Juhudi za kukuza kilimo lazima ziendane na soko huria

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,804
1,871
Sera za kuendeleza na kukikuza kilimo ni lazima ziwe sera za kitaifa (zisizobadilika) na si sera za chama au hisia za Rais aliyeko madarakani.

Kilimo ni biashara na ili ifanye vizuri na kuvutia watanzania wengi ni lazima iwe wazi kuwa itakuwa kwenye soko HURIA, bei ijipange yenyewe kutokana na demand na supply. Pia mwenye mali ndie mmiliki na aweza kuuza popote ndani na nje ya nchi. Lazima tumthamini mkulima.

Kuna mwanasiasa mmoja mwaka 2015 katika kampeni zake za kugombea Urais alikuwa anasema: Kipao mbele chake namba 1 ni ELIMU, namba 2 ni Elimu na namba 3 ni Elimu. Alishabikiwa na wapenzi wake kwa nguvu sanaaa. Nikasema, huyu kashiba- Hivi utasoma ukiwa njaa! Jibu unalo mwenyewe na hilo jibu ndio kigezo cha kuweka kipao mbele.

Mwl Nyerere alisema, yupo tayari kwenda Afrika kusini kuomba chakula kama Tanzania kuna njaa. Wakati huo nchi hiyo ilkuwa chini ya wabaguzi na Tanzania iliiwekea vikwazo A. kusini mpaka kwenye passport za TZ haikuruhusiwa kwenda huko.

Waziri Bashe yupo sahihi, kilimo ni biashara hivyo kumbana mkulima kwa kudhani anachokipata ni mali ya Taifa si sahihi. Kama tunataka kukiendeleza kilimo tumuache mkulima ajitanue na awe huru, na si wewe uliye Kariakoo umpangie bei, ni yeye ndie akupangie bei.
 
Back
Top Bottom