JPM Waite Wanafalsafa Na Wanasheria Wakusaidie Mantiki Ya Siasa

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,058
Tatizo la nchi hii ni kwamba mambo mengi yamevurugwa kinyume na misingi ilivyojengwa tangu uhuru.
Somo la siasa lilikuwa likifundishwa shuleni na vyuoni zamani, tena siyo kwamba lilikuwa likifundishwa mwaka wa uchaguzi pekee.

Leo lilikuwa ni kuwajenga wananchi kuwa na fikra pana kuhusu uvumilivu wa kisiasa, uhuru wa wananchi ikiwemo uhuru wa kutembea na kujumuika.

Somo la siasa lilitufundisha kwamba maendeleo yanatokana na kukosoana pamoja na kuhimizana kufanya kazi. Na jukumu hilo siyo la Rais peke yake, pia siyo tunda la msimu kama embe dodo.

Naamini somo hilo hakulisoma sana kwa kuwa alitaka kuwa mwanasayansi. Ni wakati wa kuwaita wataalamu wamsaidie maana hata Mwl. Nyerere anayemtaja alikuwa mwerevu wa siasa na ndiyo maana alipendekeza vyama vingi.

Bring Back Our Democracy
 
Kuna haja hata marais wastaafu wakajitosa kumshauri.inaonekana katika baraza zima la mawaziri wanaogopa kumshauri kwa weledi kwa kuhofia nyadhifa zao.ufike muda rais aambiwe wazi anakotupeleka siko.tusisubiri maafa yatokee ndo tutafute suluhu.
 
Tatizo la nchi hii ni kwamba mambo mengi yamevurugwa kinyume na misingi ilivyojengwa tangu uhuru.
Somo la siasa lilikuwa likifundishwa shuleni na vyuoni zamani, tena siyo kwamba lilikuwa likifundishwa mwaka wa uchaguzi pekee.

Leo lilikuwa ni kuwajenga wananchi kuwa na fikra pana kuhusu uvumilivu wa kisiasa, uhuru wa wananchi ikiwemo uhuru wa kutembea na kujumuika.

Somo la siasa lilitufundisha kwamba maendeleo yanatokana na kukosoana pamoja na kuhimizana kufanya kazi. Na jukumu hilo siyo la Rais peke yake, pia siyo tunda la msimu kama embe dodo.

Naamini somo hilo hakulisoma sana kwa kuwa alitaka kuwa mwanasayansi. Ni wakati wa kuwaita wataalamu wamsaidie maana hata Mwl. Nyerere anayemtaja alikuwa mwerevu wa siasa na ndiyo maana alipendekeza vyama vingi.

Bring Back Our Democracy

Wewe huna shule, umeandika vumbi tu hapa. Mantiki ya siasa ipo wazi na hao wanafalsafa wameizungumzia vizuri na tena hakuna mantiki moja kwa wanafalsafa wote, inategemea wewe ni muumini wa nani au nani unayependa mawazo yake kuhusu siasa. Rudi kasome tena halafu uje hapa na mantiki ya wanafalsafa unaowapenda ambao ungependa Rais Magufuli awafuate, hapo utakuwa umejielimisha vizuri na si hasara utajuta kuandika huu utumbo ulioandika hapa kwa kutumia heading nzuri
 
Hakuna lolote
Mlisema Jk legelege
Aliwapa Uhuru wote
Ikafikia wakati mnamtukana hovyo

Leo tumempata dawa ya Wanywa Viroba
Mtulie

Magu kaza kaza bado sana

WATANZANIA HAWATAKI UKUTA
HAWAPAKANI NA SOMALIA
 
Back
Top Bottom