Joyce Kiria: Hivi ni nani anampa mamlaka huyu mdada?

ProBook

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
558
257
Wakuu,

Huyu mwanadada amekuwa akiziexpose familia za watu kwenywe Tv na kuwasuta wanaume kama watoto, hata kama ni mwanamke ana makosa atafanya ionekane kama mwanaume ndo mwenye makosa sasa mimi hapa nina maswali machache:

Kwanza, ni nani anaempa mamlaka ya kuamua mambo juu ya familia za watu?

Pili, kwanini haheshimu familia za watu anaexpose mambo ya watu kwenye TV?

Na mwisho, kwanini mwanaume unakubali familia yako ionyeshwe kwa Tv kama kiburudisho kwa wengine?

Huyo Joyce ajifunze kuheshimu privacy ya familia za watu at least ingekuwa anawasaidia bila kuwaonyesha real characters.

Au mwaonaje wadau?
 
tatizo ni aina ya watu anaowafanyia hivyo....
sijui ndo kutojielewa... lakini nahisi anafanya hivyo kwa consent ya hao watu wenyewe sidhani kama anawezaku bump in tu halafu afanye kipindi na watu bila ridhaa yao
 
Sasa huyo mangi aliyebananishwa si alikuwa anajua anarekodiwa?

Walaumu wanaokubali to be exposed kwenye media.

Ila leo mangi kabananshwa hadi huruma.
 
Huyo jamaa toka kile kipindi cha mwanzo nilijua anawalakini sio bure...
 
Nilikuwa nasubiri huu Uzi. Mangi ana shida yule sio bure. Mwanaume familia inakushinda eti unaenda kulia lia kwenye TV. Na kuhusu huyu dada Joyce approaches zake siku zote huwa sio decent anapokuwa anamuhoji mwanaume. Ana ka ubabe flani hivi.
 
Mi nadhani kuna umatemate kidogo unatolewa!mi nimejiandaa na wife kuandaaa Bonge la igizo la ugomvi!bongo Sanaa!in reality hiwezi mjibu mwanaume hovyo Halafu huyo mwandishi akiondoka si Mtu atavunjwa miguu!!the is planned I think an haingii akilini
 
Hao wanaokubali kuwa exposed ndio wenye matatizo. mtamuonea tuu shemeji yetu.
mwacheni apige kazi kwanza yeye ndiye mwanzilishi wa hizo shoo ambazo mabinti kibao na wao wamemuiga kwa kasi.
 
Kwakuwa huyu dada ni mwanachama jf aje ajibu hoja tusiumize vichwa sana
CC ;
Joyce Kiria (Wanawake Live)
 
Nilikuwa nasubiri huu Uzi. Mangi ana shida yule sio bure. Mwanaume familia inakushinda eti unaenda kulia lia kwenye TV. Na kuhusu huyu dada Joyce approaches zake siku zote huwa sio decent anapokuwa anamuhoji mwanaume. Ana ka ubabe flani hivi.

Mangi leo kazingua kabisaaa
 
namkubali sana joyce maana amesaidia ghati chacha wa tarime aliyekatwa mguu na mumewe sasa ana mguu wa bandia na anatembea kama kawida huwezi amini.BIG UP JOYCE KIRIA
 
ilikuwaje?
sijawahi kuona kipindi chake, ila inaonekana kina washabiki, big up, ila pata consent.
pia tafuta 'feel good' situations.
watu wasijisikie wanyonge, wawe proud mwishoni mwa stor, watazamaji na unaowahoji
 
Acheni umasai. Talk show ni kitu cha kawaida kabisa kwenye tv na ilimradi mtu mzima amekubali kupata msaada kwa kufunguka hii haituhusu. Ungekua umeona kina jerry springer si ndo ungepasuka moyo kwa dukuduku?

sijawahi kuona hizo show zake lakini sidhani kama kuna maajabu. Kina Oprah wanahoji mambo magumu hadi unalia ukiangalia, seuze hayo! Mmlaka kapewa na wahusika. Kaa chonjo siku mwenza wako akikufunua ya sirini jasho litakutoka
 
Ila yule mangi sijui kama yameisha pale,inabidi joyce aende tena after one month kucheki kama mama mangi yupo salama!
 
Yaani kufichua ukatili uliokithiri, watu kuuwa wake zao na kuwapa vilema vya kudumu, unasema ni kukiuka Privacy? Wewe mtu wa Tarime usaidiweje? Nataka kuamini kwamba hatuna mtu wa sampuli yako mwingine nchini, wewe ni janga!



Wakuu huyu mwanadada amekuwa akiziexpose familia za watu kwenywe Tv na kuwasuta wanaume kama watoto,, hata kama ni mwanamke ana makosa atafanya ionekane kama mwanaume ndo mwenye makosa sasa mimi hapa nina maswali machache:
Kwanza ,ni nani anaempa mamlaka ya kuamua mambo juu ya familia za watu,?
Pili,kwanini haheshimu familia za watu anaexpose mambo ya watu kwenye TV,?
Na mwisho kwanini mwanaume unakubali familia yako ionyeshwe kwa Tv kama kiburudisho kwa wengine,, huyo joyce ajifunze kuheshimu privacy ya familia za watu at least ingekuwa anawasaidia bila kuwaonyesha real charachers ..
Au mwaonaje wadau,?
 
Back
Top Bottom