Jua limepatwa?

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Jamani angalieni jua dakika hii angani.
Ni kama limezungukwa na mduara mkubwa kama ule wa rainbow.
Wataalamu tuelezeni ni nini hiki?
 
Kwa wakazi wa Dar... Angalieni jua muda huu wa saa 7 kasoro limezungukwa na kivuli kikubwa na rangi ya rainbow kwa pembeni... Je kwa wajuzi wa mambo LIMEPATWA?

attachment.php
 
nendeni kwenye google, kuna watu kutoka sehemu mbali mbali duniani pia wame-report. ila hakuna maelezo ya kutosha
 
Mkuu ulikua unatafuta nini huko juu? nina miezi 5 sasa tangu nitazame kwa mara ya mwisho.
 
Nimesoma kwenye mtandao wanasema ni hali inasababishwa na jua kuwa karibu na mawingu yaliyoganda na kuwa barafu ambayo inareflect na kutoa huo mwanga kulizunguka jua. Hiyo hali inaitwa "Halo around the Sun" uki-google utapata maelezo zaidi
 
Ni hali ya kawaida hiyo mimi niliiona mara nyingi miaka ya mwanzo wa tisini na kwenye miaka ya 95 na 96 na nilishawahi kupita katikati ya rainbow iliyoshuka mpaka kugusa ardhi ilikuwa saa 12:30 asubuhi nakumbuka, ilinitisha baadae nikaona ah ni hali ya kawaida ya kijiografia, kama hujazoea lazima uogope!!
 
Mkuu ulipita katikati ya rain bow?
Nakumbuka wakati tupo wadogo tuliambiwa ile rain bow aka upinde ni joka kubwa sana.
 
Back
Top Bottom