Juhudi za miaka 100 za CPC zina maana gani kwa nchi za Afrika?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
VCG111164721339 (2).jpg

Baada ya kuwa madarakani kwa miaka sabini na mbili, sasa Chama cha Kikomunisti cha China CPC kinaongoza nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani. Kikao cha 6 cha wajumbe wote cha Kamati Kuu ya 19 ya CPC kilichomalizika hivi karibuni, kimejumuisha jinsi kilivyoiongoza China kupata maendeleo ya uchumi na utulivu wa jamii, juhudi ambazo zina maana kubwa kwa nchi za Afrika.

Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania Profesa Humphrey Moshi aliandika makala kwenye gazeti la The Guardian la nchi hiyo, kuwa CPC siku zote inaunga mkono utaratibu wa pande nyingi, kuchukulia “usawa na udhati” kama msingi wa uhusiano kati ya China na Afrika, na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana na nchi za Afrika.

Mwezi Aprili mwaka 1955, mkutano wa Bandung wenye maana ya kihistoria ulifanyika. Kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani zilizotolewa na hayati waziri mkuu wa China Zhou Enlai zilifungua ushirikiano wa nchi za Kusini na uhusiano wa kisasa kati ya China na Afrika. Baada ya mkutano huo, China na Afrika zilianza kujenga uhusiano wa kiwenzi wa aina mpya. CPC iliziunga mkono sana nchi za Afrika kupambana na ukoloni na kutafuta maendeleo ya kujitegemea, huku vyama mbalimbali vya kisiasa vya Afrika vikijifunza uzoefu na maarifa muhimu kutoka kwa China.

Tayari ushirikiano kati ya China na Afrika ulikuwa umepata maendeleo, na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC lililozinduliwa mwaka 2000 liliinua uhusiano kati ya pande hizo mbili hadi kwenye kiwango cha juu zaidi, cha sekta nyingi zaidi na cha kimkakati zaidi. Katika miaka 20 iliyopita, China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika, na mwaka 2019thamani ya biashara kati yao ilifikia dola za kimarekani bilioni 208. China imejihusisha kwenye sekta mbalimbali za ujenzi wa miundombinu barani Afrika, na kutoa msaada mkubwa katika mambo ya usafiri, mawasiliano ya simu, maji safi, nishati n.k. Katika kupambana na janga la COVID-19 ambalo limewaua watu zaidi ya milioni 5 duniani, China pia imetoa msaada mwingi kwa Afrika.

Lakini kwa nchi za Afrika, nafasi ya China sio tu ni mwenzi wa kidiplomasia au nchi inayotoa msaada wa kiuchumi, bali pia maendeleo yake yana maana kwa nchi za Afrika. Moja ya maana hizi ni kushikilia uongozi wa CPC na kutoa kipaumbele kwa maslahi ya watu. Mfumo wa kidemokrasia mashinani umehakikisha kuwa watu wana haki za kutoa maoni juu ya masuala yanayohusu maisha yao, huku utaratibu wa kuchagua watu mashuhuri wa ngazi ya juu unahakikisha watu wenye vipaji vya uchumi, sayansi na uhusiano wa kimataifa wanaongoza nchi na kutoa maamuzi sahihi katika kutunga sera za taifa. Cha muhimu zaidi ni kuwa hii inahakikisha siasa na sera zinakuwa endelevu, jambo ambalo ni muhimu kwa nchi za Afrika. Pili, kama CPC, katika kuongoza nchi kutunga sera za kiuchumi na kijamii, nchi za Afrika zinapaswa kufanya uvumbuzi kwa nadharia zilizopo, kutoa maamuzi kwa kujitegemea na kufuata njia ya taifa lenyewe. Ingawa China imejifunza uzoefu na mitindo ya nchi za nje katika kujiendeleza, lakini sio kama inaiga moja kwa moja, bali inatunga sera zake kwa mujibu wa historia, utamaduni, jiografia na siasa. Aidha, CPC inashikilia kujifanyia mapinduzi, kwa mfano China imeshughulikia vizuri suala la ufisadi, ambalo bado ni tatizo sugu linalokwamisha maendeleo ya Afrika.

Mapema karne ya 20, CPC ikiwa ni chama kidogo chenye wanachama wapatao 50 kilianza safari yake ya miaka 100 ya kwanza, sasa kinaingia kwenye miaka 100 ya pili na kuongoza nchi inayowajibika na kujenga dunia. Katika siku za baadaye, CPC inatarajiwa kushirikiana na nchi nyingine na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom