FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,052
- 40,715
Kwa jua tulilonalo hapa Tanzania ambalo ni la uhakika na halina kusua sua,hatuna winter wala spring na upuuzi mwingine kama huo, jua kwetu ni mwaka mzima, UTAJIRI ULIOJE!
Jua ndio chanzo cha awali kabisa cha nguvu kwa kila kiumbe hai (wanyama, mimea nk), ndio chanzo cha nguvu ya nishati zote hapa duniani, iwe umeme maji, umeme wa gesi asilia, umeme jua, umeme wa gesi za wanyama, mafuta ya petrol nk.
Mfano kwenye umeme wa maji, jua huyeyusha maji kwenye mito, maziwa nk. na kuyageuza mvuke ambao hutengeneza mawingu na kisha mvua kunyesha na kujaza mabwawa, ile 'potential energy' ya maji yale ni imetoka kwenye jua. ZAWADI ILIOJE!
Sasa basi tufanyeje kuvuna huu utajiri wa jua?
1.) Tulime sana, tena sana, ni dhambi kubwa kuliacha jua linamwagikia chini na ardhi ipo, mimea ina 'solar panel' za asili (majani) ambayo yanauwezo wa kudaka nguvu ya jua na kuihifadhi kama chakula, hapa kwetu almost kila kitu kinakubali, iwe mchele, iwe mahindi, iwe korosho ya yule mbunge alielia kama mtoto, iwe karanga, iwe matikiti, zabibu, nyanya, vitunguu, pilipili, karoti, daah, yaani hadi raha hapa Tanzania, na amani ya kumwaga, BARAKA ILIOJE!
2.) Tufuge wanyama sana tena sana!
Wanyama wengi huwa wanakula majani hivyo kuikamata ile nguvu yote ya jua iliyodakwa na majani na hivyo huhifadhi nguvu ya jua katika mfumo wa nyama. Kwakweli ni aibu kuacha majani yenye nguvu nyingi toka kwenye jua yakauke na kuoza, hiyo ni pesa nyingi sana tunaitupa, huo ni utajiri tunauacha unamwagikia chini, fuga hata mbuzi tu, yaani na jua lote hili linalomwagikia chink utakuta lisomi linazunguka na mavyeti likitafuta ajira kwa wahindi, USHENZI ULIOJE!
3.) Tujenge mabwawa makubwa tena mengi, yaani mengi!
Nashangaa huu udhaifu wa kuogopa watu wa mazingira juu wa ujenzi wa mabwawa ulitoka wapi, Tanzania inapoteza matrillion ya shilingi kila mwaka kwa kuacha maji ya Rufiji yakimwagikia baharini bila kuzalisha umeme, ule ni utajiri, tusiache utajiri wa jua umwagikie chini jamani, ni dhambi kubwa sana, STIEGLER'S GORGE DAM project ni utajiri unaokuja, MW 2100 ni mabilioni mengi sana kila mwaka, MRADI ULIOJE!
4.) Bila kusahau tuwekeza sana kwenye umeme wa Solar unaovuna jua moja kwa moja, biogas, gesi asilia na mengine...., je, unafahamu na zingine za kuukinga utajiri huu unaomwagikia chini?
================================

Uzinduzi Mradi wa Umeme, mto Rufiji: Rais Magufuli aagiza sehemu ya Selous kuwa Hifadhi ya Taifa. Fedha zilizorudishwa kutoka Kenya kujenga barabara
Leo Julai 26, 2019 Mhe. Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi kwenye uwekaji jiwe la msingi la mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji Rais Magufuli aliwasili Rufiji akitokea Dar es Salaam akitumia treni ya reli ya TAZARA kwa kupitia Fuga na Kisaki UPDATE: Waziri wa Nishati, Medard Kalemani...
www.jamiiforums.com