maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Hakuna ulaji mnono uliopata kutokea katika nchi hii tangu uhuru kama huu wa IPTL na mwanae ESCROW.
Ni ulaji ambao ulitengenezwa na kigogo wa vigogo na utazama na gogo la magogo kwa sababu sasa mambo yanaanza kuanikika.
Ufisadi huu ndiyo uliotaka ututumbukize kwenye miaka mingine 10 ya maktaim ya kiuchumi kwa kutaka kumpandikiza mmoja wao awe Rais wetu wa awamu ya tano ili awalindie wezi mali walizoiba.
Niliisha andika mara nyingi huko nyuma kwamba Magufuli asihangaike sana kumtafuta mwizi na wajanja wanaoifilisi nchi hii kupitia IPTL kwa sababu kwa namna yoyote ile na kwa jinsi mambo yalivyosokotana itafika mahali wahusika wenyewe kwa wenyewe watapandishana kwenye stuli, watavishana kitanzi shingoni na watamsimamisha mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ili asimame abitue stuli.
Rais ataibitua stuli taratibu kwa mguu wake wa kushoto na kurudi kuketi kwenye sofa lake kuendelea kunywa Nzagamba ya kisukuma. Wezi wetu watabakia wananing'inia.
Imeishajulikana mabilioni yalifichwa Australia na dogo mmoja wa ukoo wa lililokuwa gogo kuu la ikulu, haina shida siku itafika.
Bila shaka itafika siku akina Servacius Likwelile, Fredrick Werema, Eliakim Maswi, Sospeter Muhongo, Benno Ndulu, Joseph Makandege, singasinga Seth, Mizengo Pinda na hata Jakaya Kikwete mwenyewe watasimama wapaze sauti na watatuambia zilikofichwa pesa zetu walizotuhubiria mpaka bungeni kwamba pesa ile haikuwa yetu, ilikuwa yao wezi mashujaa.
Nafikiri kwa namna gazeti la Mwanahalisi toleo no. 332 la tarehe 28-3 March 2016 lilivyoripoti, sina chembe ya kulitilia shaka litatumalizia kadhia hii kwa kuiendeleza stori hii mpaka mwisho. Niwaombe watanzania safari hii tushikamane tusiogope kinyacho kama ni mitaani tuingie kushinikiza yeyote aliye husika ashtakiwe, hata kama ni Kikwetwe akamatwe maana hatukumchagua aende ikulu kutuibia.
Mliofungwa Segerea na Ukonga jiandaeni safari hii muyapokee magogo siku si nyingi zijazo.
Babu Seya upoooo? Tuandalie virago baba tuko vigogo na gogo nusu dazeni.