Watulie tu wasihoji, kwa kuwa Magufuli anatumia unlimited powers alizopewa ndani ya Katiba yetu ya sasa.
Ndiyo maana nasema hao wabunge wa CCM wasithubutu kulalamika, kwa kuwa ndiyo hao kwenye Bunge maalum la Katiba, walidiriki kuitupa kwenye 'dustbin' Rasimu ya Tume ya Warioba iliyotokana na maoni ya wananchi ambayo iliyapunguza sana madaraka ya Rais.
Wao CCM waliamini kwa kuwa na Katiba 'mbovu' yenye kumpa madaraka makubwa sana Rais, ambayo yanamfanya awe kama 'Mungu-mtu' ndiyo itakuuwa kinga ya chama chao.
Sasa kwa bahati mbaya sana kwa CCM na kwa bahati nzuri sana kwa Umma wa watanzania, amepatikana Magufuli ambaye kimwili yuko CCM lakini kiroho yupo Ukawa.
Ndiyo maana zaidi ya 90% ya wanaoisoma namba hapa nchini kwa sasa ni makada wakubwa kabisa wa CCM.
Nami nasisitiza kuwa kutokana na ile dhambi kubwa sana waliyotufanyia waTz ya kututupia kwenye dustbin ile Katiba yetu pendwa iliyokuwa ndani ya Rasimu ya Tume ya Warioba, wacha hiyo dhambi waliyotufanyia waTz, iwatafune wanaccm hadi mwisho wa dunia!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.