Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,296
- 18,892
Mimi naona kama vile approach ya Tanzania kwenye mgogoro wa mpaka ilikuwa ni ya kibabe zaidi kuliko ile ya nchi kubwa kuongea na nchi ndogo jirani kwa jambo linalowahusu wote. Hali hiyo imemfanya mama huyu awe cornered kuwa iwapo atakubaliana na madai ya Tanzania basi itakuwa kama vile aliogopa vile vitisho; na hali hiyo ina complicate process yote. Iwapo tungekuwa na kiongozi wa busara akatuma ujumbe pale Lilongwe na kuongea naye kabla ya kutangaza magazetini huenda mambo yangekwenda tofauti. Iwapo mgogoro huu utakuwa mgumu kutatua, inawezekana zaidi kuwa ni kosa la Tanzania kuliko kosa la Malawi.
Historical documents zilizopo kuhusu mpaka huo, hata kama zinaonekana kuifeva Malawi, ziko against madai ya nchi zote mbili; kwa hiyo ni vizuri wote wawili wakakaa pamoja kumaliza tatizo hilo. Swala la kuwepo mafuta au gesi kwenye ziwa hilo inaweza kuwa ni ndoto tu ambayo huenda baada ya kufanya utafiti na tutakuta kuwa hakuna mafuta kitu au kuna mafuta kidogo sana ambayo thamani yake ni chini ya gharama za kuyachimba. Lakini hayo yanaweza kutokea baada ya kuwa tumeharibu ujirani wetu kutokana na kuwa na viongozi wasiokuwa na busara.
Halafu mwishoni nadhani tatizo jingine kubwa ni ujinga na uzembe wetu waafrika kudhani kuwa tunaweza kunyanyua uchumi wetu kwa kutegemea njia fulani rahisi kama vile mafuta. Tungekuwa na akili kama wenzetu huo Asia ambao wakauza uchumi wao bila kutegema njia yoyote rahisi huenda matatizo kama haya yangekuwa hayatusumbui sana. Angalia Zanzibar inavyozozana na mwezake Tanganyika ambaye wamekuwa nchi moja kwa miaka zaidi ya arobaini lakini kusikia kuwa kuna njia ya mkato inayoitwa mafuta basi kumetokea mgogoro baina yao na wala mwisho wake haujulikani. Nina imani kwa mtizamo huo, hata tukipata mafuta hayo hayatusaidia chochote.