Uchaguzi 2020 Joyce Sokombi: Nitaanzisha mfuko wa kusaidia makundi maalum

NCCR Mageuzi

Member
Oct 3, 2007
23
63
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma mjini kupitia chama cha NCCR Mageuzi ndugu Joyce Bitta Sokombi amesema endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ataanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya kusaidia makundi maalumu katika kata za Manispaa ya Musoma ikiwemo wazee na walemavu.

Bi. Sokomi amesema lengo la kuanzisha mfuko huo, ni kuyawezesha makundi hayo kumudu mahitaji yao ya kila siku ikiwemo matibabu ukilinganisha na hali ilivyo sasa hapa nchini.


Aidha Bi Sokombi ameahidi pia kuwezesha ujenzi wa shule ya sekondari ndani ya eneo la Kata ya Iringo kwa lengo la kuwaondolea adha wanafunzi wa kata hiyo, ambao kwa sasa wanasoma katika Shule ya Sekondari ya Nyabisare iliyopo Mtaa wa Nyabisare Kata ya Bweri ambapo ni umbali mrefu kutoka katika kata hiyo.

“Nitatafuta eneo ndani ya kata ya Iringo kuwezesha ujenzi wa sekondari, hii pia itaimarisha usalama wa wanafunzi wetu wa kike kusoma kwa ufanisi, nitahakikisha pia nawezesha ujenzi wa bweni kuwaondolea adha ya kutembeaumbali mrefu”-Alisema ndugu Joyce Sokombi

Jana Oktoba 01, 2020 mgombea ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini ndugu Joyce Bitta Sokombi alifanya mkutano wa kampeni za kunadi sera na kuomba kura kwa wananchi wa Kata ya Iringo Manispaa ya Musoma,
s1.png
 
Back
Top Bottom