Jua haki yako ukiwa barabarani ukishikwa na trafiki.

LOOOK

JF-Expert Member
May 17, 2011
3,389
672
UMEWAHI KUKAMATWA NA POLISI BARABARANI?


Je, umewahi kukamatwa na polisi wakati ukiendesha gari, pikipiki au baiskeli?
zijue haki na wajibu wako !
Bila kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani kutakuwa na vurugu katikabarabara zetu.
Soma na ujifunze kanuni, Sheria Mpya za Barabara – iwapo kila mmojaatazifuata sote tutafika tunapokwenda kwa urahisi na usalama zaidi. Polisi wana kazi ngumu na muhimu sana ya kutekeleza sheria. Lazima kushirikiana nao,isipokuwa kama wanatenda kinyume na sheria.

Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati ganianakusimamisha uwapo barabarani.

Mamlaka ya kusimamisha gari lako:
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako – kamaatakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani – pia anaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).
Leseni ya kuendesha gari:
Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako yakuendesha gari – anaweza kukataa fotokopi – hata hivyo, unaweza kuamua kupelekaleseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa.Ili kuepukamatatizo, wakati wote tembea na leseni yako kwenye gari (RTA s.77).
Hati ya usajili:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili – gari lazima liendane na maelezo yakwenye kibandiko, lakini vitu vidogokama rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).
Leseni ya barabarani, na bima ya gari:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama umebandika leseni halali ya barabarani nakibandiko cha bima kwenye kiwambo cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).
Kunyang’anywa:
Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseni isipokuwa kwa mujibu wa sheria.
Mikanda ya kiti ya usalama:
Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima mfunge mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari iwe inatembea au imesimama) – unatendakosa kama unaendesha wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria wote wafunge mikanda.
Kuendesha baada ya kunywa pombe:​
Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe (kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi cha pombe kwenye damu yako ni zaidi ya kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na hatiaya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).

Kutumia simu ya mkononi wakatiunaendesha:
ingawa sheria haikatazi hili mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la “​
kuendesha kwa uzembe” (RTA, s.42, s. 50).
Mwendo kasi:
Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa Ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) – ofisa wa polisi anaweza kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unaweza kupinga ushahidi wake mahakamani (RTA s.51, s.73 (2)).
Kustahili kuwepo barabarani:​
Ofisa WA polisi ana haki ya kukagua Kama gari lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki, taa, indiketa na usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri –unawezakutakiwa kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa magari wapolisi (RTA, s.39.1, s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.

KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU KWAMBA UMEFANYA KOSA: Mara nyingi utapewa uchaguzi wa kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 20,000 kwaofisa wa polisi, au kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka. Ofisa ataandika maelezokwenye Fomu ya Polisi ya PF 101, na nyote wawili mtatia saini – kamwe usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu iliyotiwa saini. Unaweza kwenda Na ofisa kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo. Kama unakubali kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA, s.95).
KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIAYOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisianakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishikwa Ofisa Msimamizi Mkuu – ambaye atachunguza na kujibu.
Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu –usitoe rushwa na usipokeerushwa.​


Unaweza ukapenda kukata maelezo haya na kuyaweka kwenye gari lako – lakini kumbukakwamba ni mwongozo tu.
 
Na hawa Askari wa TiGo (Manyigu) Husumbua sana watu na kazi yao ni Kuomba Rushwa tu wakikushika wanakupeleka hadi Kituoni tena sometime huwaweka watu lookup ili kuwatisha watoe rushwa kubwa

pia husumbua hadi mitaa ya ndani ndani ambayo huwa haina ajali wala msongamano, Kazi yao ni Kutafuta rushwa kama ni askari wa barabarani basi na wao wakikuta foleni kubwa wasaidie kupunguza misongamano kwa kutoa maelekezi ya kitrafic, wao wanapenya penya tu na kutokomea sidhani kama wana faida yeyote barabarani zaidi ya kuleta karaha kwa waendesha magari na pikipiki. Wakakamate Majambazi tu na Bunduki zao Migongoni... Watu huwa wanachoka wamekuwa too much.

Mnatubana kwenye kodi,Road Licence Maisha magumu imekuwa kama unamziba mtu pua,mdomo na masaburi atashindwa kupumua
 
Na hawa Askari wa TiGo (Manyigu) Husumbua sana watu na kazi yao ni Kuomba Rushwa tu wakikushika wanakupeleka hadi Kituoni tena sometime huwaweka watu lookup ili kuwatisha watoe rushwa kubwa

pia husumbua hadi mitaa ya ndani ndani ambayo huwa haina ajali wala msongamano, Kazi yao ni Kutafuta rushwa kama ni askari wa barabarani basi na wao wakikuta foleni kubwa wasaidie kupunguza misongamano kwa kutoa maelekezi ya kitrafic, wao wanapenya penya tu na kutokomea sidhani kama wana faida yeyote barabarani zaidi ya kuleta karaha kwa waendesha magari na pikipiki. Wakakamate Majambazi tu na Bunduki zao Migongoni... Watu huwa wanachoka wamekuwa too much.

Mnatubana kwenye kodi,Road Licence Maisha magumu imekuwa kama unamziba mtu pua,mdomo na masaburi atashindwa kupumua

mkuu kuhusu hwa tgo kwakweli ni zaidi ya usumbufu ucoelezeka kabisa kila k2 wanajua wao wanakwambia ni kazi maalumu wanafanya kazi zote wanakagua bima,roadlicence, matairi , leseni ila kuandika notification awawezi mpaka wakupeleke kwa trafik
 
Naomba kufahamu:

1. Afisa wa polisi (traffic) - baada ya kukusimamisha barabarani - nawe ukatii - JE ANA HAKI YA KUCHOMOA SWITCH YA GARI LAKO - TENA KWA HASIRA - NA MANENO MENGI YA VITISHO? - kama nitakupeleka mahakani............... lete leseni .............lete kadi ya gari - HUKU AKIRUKA RUKA KUONYESHA JASBA - HASIRA NA VITISHO??? HATIMAYE KUINGIA NDANI YA GARI LAKO NA KUANZA KUONGEA KWA UPOLE NA KUANZA KUOMBA RUSHWA??????

2. Hata kama ni kwenda KITUONI - NI LAZIMA AINGIE NDANI YA GARI YAKO UMPE LIFT KWENDA KITUONI???

JAMANI NAOMBA MSAADA - UKIFANYIWA HIVYO UCHUKUE HATUA GANI???


ASANTE
 
shule hii ni nzuri ila tatizo ni pale unapokumabana na polisi aliye kunywa damu ya rushwa na ikajaa ndani ya akili yake hata kama anajua si kosa analazimisha kuwa kosa
 
je notification inalipwa hapo hapo au unalipia kituoni? Na kama ni kituoni ni lazima umwachie polisi ufunguo wa gari ukalipe kwanza ndo uchukue ufunguo wako? Au akishanipa notification natakiwa niende mwenyewe ni kalipie ndani ya muda fulani?
 
Asante mkuu, ila naomba kuuliza. Mimi siku moja nilishikwa na hao kunguru weupe, akakagua kila kitu akakuta kiko fresh, mwisho akaniruhusu kuondoka ile nataka kuondoka akanizuia akaniambia nioneshe fire extinguisher, nikamwambia haipo, telemka ulipe faini, nikawambia sina hela ( ni kweli sikuwa na hela) nilikuwa na sh 5000 tu kwenye mkoba, akaniambia acha gari ukatafute hela sh 20,000 uje ulipe ndo utachukua gari yako, je hii ni sawa kumwachia trafiki gari ukatafute hel ya faini?
 
Kunyang'anywa:



Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseni isipokuwa kwa mujibu wa sheria.
hiyo sheria inasemaje? What's the point of putting up some sloppy "mwongozo" ambao unakurudisha tena kwenye "isipokuwa kwa mujibu wa sheria," sheria inasemaje?


Mwendo kasi:


Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa Ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) – ofisa wa polisi anaweza kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unaweza kupinga ushahidi wake mahakamani (RTA s.51, s.73 (2)).​

Na kama sio eneo la hatari speed mwisho ngapi, speed of light? Na kama hakuna alama utajuaje wapi ni eneo la hatari? Hii nayo ni crap.
 
Mie hua siilewi hii RTA nahisi irekebishwe.
Kuna kifungu cha kulipia licence kila baada ya miaka mitatu mitatu...lakin ilitaja iwapo hujailipia miaka mitano itakua haifai tena ku-renew ie malipo...ikasema iwapo kwa sababu maalum.

Na nmeona hizo Act hua na huo usemi ''iwapo'' au '' bila'' sasa hapo kwanini isiwe wazi?

Hua nashindwa kuelewa hizo kanuni za enzi izo!.
 
Kma unaweza tafadhali weka hapa hii sheria ya matumizi ya barabara/traffic act n regulations zake tuisome wote
 
Naomba kufahamu:

2. Hata kama ni kwenda KITUONI - NI LAZIMA AINGIE NDANI YA GARI YAKO UMPE LIFT KWENDA KITUONI???

ASANTE

Ndugu yangu, nilishaweka nadhiri, kamwe trafic aliyenikamata hatopanda kwenye garui langu niende nae kituoni. Aliyemuajiri akamate watu barabarani na kuwapeleka kituoni ampe na usafiri, na hii ninawafanyia trafic wote. Nakumbuka kipindi hiki cha sikukuu, kuna trafic alinikamata nikiwa na gari ya mdogo wangu tulibadilishana yeye kachukua yangu aende nayo mkoani, alikagua kila kitu kikawa safi, kasoro kadi ya gari ilikuwa photocopy iliyothibitishwa na TRA ambayo yeye aliikataa akawa anataka original card, ukweli ni kwamba najua photy copy iliyothibitishwa ni halali, sijui ni kwa nini trafic huyu aliikataa, hivyo nilimpigia simu ndugu yangu aniambie original ameweka wapi, at the time nampigia simu hakupokea hivyo teafic huyo akaniambia twende kituoni akataka kupanda gari langu.

Nilichofanya nilifunga milango ya gari, nikamwambia utanikuta kituoni na mimi siwezi kumpakia yeye kwenye gari lango,ilikua hapo akiba hivyo aliniambia niende makao makuu. Alikasirika sana, akamwita mwenzake mwenye pikipiki anifate, nilimuacha hapo nikaenda kituoni, bahati nzuri kabla sijafika kituoni ndugu yangu alinipigia simu kunielekeza kwamba aliweka kadi ya gari chini ya kiti, hivyo trafic alipofika kituoni akiwa amevimba kwa hasira ya kumnyima lift, akaanza kufoka, lazima ulale ndani, unajifanya mjanja, na blabla nyingi sana me nikamuacha tu aongee amalize, alipomaliza nikamwambia bahati nzuri mwenye gari amenipigia na kunielekeza kadi ilipo, hii hapa hivyo sina kosa niachie niende.

Hakuwa na cha kunikamata tena, alibaki kulalamika tu. Kifupi hakuna haki ya kumpakiza trafic aliyekukamata kwenye gari lako, akikugeuzia kibao ndani ya gari akuteke je?
 
usisumbue akili za watu, traffic wanachotaka ni pesa tu, hamna kingine, na huwezi kushindana nao...wakikusimamisha kuwa mpole tu, usijifanye mjanja, watakupotezea muda wako bure.
 
Back
Top Bottom