JPM aweza Kuwa the worst President of All times?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,019
3,880
Ni swali na mjadala

Kutokana na mfululizo wa kushindwa kipropanda,kisera na hata kiutendaji je kuna uwezekano tukasema kwamba JPM aweza kuwa Rais mwenye kiwango cha chini cha utendaji wa wakati wote?

Tunafahamu kwamba JPM hakulelewa na Mwalimu kisiasa ukilinganisha na Mwinyi,Mkapa na Hata Kikwete.

Tunafahamu kwamba JPM hakuwa mwana mtandao kwa hivyo hakuwa na mkakati wowote wa kisiasa wala ajenda ya kisiasa

Tunafahamu kwamba JPM pamoja na jitihada zake za kujionesha kuwa na Misimamo bado hata tangu akiwa kiongozi alioneka zaidi kuwa mtu mwenye EGO zaidi kuliko Kiongozi mwenye Msimamo.

Tunaona na kufahamu kwamba pamoja na kukaa ikulu miaka minne sasa JPM bado hajaweza kufanya serikali yake kuwa na common Agenda,yaani kila kiongozi ana lake na hakuna mipango na vipaumbele vya kueleweka

Tunaona mambo mengi makubwa ambayo yalionekana kuwa mazuri yameishia kwa aibu ukianza na Makinikia ambalo mpaka sasa linaonekana limemtia aibu kubwa kwani sasa anaomba kwa huruma apatiwe pesa hzo ndogo na sio kudai.

Ukiangalia swala la Korosho limemfanya ajutie kauli yake ya kuwachapa shangazi wa kusini kwani ameishiwa kutapeliwa tena mbele ya uso wa dunia na machalii wa Nairobi

Ukiangalia swala la Elimu bure sasa limegeuka kuwa sanaa

Ukiangalia tatizo la ajira ni bomu ambalo liko mbioni kulipuka

Ukiangalia ndani ya CCM hakuna anayemuunga mkono na wengi wanajikomba ili tu wapate vyeo na basi lakini hawamuungi mkono hata kidogo.Chama kimejaa mamluki kibao.

Ukiangalia kwa Kiasi kikubwa kuna mambo mengi sana ambayo yanashindwa,yameshindwa na yatshindwa kwa awamu yake hii.

Je unafikiri tunaweza kusema kwamba huyu ni mmoja katika ya Viongozi wabaya wa wakati wote kuwahi kutokea katika nchi hii?
 
Korosho
Elimu bure
Ajira

Hii ndo mifano uliyotoa,usiwe bias kwenye thread yako maana imekaa kimipasho flani hivi.Unapokuwa mwandishi jaribu kubalance story leta mabaya yake,wapi kashindwa na wapi kafaulu halafu tupime kweli uyasemayo yana ukweli? Lakini kwa thread yako hii naishia kusema wewe haupo tofauti na waimba taarabu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mwana ccm ila suala la korosho tu ndio naona bomu kweli kweli bora makinikia hayanuathiri mtu direct kitu gani kilimfanya aingie kichwakichwa kwenye korosho kawasababishia watu hasara vyama vya msingi na ushirika havina pesa wasafirishaji hawajalipwa korosho hazijanunuliwa mshaurini mheshmiwa serikali haiwez fanya biashara mwingereza alikuwa bega kwa bega na wahindi yeye anakusanya kodi sasa yeye nani ashindane na wafanyabiashara? Tutaona kampeni ataongea nini kusini.

Yeye kaainisha hayo we njoo ya uyaonayo mema
 
Korosho
Elimu bure
Ajira

Hii ndo mifano uliyotoa,usiwe bias kwenye thread yako maana imekaa kimipasho flani hivi.Unapokuwa mwandishi jaribu kubalance story leta mabaya yake,wapi kashindwa na wapi kafaulu halafu tupime kweli uyasemayo yana ukweli? Lakini kwa thread yako hii naishia kusema wewe haupo tofauti na waimba taarabu!

Sent using Jamii Forums mobile app
binafsi sion alichofaulu hata robo.Labda kama wewe unayo unijulishe maana mimi sioni kabisa hata kwa kuigiza tu
 
Mimi mwana ccm ila suala la korosho tu ndio naona bomu kweli kweli bora makinikia hayanuathiri mtu direct kitu gani kilimfanya aingie kichwakichwa kwenye korosho kawasababishia watu hasara vyama vya msingi na ushirika havina pesa wasafirishaji hawajalipwa korosho hazijanunuliwa mshaurini mheshmiwa serikali haiwez fanya biashara mwingereza alikuwa bega kwa bega na wahindi yeye anakusanya kodi sasa yeye nani ashindane na wafanyabiashara? Tutaona kampeni ataongea nini kusini.

Sent using Jamii Forums mobile app

Halafu ajawahi tembelea kusini atakuja wakati wa shida ( kuomba kura
 
Back
Top Bottom