Juhudi za kuwatetea Ngeleja na Malima KUHUSU UADILIFU WAO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Juhudi za kuwatetea Ngeleja na Malima KUHUSU UADILIFU WAO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndinani, Nov 28, 2011.

 1. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Toka ripoti ya Jairo ijadiliwe bungeni na mapendekezo yake kuwekwa bayana ,kumekuwepo na juhudi za makusudi za hawa wabunge wawili wakiwatunia waandishi wa habari mamluki kutaka kuwasafisha kuwa zile milioni nne nne walizokomba kama entertainment allowance ilikuwa halali yao.
  Juhudi hizo zinajionesha waziwazi kwenye gazeti la mwananchi la tarehe 28/11 ambapo mwandishi anadiliki kusema kanuni na taratibu zinaruhusu hawa watu wapewe hiyo posho bila kiwango!!

  Tatizo la hawa jamaa sio kana kwamba they were not entitled to entertainment allowance la hasha; hizo fedha zingekuwa ni entertainment allowance ya halali zingekuwa properly budgeted for, hivyo zingekuwa na baraka ya hazina kitu ambacho hizo za Jairo hazikukidhi masharti hayo. Hawa kama viongozi wa wizara walitakiwa kulijua hilo na kama hawakulijua basi hawafai kuwa mawaziri!

  Huyu Malima nadhani tabia ya kutokuwa muadilifu ni hereditary; baba yake pia alituibia sana alipokuwa waziri wa fedha enzi ya Mwinyi kabla ya kwenda kuunda chama cha NRA ambako ndiko mwanae alikotokea kabla ya kujiunga na CCM!!
   
 2. P

  Panda Kapesi JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 284
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Duh!
  Nakubaliana na wewe lakini hapo pa kurithi ufisadi toka kwa baba yake nadhani umekwenda too far!
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mwananchi limeanza kupoteza heshima kwa kasi ya ajabu.
   
 4. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama ni kinyume na sheria, washtakiwe mahakamani. Kama ni vinginevyo mjadala uishe..

  Watu wamesign na kubariki mikataba feki and they got away with it, na sasa wanajisafishia njia ya kwenda Ikulu. Itakua hizo paDM zinazotambulika kihalali? Si kuwa nasupport lakini ni vigumu kumng'oa mtu kwa kigezo hicho, lets just face the reality!
   
 5. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  kumbe wanapenda uwaziri alafu wanafanya madudu.
   
 6. peoples power

  peoples power JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 468
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mtoto wa nyoka ni nyoka tu, hivi mlitegemea nini hapo kwa huyo kilaza malima zaidi ya ufisadi kama wa baba yake.shame on him:juggle::juggle::juggle::juggle:
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  ukweli lazima usemwe hadharani tena kwa sauti kuu. Wengi wanajua kuwa Kighoma Malima alikufa kwa shinikizo la damu, baada ya akaunti zake za benki za nje ya nchi kufungwa tena na kiongozi wa Tz ya leo. Na huo uwaziri ni kama fADHILA TU KUPOOZA MACHUNGU YA KUULIWA BABAKE!
   
 8. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndiyo maana watu hawana na imani na tume tunazoziunda, yaani kila kitu kipo wazi lakini wahusika hawachukuliwi hatua labda tunasubiri malaika Gabriel au Jibrili kwa Kiislamu aje amuwajibishe Ngeleja na Malima.
   
 9. nyengo

  nyengo JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Yaani mpaka sasa Jairo na Ngereja hawaja achia ngazii!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hiyo tume hatuna imani nayo nashauri tuiundie tume.
   
 11. M

  Mzee Kijana JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 748
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 80
  Umeanza vizuri arguments zako na pengine kuna ukweli ndani yake. Lkn hapo kwenye red ndipo ulipoharibu. Nayakini tukikupa kazi ya kuthibitisha wizi wa baba yake (Marehemu Prof. Kighoma Ali Malima) huna chembe ya ushahidi hata mmoja zaidi ya dhana tu.

  Kama una concrete and solid evidence za wizi of the late Prof. zimwage hapa jamvini. Tafadhali mwache yule Mzee apumzike kwa amani.
   
 12. U

  Umsolopogas JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Heredit is all about genes my friend, and genes never lie. Labda kama mtoto wa kuazima
   
 13. K

  Kachest Senior Member

  #13
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wale sio rahisi kuachia ngazi labda JK ajiajibishe otherwise tulie tu.
   
 14. k

  kimeta cha ufisadi JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ooooh wadau wangu Ngeleja na Malima ni kweli hawana hatia, yenye hatia ni KATIBA tuliyo nayo, hebu ktk katiba mpya ijayo wayazingatie hayo, WAZIRI hana power kwa mfumo wetu uliopo.kuhusu posho mbona hata Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuuMzumbe hakiingia kwenye kikao cha senate hulipwa 850000 sembuse kwa mawaziri jamani? mlitaka waziri akawalaze wageni wake kwenye HOSTEL za UDOM.Poa bwana naomba kuwasilisha.
   
 15. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
   
 16. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
   
 17. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pumba kwenye red highlight.
   
 18. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hadithi za abunuas hazitatusaidia. Tuongee na kuandika fact daima hatutapotea.
   
 19. m

  matawi JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Don't worry about gazeti. Likiendelea kubowa watu wataacha kununua including wewe mwenye gazeti atatafakari na mwishowe atagundua dhambi yake
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwani Malima na Ngeleja si mafisadi? Baba yake Malima hakuwa fisadi? Hakupata mshtuko wa moyo alipokuta akaunti yake ikiwa tupu London? Tupe facts basi.
   
Loading...