JUA LA UTOSI MSTARI WA TROPIKI YA KANSA

NTEGEYE Jr

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
322
500
Kutokana na Mzunguko wa Jua la Utosi (The Overhead Sun, ingawa kiuhalisia sio Jua linalozunguka juu ya uso wa Dunia), Jua la Utosi liko maeneo ya kusini mwa mstari wa IKWETA, kwa maana nyingine kesho tarehe 21 Juni 2017 ni Summer Solstice. Kwa kifupi Summer Solstice ni kwa wakati huu (Joto kubwa Ulaya) na Winter Solstice ni Desemba (Joto kubwa Kusini mwa Afrika).

Hali hiyo husababisha idadi ya saa ambapo mwanga wa Jua huonekana hapa Duniani kupunguza kadri umbali unavyoongezeka kutokea maeneo ya mstari wa IKWETA kuelekea Ncha ya Kusini mwa Dunia na huongezeka kutokea maeneo ya mstari wa IKWETA kuelekea ncha ya Kaskazini. Kama inavyoonekana kwenye Ramani hapo chini.

Ndugu zetu Waislamu waishio katika mji wa Punta Arenas Nchini Chile katika bara la Amerika Kusini wanafunga kwa saa 10 (kuanzia saa 12 na dakika 34 asubuhi hadi saa 11 na dakika 41 jioni. Katika jiji la Nairobi, wanafunga kwa saa 13 (kuanzia saa 11na dakika 15 asubuhi hadi saa 12 na dakika 32 jioni).

Kwa wale waishio katika Mji wa Nuuk huko Greenland, wanalazimika kufunga kwa saa 21 (kati ya saa 24 kila siku yaani kuanzia saa 8 na dakika 24 usiku wa manane hadi saa 5 na dakika 14 Usiku.

Hii ndio Jiografia. Tunaweza pia kuongeza ufahamu hapa. Naamini Dr. Noorali Jiwaji na wataalam wengine
 

galindas

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
985
1,000
Kuna watu hawajui tofauti hii ya muda. Zipo nchi nyingine wanaendeshwa kwa masaa na sio kuchomoza kwa jua. Unaenda kulala kwa sababu ni muda wa kulala na sio kwamba giza limeingia.
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,861
2,000
Kama inavyoonekana kwenye Ramani hapo chini.


Hiyo ramani iko wapi??? Weka picha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom