhusu mikopo ya riba nafuu huko EU, kupata mkopo wa riba ya 1-3 % huko ni kitu cha kawaida, bongo ni kiwanda gani kinaweza pata huo mkopo, SSH anatengeneza bomu la kujitakia, upuuzi mtupu.
Unapata Mkopo, alafu shughuli za kuwekeza hazipo kutokana na value for money haipo. Unazalisha bidhaaa ambazo haziwezi kushindana
 
Endelea kujidanganya. Mimi naishi Mashariki ya mbali huku na Juice za Azam zinauzwa hadi huku, sembuse Kenya? Kipindi Kikwete anatoka Azam walishaanza kuuza Juice zao Kenya ila mahusiano ya kinchi yaliharibika kipindi cha JPM ndio maana mauzo yalipungua. Haya makubaliano ni neema kwetu. Tatizo watu tumezidi woga. Wakenya ni watu wa kawaida tu.
Na mwambie ssb kapasua mawimbi huko now yupo south africa
 
Tutakuja kujua baadae kuwa hatuna rais, ila wacha tupige miruzi na vigelegele kwa Sasa!

What's going to happen is an influx of Kenyan made goods in Tz, our export will be totally reduced hence decline of our currency due to higher importation of goods than exportation.

Rais huyu anajaribu kuivua chupi nchi ili kila taifa lijipigie litakavyo, soon ujanja ujanja wa Kenya dhidi ya Tz utarudi kwa Kasi.
mkuu
 
Tiles za goodwill na twyford Tanzanzia mara kadhaa nimeshuhudia zikishindwa kuingia kenya kwa sababu ya ubora hafifu, ,
Twyford wana kiwanda kenya lakini products zao ni level za juu kuliko twyford Tanzania

Bila usbishi wakenya wapi vizuri kwenye quality control
Mkitengenezewa zenye ubora mtamudu gharama ya kuzinunua????
 
Hii poa sana. Wajitahidi kumaliza hiyo ya EPA haraka hili tuna na wigo mkubwa wa uchaguzi wa bidhaa. Kwani lini kulinda bidhaa kutaisha? sisi raia wa kawaida tumeshachoka kuwalindia matajiri wa tanzania viwanda vyao. MAMA fungua koki zote hili akili iwaingie wenye viwanda wazalishe bidhaa zenye ubora kukabiliana na ushindani.
 
Kosa kubwa alilofanya Magufuli ni kujaribu kuwazibua masikio wajinga.

Magufuli alikuwa anaongoza taifa la watu wajinga na wapumbavu ambao kwao uccm na uchadema ni agenda yao kuu. Ndio maana kuna mataifa yakikuwa yanasema tupeni sisi huyo mtu atuongoze walau mwezi mmoja tu.

Kila mahali alipokuwa anapita alikuwa anawaambia watu fanyeni kazi, limeni mazao muwe na chakula cha kutosha kisha ziada uzeni nje mpate fedha,! Tena akawambia usipofanya kazi ikija njaa selikali haitakupa chakula itakuacha ufe, ile ilikuwa ni kuwa encourage watu wafanye kazi, ila wajinga wakasema ni mkatili.

Akasema inauma sana kuona unaenda dukani kununua bidhaa toka nje wakati material ya hiyo bidhaa unalala nayo kila siku. Na akijaribu kuwaambia watu wekezeni viwanda vyenu kila kona ya nchi ili muzalishe bidhaa kutokana na material za sehemu husika badala ya kuuza hizo materials kisha mnarudishiwa bidhaa kwa bei juu.

Suala la sukari kwa mfano, ingekuwa nchi yenye watu wenye afya ya akili muda huu tungekuwa tunaongela tuna viwanda hata 20 vya sukari maana alipozuia sukari toka nje wenye mitaji ilitakiwa kwenda kuwekeza kwenye mashamba ya miwa na kufungua maviwanda ili kuhakikisha sasa wanateka soko lote la ndani. Badala yake wakaishia kumtukana.

Magufuli alikuwa anataka kuona badala ya watu kuuza materials na yale materials kurudi kama bidhaa na kuuziwa kwa bei ya juu basi watz wenyewe wafanye yote hayo kisha wauze bidhaa badala ya materials.

Samia anaturudisha kule kule. Yani badala ya kuhamasisha watu wafungue viwanda tuuze na sisi bidhaa yeye anahimiza hivyo vibidhaa vije kwa wingu zaidi. Hatutafika popote.
Hatutafika popote



Sasa mdau unataka tufike wapi???
 
Vip kwasasa mkuu, watu hawavushi tena??? Na kama wanavusha kuna utaratibu gani?
Konyagi inavuka sana tu kwenda kenya , utaratibu ni kuwa Quality iwe ya juu
Konyagi ina alcohol level ya 35%abv , kebs wakipima wakaikuta ina 34.4% imekula kwako inarudi hata kama ulishalipa entry na fees zote.
 
Mkitengenezewa zenye ubora mtamudu gharama ya kuzinunua????
Mkuu hakuna kitu expensive kama counterfeit au low quality products ,
Low quality tiles zitakufanya kila siku ukimbizane na mafundi ku replace hizo zilizopoteza ubora

Ni bora ununue ghali lakini mara moja kuliko kurudia rudia
 
Hakuna maendeleo bila ushindani...na faida zake ziko wazi...Kama nchi kiwango cha mapato kitaongezeka kupitia Kodi itakayokuwa inalipwa kupitia bidhaa zinauzwa na tozo mbali mbali... Idadi ya wateja imeongezeka...
Sasa ni karibu ya watu milioni 120....hivyo uzalishaji na ajira vitaongezeka....bei za bidhaa zitashuka....lakini pia tutapata bidhaa bora..... mfano mzuri ni makampuni ya simu....miaka ya nyuma tuliuziwa line mpaka alfu kumi...leo line buku...lakini mbona hata Sasa ushindani upo... Azam cola...mo cola...coca cola...Pepsi....huko kwenye maji ya kunywa ndio usiseme....lita 1.5 sasa ni mia tano tu....unga wa ugali hivyo hivyo...bia leo mpaka buku jero....Kvant ....Konyagi....na kina Faru john....tuache uoga.... tena itatusaidia kwenye kupanua uelewa na ugunduzi....ukiwa mzembe biashara inakufa....tena hata hawa Tanesco watafutiwe mshindani.... hawaeleweki kabisa.
 
Naona jamaa anapenda sana Del Monte juice ila kwa kukusaidia ni kwamba Del mounte Iko kiwanda Kenya na Tanzania pia kipo ila asili yake ni USA na kuwekezwa mara ya kwanza South Africa

Ila ninachoweza kusema zote nimewahi kunywa lakini bado Azam naikubali ( Tropical Azam)
So vitu vikae sokoni tujichagulie
Offcorse mimi ni Mzalendo wa bidhaa za ndani Sitaacha Azam tropical kwa kweli sijaona mbadala wake.

Kwenye maziwa fresh yakiruhusiwa Azam ataumizwa na Brookside milk kwa sababu ya bei
Brookside 2000 ubora uko juu
Azam 3500 sina uhakika sana

Ushauri wangu tuunge mkono bidhaa zetu za ndani zile ambazo kwa kweli zina ubora.
Kwa sababu Kenya wanaweza kuamua kutengeneza bidhaa fake za kuja huku wakijua mtanunua kisa hamtaki vya kwenu.
True bado azam naona ni juice Bora kabisa kwangu
 
Una endorse mkataba wa EPA na EU, sisi tunapeleka nini EU hadi uruhusu bidhaa zote za EU ziingie Tz duty free ? Huyu ndio Rais atakayeua kabisa manufacturing industry ambayo ndio kwanza ilikuwa jnaanza kukomaa baada ya kazi ya muda mrefu ya Mkapa, JK na JPM.
Seek truth from facts. Don’t jump onto conclusion. Mkuu, Hope unajua kwamba sasa EAC ni soko moja na tuna sheria moja ya forodha
 
Back
Top Bottom