Journalists, Tunaomba kusikia toka kwa Mkapa na Kikwete

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,703
4,697
Matatizo yaliyowekwa wazi wiki hii kuhusu uchimbaji wa dhahabu nchini ni matokeo ya utawala wa Mkapa na Kikwete. Hawa ni wahusika wakuu na haiingii akilini kwamba hawakuweza kujua au hawakutaka kuwatumia wataalamu wetu kuyajua yaliyokuwa yakisemwa na kulalamikiwa.

Mikataba ya madini iliombwa iwe wazi kwa wabunge ikatangazwa na waziri mmoja asiyejulikana kwa sasa yuko wapi kwamba ni siri ya serikali. Vifungu vya kisheria au sheria zikapitishwa bungeni kwa hati ya dhalula. Wananchi wakalalamika na kuna wakati Mzee wa kilalacha akatiwa kashkash kwa kusema Mkapa alipewa pande la dhahabu mgodini.

Lakini juu ya yote haya viongozi hawa wote wawili waliopita hawakutaka kusikia. Je, ni kweli hawakunufaika na udhaifu huu wa mikataba na usimamizi mbovu? Je, waliamini waTZ wote isipokuwa wao ni bweges?

Ni vizuri kwa waandishi wa habari wawatafute watu hawa ili watueleze juu ya tabia hizo.
 
Umenena vyema tusisikilize ya upande mmoja tu, wa baba J. na kamati yake tusikie na ya watangulizi wake.
 
Back
Top Bottom