Juhudi za Pinda za kujisafisha machoni mwa Watanzania


BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
82,027
Likes
121,422
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
82,027 121,422 280
Date::3/4/2010
Pinda awakaanga wakuu wa mikoa

*AWAITA DODOMA, AWATAKA WAJIELEZE KWA DAKIKA TANO

Habel Chidawali na Tausi Masanja, Dodoma
Mwananchi

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewaita na kuwaweka kiti moto wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kwa kuwataka kila mmoja kueleza namna alivyojipanga kukabiliana na kushuka kwa elimu nchini na maafa ya mvua za El-Nino.


Kila mmoja alipewa dakika tano kueleza mikakati yake ya mbele na leo wakuu hao wa mikoa watakuwa na kibarua kingine kwa kueleza namna walivyojipanga kuhusu mambo ya elimu ikiwemo ufaulu wa wanafunzi.


Waziri Mkuu Pinda amewaita wakuu hao wa mikoa wakati mikoa ya Dodoma, Morogoro na Kilimanjaro, ikiwa inatibu majeraha ya maafa yaliyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika baadhi ya maeneo yake.


Maafa hayo yalitokea Same, Kilimanjaro na kusababisha kaya 1,000 kukosa makazi na kati ya hizo, 960 ni za Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na zaidi ya 30 Dodoma, huku Same nyumba nne zikiwa zimeharibiwa. Akiahirisha Mkutano wa 13 wa Bunge, mwaka juzi Pinda alisema kuanzia wakati huo wakuu wa mikoa na wilaya wangepimwa kwa vigezo vya mabadiliko katika sekta za maendeleo ya wananchi, hasa kilimo na kuongeza uzalishaji.


Akitoa maelekezo jana katika mkutano huo unaowahusisha wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa yote ya Tanzania Bara unaofanyika katika Ukumbi wa New Dodoma Hotel mjini hapa, kibarua kilikuwa ni kwa wakuu wa mikoa ambao walisimamishwa mmoja baada ya mwingine kueleza mikakati yake. Kila mmoja aliposimama alielezea namna walivyojipanga kukabiliana na mafuriko yaliyotokea na yanayoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini hivi sasa.


Tofauti na mikoa mingine, ilipofika zamu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alimwambia waziri mkuu kuwa pamoja na mafuriko hayo, lakini hawezi kuwalazimisha wananchi wa jiji hilo kuhama katika maeneo yao na badala yake ataendelea kuwashauri tu. Lukuvi alisema mwaka huu (mwaka wa uchaguzi) umekaa vibaya hivyo hawezi kubomoa nyumba za wakazi wa jiji hilo.


Hata hivyo mkuu huyo alisema tofauti na wakuu wenzake, yeye mkoani kwake huwa hazungumzii suala la njaa hivyo akajikita katika suala la afya. Alisema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo katika Jiji la Dar es Salaamu ni jinsi ya kuondokana na ugonjwa wa kipindupindu.


Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Enos Mfuru alisema chanzo cha mauaji ya watu 17 yaliyotokea hivi karibuni ni mbuzi 25 ambao waliibwa kabla. “Mheshimiwa Waziri Mkuu sisi pamoja na suala la mafuriko, lakini kwetu kuna tatizo la mafuriko mengine ambalo linatokana na mauaji ya kulipiza kisasi katika koo zinazohasimiana,” alisema Mfuru.Mkuu huyo alisema kuwa kutokana na mauaji ya watu hao 17 tayari jeshi la Polisi limekwishawatia mbaroni watu 9 ambao wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo na kwamba watafanya kila liwezekanalo ili wahusika kamili waweze kupatikana. Hata hivyo Pinda aliilaumu Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) kuwa wanafanya kazi kwa mashaka na kwamba, wanawachanganya wananchi.


“Hawa jamaa hata mimi nashindwa kuwaelewa sijui ni kwa sababu ya vitendea kazi duni au nini, maana wanawachanganya wananchi.


Hadi leo watu hawajui kama mvua hizi ni za El-Nino au bado kuna mvua zingine kwa kweli taarifa zake zinachanganya,” alisema kwa ufupi. Waziri mkuu jana alikuwa tofauti na siku zote ambapo aliingia akiwa mwenye furaha na kuanza kwa utani ambapo aliwataka wakuu wa mikoa pamoja na makatibu tawala kujua salamu ya CCM.


“Lazima na ninyi mjifunze salamu za Chama Cha Mapinduzi. Tunaposema kidumu Chama Cha Mapinduzi mjue namna ya kupokea sio mkiambiwa basi mnamung’unya maneno na kujificha.
Haya CCM hoyeee!” alisema Pinda. Wakati akijumuisha taarifa za kutoka kila mkoa aliwataka wakuu wa mikoa hiyo kusimamia kikamilifu matumizi ya ardhi katika maeneo yao na kusimamisha kilimo cha mabondeni, ambacho alisema kwa kiasi kikubwa kimechangia mafuriko yaliyotokea Kilosa, mkoani Morogoro.
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,674
Likes
5,076
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,674 5,076 280
Hana haja ya kuwaita, si tumeona humu picha kibao zinazoelezea hali halisi ya elimu.

Kujieleza kila mmoja atajieleza vizuri kwa kumridhisha PM.

Atembelee huko au ambane waziri wake wa elimu( ambaye naamini ndio ilikuwa kazi yake hiyo).Pia wao kama serikali lazima waangalie part yao, kama kutenga bajeti, kuanzisha shule zisizo na waalimu n.k

shule nyingi za remote hazina walimu, na hakuna anayetaka kwenda huko. serikali ifanye mkakati wa kuwalipa watu kulingana na umbali kutoka mijini ( au kutafuta mfumo wowote wa kuwahamasha walimu kwenda huko vijijini)

suppose mtu amemaliza chuo kulikuwa na umeme, tv, n.k leo anapangiwa shule sehemu ambayo haina hata umeme au miundo mbinu inakuwa vigumu kwa huyu mtu kwenda.
 
B

Boramaisha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
820
Likes
7
Points
0
B

Boramaisha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
820 7 0
Sidhani kwamba Pinda ana sababu yoyote ya kujisafisha. Kwa uchafu gani alionao?
 
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
7,370
Likes
1,618
Points
280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
7,370 1,618 280
Sidhani kwamba Pinda ana sababu yoyote ya kujisafisha. Kwa uchafu gani alionao?
Pinda amejipaka najisi ambayo asipojisafisha atanuka muda wa uwaziri mkuu wake wote uliobaki!! Pinda anajiita mtoto wa mkulima, amekwenda Igunga jimboni kwa fisadi papa RA na kuwaambia wananchi kuwa wasisikilize yale yanayozungumzwa bungeni kwani yote ni POROJO NA UZUSHI!! Amewaambia kuwa mbunge wao ni mtu safi kwahiyo wamrudishe bungeni mwezi October!! Haya ni maneno yanayomuweka Pinda kundi moja na mafisadi na ndio maana anawaogopa na kudiliki kusema kuwa wakikamatwa nchi itatikisika; huyu bwana anakibarua cha kujitakasa kwa maneno yake ya kuutetea ufisadi na kulikashifu BUNGE!!
 
JoJiPoJi

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2009
Messages
2,706
Likes
2,095
Points
280
JoJiPoJi

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined Aug 8, 2009
2,706 2,095 280
salam za chama tena kwenye vikao vya serikali,, kweli huu mwaka dume
 
S

samvande2002

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2009
Messages
414
Likes
12
Points
35
S

samvande2002

JF-Expert Member
Joined Mar 6, 2009
414 12 35
mh, kazi ipo; kwanza haina haja ya kuwaita wakuu wa mikoa kwenda dodoma, ni kuongeza gharama kwa taifa. kwa mawazo yangu, pinda kama waziri mkuu alikuwa anatakiwa ku deal na waziri wa elimu tu juu ya poor perfomance ya wanafunzi. waziri husika ndio angetakiwa kuwa responsible zaidi.
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
Hana lolote..Kujieleza ni fursa ya kujitetea lakini pia dakika tano mtu ataeleza nini?
 
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
5,971
Likes
46
Points
0
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
5,971 46 0
Juhudi za Pinda za kujisafisha machoni mwa Watanzania- as understood by Bubu Ataka Kusema

Pinda awakaanga wakuu wa mikoa- as understoond by Mwananchi's writers

Pinda akutana na Ma RC dodoma as understoob by mtazamajiSwali what should be the unbiased heading of the content ?
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
14,623
Likes
9,235
Points
280
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
14,623 9,235 280
..yaani unamuita Mkuu wa mkoa toka kituo chake cha kazi mpaka Dodoma halafu unampa dakika 5 kujieleza? this doesnt sound right to me.
 

Forum statistics

Threads 1,250,989
Members 481,550
Posts 29,753,440