Judge Joseph Sinde Warioba ana hisa Celtel??

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Wakuu,

Nina swali,Je Jaji warioba ana hisa katika Kampuni ya Celtel? There is a story I have here mpaka naanza kuogopa.

Inasemekana alikuwa ni mmoja wa watu wa kwanza kuwa wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Celtel na ninajaribu kujua alikuwa akiiwakilisha serikali au na yeye ni mwana hisa?

Ukikumbuka, kampuni ya Celtel haikuwahi kutumia pesa yake kuanzisha kampuni hiyo ambayo hivi karibuni itabadili jina na kuitwa Zain.

Mie nataka kujua kuhusu hili.

Connecting to the dots...
 
Wawekezaji kwenye nchi zetu hutafuta watu wenye political connections na kwaingiza kwenye bodi zao za wakurugenzi.

Kazi yao si kuwekeza bali kupenyeza rupia pale inapobidi, kunapotokea na pingamizi katika miradi yao. Ndio maana Msekwa alipewa Vodacom wakati wa vita dhidi ya ukiritimba wa kuhodhi mawimbi wa Mobitel.

Ukichunguza utagundua pia kampuni yake ni mwakilishi wa kisheria wa makampuni ya madini!!!!

Any dots missing?
 
kama akiwa na hisa, kwani kuna tatizo gani? ni watu wa nje tu ndo wana sifa za kuwekeza? yaani kuwekeza kwa mtz ni dhambi tena wakuu? mimi mwenyewe ni mwana JF lakini nikipata chance celtel au popote pale siwezi kuilazia damu. kwani kuna kosa gani kuwekeza.
 
Tatizo siyo kuwekeza ,ila mazingira ya wao kuwekeza ndiyo yanatia shaka,Iweje Kampuni imetoka Nje na itafure Mtanzania wa kuwasaidia kupata pesa.Je unajua Celtel ilianzishwa vipi?

Suala la Pili ni kuhsu hizo pesa wamezitoa wapi kuwekeza katioka Makampuni makubwa.Ndiyo maana Mwalimu alishwahi kuuuliza Ukwasi alionao Mamvi aliiutoa wapi?
 
Wawekezaji wana uhuru wa kuchagua wajumbe wao wa bodi kutokana na sheria za nchi zilizopo. Kigezo kimoja katika sheria hizo ni kuwa kuwepo na angalau mjumbe mzawa. Wawezekezaji wanatumia fursa hiyo kutafuta watu wenye ushawishi na watakaofanikisha interest zao. Biashara ndivyo ilivyo.

Na si Warioba tu, alianza Dr.Salim A.Salim, tena akiwa body member wa MSI. Kwanini Dr.Salim A.Salim alikuwa "favourable" candidate? Kwa sababu ya influence yake toward governments in Africa. Utakumbuka early 2000s, ndio alikuwa ametoka AU (former OAU) na alikuwa na links/relationships with many African leaders, na hii imesaidia sana MSI/Celtel kuenea/penetrate kwa haraka within African countries.

Tatizo si Warioba, tatizo ni sisi na sheria zetu.
 
Nani alitengeneza Sheria zetu kama siyo hao hao???
 
Judge Warioba ni mjumbe wa bodi ya TTCL, akiwawakilisha Celtel International. Serikali nayo inawawakilishi wake kwenye hiyo bodi.....kama sikosei Celtel wana hisa 35% na serikali 65%....hivyo wote wana haki wa kuchagua wawakilishi wao!

As for yeye binafsi kuwa na hisa Celtel...zein..hapana hana!
 
Mkuu Gembe hili la wawekezaji mimi linaniuma kichwa sana maana sasa hatuletewi wawekezaji ila tunaletewa wachukuaji maana hakuna anayeonekana kuleta kwetu bali kuja kukwapua. Kipima Joto cha ITV kimeuliza swali zuri sana leo, mwekezaji kupewa reli ya kati kumetimiza lengo? hii inatokana na ukweli huu huu kwamba yaonekana hawa viongozi wetu wanatengeneza wao sheria za kuhakikisha wanakula bila tatizo.
 
Judge Warioba ni mjumbe wa bodi ya TTCL, akiwawakilisha Celtel International. Serikali nayo inawawakilishi wake kwenye hiyo bodi.....kama sikosei Celtel wana hisa 35% na serikali 65%....hivyo wote wana haki wa kuchagua wawakilishi wao!

As for yeye binafsi kuwa na hisa Celtel...zein..hapana hana!
Kigoma asante kwa habari ulizotupa,kumbe ni member wa bodi ya TTCL pia?

so far yeye ni au alikuwa

1.Mjumbe wa Mwananchi Gold Minning
2.Mjumbe wa TTCL akiwakilisha Celtel ina maana ana hisa TTCL(kwa upeo wangu ninahisi kuna fact hapa)

Swali ambalo nitaka kujua ambalo ninahisi kumekuwa na uzugujai mkubwa sana kwa watanzania,Je ni nani alikuwa Mwenyekiti wa ile Tume ya Rushwa aliyounda Mkapa?
 
Nani alitengeneza Sheria zetu kama siyo hao hao???

Kutambua tatizo ni mwanzo wa kutatua tatizo.

Mwanzoni umeanza hoja hii kwa kulaumu, ukasahau pia tuna tatizo kubwa sana kwenye sheria zetu. Na sheria zetu tunazitunga sisi wenyewe, kupitia kwa wawakilishi wetu, ambao wewe ukiwa mmoja wapo wa wanaowachagua. Sasa unasemaje sheria zinatungwa na "wao" ?
 
kama akiwa na hisa, kwani kuna tatizo gani? ni watu wa nje tu ndo wana sifa za kuwekeza? yaani kuwekeza kwa mtz ni dhambi tena wakuu? mimi mwenyewe ni mwana JF lakini nikipata chance celtel au popote pale siwezi kuilazia damu. kwani kuna kosa gani kuwekeza.

Mkuu,

Tatizo ni kwamba hawa watu tayari wana ajira zao na hawapaswi (kulingana na maelekezo ya tume ya maadili ya viongozi) kuwa na aina ingine ya kipato na wasilifahamishe Bunge au serikali kwa ujumla.

Ila hakuna tatizo kwa mtanzania wa kawaida ambae hana majukumu kama ya viongozi hawa, kuwa na hisa katika makampuni hayo yanapokuja kuwekeza Tanzania.

Pia sheria inawaruhusu investors kutafuta local partners ambao kwa bahati mbaya ni wale viongozi na watu wenye vyadhifa, ambao tayari wamekwishaiba na wanajipanua kibiashara na kunyima nafasi wananchi wa kawada kufanya hivyohivyo.

Sasa kikubwa zaidi ni kwamba makampuni yoote uchwara yanayokuja kwa mgongo wa uwekezaji, yanakuwa hayana mtaji wa kutosha na hivyo kuwekeana mikataba na serikali na kuchukua sehemu yote ya mtaji wa mashirika hayo ambayo yalianzishwa kwa kodi za wananchi miaka hiooo! yalipoanzishwa, je huo sio wizi?

You see what I mean mate!
 
Kigoma asante kwa habari ulizotupa,kumbe ni member wa bodi ya TTCL pia?

so far yeye ni au alikuwa

1.Mjumbe wa Mwananchi Gold Minning
2.Mjumbe wa TTCL akiwakilisha Celtel ina maana ana hisa TTCL(kwa upeo wangu ninahisi kuna fact hapa)

Swali ambalo nitaka kujua ambalo ninahisi kumekuwa na uzugujai mkubwa sana kwa watanzania,Je ni nani alikuwa Mwenyekiti wa ile Tume ya Rushwa aliyounda Mkapa?

Connection yako ya dots ina walakini. Kwa hiyo unataka kusema mtu kuwa mjumbe wa bodi hizo anakuwa ni mla rushwa ?
 
Connection yako ya dots ina walakini. Kwa hiyo unataka kusema mtu kuwa mjumbe wa bodi hizo anakuwa ni mla rushwa ?

Mkuu Korosho..

sijasema anakuwa ni mla Rushwa ila anaweza kuwa miongoni mwao wala Rushwa...
 
Kwa muda mrefu sasa hivi nchi yetu imekuwa na katabia ka wakubwa na wastaafu kupeana ULAJI kwa kuchaguana kwenye BOD(Board of Directors). Lakini ukiangalia Good Corporate Governance practices zinaweka wazi kuwa political figures kama wabunge, mawaziri n.k wasiwe wajumbe wa BOD ili kuepuka muingiliano wa Maslahi.

Kwa nafasi ya warioba kwa sasa ambaye si mmbunge, waziri au hata decision maker katika serikali ya sasa hawezi kuwa na undue influence so kuwa mjumbe si tatizo mradi tu awe anafit katika nafasi hiyo na sio Rubber Stamper, yaani anahudhuria vikao kwa ajili ya posho lakini hana analolijua. Pia kuhusu kuwa na Hisa (stocks or Shares) Si tatizo kwa mtu yeyote provided hela aliyotumia kuinvest ni ya kwake kaipata kihali na si ufisadi. Kwani kuwa na mradi si dhambi kama umepatikana kihalali.

Cha kujadiliwa hapa ni kwamba je ana share kiasi gani na kazipate, ni Bonus shares, lobying shares au amenunua shares DSE. Ila tuskurupuke na kuanza kujadili kitu ambacho hakina details wenye details mwageni hapa tuanze kuchambua kwa kutumia theories mbalimbali ikiwepo shareholders' theory, Corporate Governance theories etc
 
Kutambua tatizo ni mwanzo wa kutatua tatizo.

Mwanzoni umeanza hoja hii kwa kulaumu, ukasahau pia tuna tatizo kubwa sana kwenye sheria zetu. Na sheria zetu tunazitunga sisi wenyewe, kupitia kwa wawakilishi wetu, ambao wewe ukiwa mmoja wapo wa wanaowachagua. Sasa unasemaje sheria zinatungwa na "wao" ?

Tatizo wale tunaowachagua wanakosa umakini,kuna kosa kubwa sana wapinzani na wabunge na wapinzani wamelifanya na kupitisha moja ya sehria moja ambayo italeta madhara makubwa sana kwa baadaye..

Nilishawahi kumbwambia zitto,ila mpaka leo amekaa kimya kwa sababu alipigwa butwaaa kwanini hakuliona/hawakuliona hili mapema na Sheria ilishapita na inasubiri mkulu kuanguka.Ninahisi hawna muda wa kutosha kupitia hizi sheria au hawajui sheria vizuri..Je kuna haja ya Wananchi kama wao kupitia sheria hizi kabla hazijapelekwa Bungeni ili wao kuamua nini.

nitaliandikia siku nyingine,nimewapa muda wa kulirekebisha..
 
Kwa muda mrefu sasa hivi nchi yetu imekuwa na katabia ka wakubwa na wastaafu kupeana ULAJI kwa kuchaguana kwenye BOD(Board of Directors). Lakini ukiangalia Good Corporate Governance practices zinaweka wazi kuwa political figures kama wabunge, mawaziri n.k wasiwe wajumbe wa BOD ili kuepuka muingiliano wa Maslahi.

Kwa nafasi ya warioba kwa sasa ambaye si mmbunge, waziri au hata decision maker katika serikali ya sasa hawezi kuwa na undue influence so kuwa mjumbe si tatizo mradi tu awe anafit katika nafasi hiyo na sio Rubber Stamper, yaani anahudhuria vikao kwa ajili ya posho lakini hana analolijua. Pia kuhusu kuwa na Hisa (stocks or Shares) Si tatizo kwa mtu yeyote provided hela aliyotumia kuinvest ni ya kwake kaipata kihali na si ufisadi. Kwa kuwa na mradi si dhambi kama umepatikana kihalali.

Cha kujadiliwa hapa ni kwamba je ana share kiasi gani na kazipate, ni Bonus shares, lobying shares au amenunua shares DSE. Ila tuskurupuke na kuanza kujadili kitu ambacho hakina details wenye details mwageni hapa tuanze kuchambua kwa kutumia theories mbalimbali ikiwepo shareholders' theory, Corporate Governance theories etc

Ndio mkuu,

Lakini napingana na wewe kwani Jaji Warioba ni mwanasheria kitaaluma na ntakubali tu ikiwa yeye atakuwa ameajiriwa kama mshauri wa kisheria wa kampuni hio.

Cha kujiuliza hapa ni je yeye ni major au minor shareholder na aliweka stock kiasi gani?

Na kama ameingia kwenye kampuni hio akiwa shareholder na ana direct or indirect equity interest kwamba hajishughulishi sana na uendeshaji wa kampuni hio?
 
Hauoni kama unamchafulia tu mshikaji? Mbona inaonekana kama vile mtu ukiwa na bifu na mtu yeyote, unatakiwa kuja kumuweka kwenye kinywa cha wanaJF ili wamtafune ili kutimiza azma yako kwao?

Is there any regulation which regulates the truth of the allegations put in this JF? u hata mimi nikiwa na bifu na mtu, na nimemshindwa huko mtaani natakiwa nimlete hapa mnisaidie kumkomesha?

Someone explain to me please.
 
Judge Warioba ni mjumbe wa bodi ya TTCL, akiwawakilisha Celtel International. Serikali nayo inawawakilishi wake kwenye hiyo bodi.....kama sikosei Celtel wana hisa 35% na serikali 65%....hivyo wote wana haki wa kuchagua wawakilishi wao!

As for yeye binafsi kuwa na hisa Celtel...zein..hapana hana!

Kigoma,

Utakuwaje board director wa kampuni binafsi bila wewe kuwa na shares? Hapo corporate governance inaelekea hakuna kabisa.

Ningelewa kama angelikuwa board member akiwakilisha serikali, hapo angelikuwa analinda maslahi ya sisi sote.

Nitashangaa kweli kweli kama mtu atakuwa board member wa Celtel huku yeye mwenyewe hana kitu. Unaweza ukawa CEO au Executives wengine bila kuwa na shares lakini sio hao part time board members maana kikawaida hao wapo kulinda maslahi ya wana shares wakiwemo wao wenyewe.
 
Back
Top Bottom