Juhudi kubwa zimechukuliwa katika kuimarisha sekta ya mawasiliano Zanzibar ili iweze kusaidia kukuza uchumi na shughuli za kijamii

Sep 8, 2020
67
133
#MAWASILIANO.

Juhudi kubwa zimechukuliwa katika kuimarisha sekta ya mawasiliano Zanzibar ili iweze kusaidia kukuza uchumi na shughuli za kijamii.

Mafanikio yaliyopatikana wakati wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ni kama ifuatavyo:

1. Kuanzisha Wakala wa Mkongo wa Mawasiliano Zanzibar ambao unasimamia uendeshaji wa Mkongo wa Taifa kibiashara pamoja na kituo cha kutunzia kumbukumbu za kimtandao (Data Center) kwa Zanzibar.

2. Kuendeleza uunganishaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye majengo 84 ya Serikali.

3. Kuimarisha mawasiliano kwa kuuza uwezo wa ziada wa matumizi ya mkongo kwa sekta binafsi.

4. Kufanya mapitio na kuuimarisha Mkongo wa Mawasiliano.

5. Kukamilika kwa ujenzi wa vituo 10 vya huduma za mawasiliano ya mtandao kwenye wilaya zote za Zanzibar kwa matumizi ya jamii.

Kwa kipindi cha mwaka 2020-2025, CCM itaielekeza SMZ kutekeleza mambo yafuatayo;

1. Kujenga kituo mbadala cha kuhifadhia taarifa (Disaster Recovery Centre).

2. Kujenga miundombinu ya TEHAMA pamoja na kushajiisha matumizi ya TEHAMA kwa jamii.

3. Kutanua matumizi ya mkongo wa Taifa wa mawasiliano kuwa wa kibiashara.

4. Kuboresha na kuimarisha kituo cha sasa cha “data center” kwa kuondoa vifaa chakavu na kuweka mifumo mipya.

Tunaomba KURA yako kwa ajili ya Mawasiliano salama na rahisi kwa miaka mitano ijayo.
#ChaguaDr.Mwinyi,
#ChaguaDr.Magufuli
 
Back
Top Bottom