Joto la siasa za mabadiliko na mustakabali wa Tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joto la siasa za mabadiliko na mustakabali wa Tz

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Membensamba, Nov 5, 2010.

 1. M

  Membensamba Senior Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dr. Slaa na chama chake cha CHADEMA wamezindua zama mpya katika ulingo wa siasa Tz. Ni zama za siasa za mabadiliko. Mabadiliko ya kifalsafa, na kisera yanayotoa mtazamo mpya na dira mpya kwa taifa.

  Kawaida ya mabadiliko huitaji viongozi ambao ni "charismatic" au "transformational" kuyaongoza. Viongozi hawa huwa na mvuto unaosababisha mkondo wenye nguvu wa wafuasi wasioweza kupingwa katika azma yao, kama vile mkondo wa mafuriko ya maji usivyoweza kupingwa au kuzuiwa. Kwa kawaida mkondo huu huvunja kila kizuizi na kupita kuelekea kwenye shabaha yake. Viongozi "charismatic" na "transformational" kama Martin Luther King, Nelson Mandela nk ni mifano mizuri. Hawakukatishwa tamaa na kufungwa, kubezwa, wala chochote. Na ingawa wengine wao walikufa kabla ya kuyaona matunda ya juhudi zao, wamebaki kuwa mashujaa wakuu wa mabadiliko duniani.

  Namtia moyo Dr. Slaa na wote wanamapinduzi, mshike uzi ule ule, hata baada ya uchaguzi mpaka ufisadi uwe historia nchini Tz. Nanyi wana JF, nawaalika kuchangia hoja za kujenga na kuchochea mabadiliko nchini. Hebu tusahau kidogo maumivu tuliyoyapata kwenye uchaguzi. Sasa tuambiane, CHADEMA IFANYE NINI ILI 2015 TUANDIKE HISTORIA? LETE HOJA.
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Ni kweli. Uchaguzi umeisha. JK kaapishwa na kesi imefungwa. Kama kupigwa bao tumepigwa na hakuna cha kufanya. Ukweli unajulikana lakini baada ya siku chache ni wachache watakaokumbuka kuwa JK alirudi kwa njia chafu. Vyombo vya habari vimeishaanza kazi ya kusahaulisha yaliyotokea. Kwa hiyo tunapaswa kufanya "postmortem" ili kupata mafunzo yatakayosaidia katika chaguzi zijazo. Binafsi naomba yafuatayo yaangaliwe kwa umakini:
  1. KATIBA, SHERIA NA KANUNI ZA UCHAGUZI: Huu ndiyo uwanja wa mchezo. Lakini uwanja wenyewe umetengenezwa kwa faida ya mshindani mmoja, ambaye vile vile ndiye mwamuzi wa mchezo. Kama hatutakomaa kubadilisha uwanja matokeo yatakuwa yale yale kila mara.

  2. TUME YA UCHAGUZI: Inajulikana wazi hii tume siyo huru. Ni ya CCM iliyojkaa makada wa CCM kwa faida ya CCM. Hata wasimamizi wa mikoani/wilayani ambao ni watumishi wa serikali nao ama ni makada wa CCM au wanafanya kazi chini ya vitisho kutoka juu ili kukipendelea CCM. Ushahidi ni waraka wa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kwa watendaji wengine. Bila kuifanya hii tume kuwa huru kwa kushirikisha vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi matokeo yatakuwa yale yale na maafa makubwa yataweza kutokea.

  3. CHACHU YA VIJANA: Uchaguzi huu umeonyesha kwamba viongozi vijana ndio wataongoza mabadiliko. Kila chama kijue kwamba huu ni wakati wa kukabidhi mikoba kwa vijana. Kiwatayarishe vijana kwa ajili ya uongozi na kuwahamasisha vijana kwa ujumla kama wapiga kura kwa sababu ndiyo wengi na ndio taifa la kesho kama siyo la leo.

  4. WANAWAKE: Wananawake ni sehemu muhimu ya wapiga kura ni lazima walengwe kwa makusudi kabisa. Vile vile wanawake ni wafahidhina (conservative). Hawabadiliki haraka. Wale ambao wamezoea CCM wanahitaji ushawishi wa ziada kuwageuza ili wawe na mtazamo tofauti. Wanawake mara nyingi wanakwenda kwa makundi ya "ushoga". Lazima kubuni mbinu ya kuwateka wanawake.

  5. DAFTARI LA WAPIGA KURA: Ni wazi kuwa takwimu za wapiga kura zina mshikheri. Ingawa sasa tunafanywa tuamini kwamba watu wengi waliojiandikisha hawakupiga kura binafsi naamni kwamba hilo siyo tatizo pekee. Ni kweli kuwa watu wengi hawakupiga kura kwa sababu majina yao hayakuonaekana. Ni kweli wanafunzi wa vyuo hawakupiga kura kwa sababu vyuo vilifungwa. Pia ni kweli kwamba baadhi ya watu walihama au wamefariki. Lakini hayo yote hayaelezi kiwango cha ukubwa wa tofauti ya kitakwimu. Binafsi naamini kwamba daftari la wapiga kura lenyewe limechezewa kwa kuongezewa idadi kubwa ya wapiga kura feki. Hii ililenga kuhakikisha kuwa kama kura za wagombea zinakaribiana ujanja unaweza kutumiwa kuingiza kura feki na bado hesabu ikabaki haijazidi idadi ya wapiga kura waliojiandikisha (wanaosemekana wamejiandikisha kwa mujibu wa Tume).

  6. MAWAKALA WA VYAMA: Ni vizuri kuwatayarisha mawakala wa uchaguzi mapema inavyowezekana badala ya kungojea karibu na uchaguzi ambapo mawakala wengine wanakwenda bila kujua ni kipi hasa wanasimamia. Napendekeza chama kifundishe wakufunzi wa uwakala ambao kwa Kiingreza wanaweza kuitwa MASTER TRAINERS. Kila wilaya watoke Master Traianers wawili wapewe mafunzo kuhusu sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi na jinsi ya kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi. Hawa wakirudi walilayani kwao ndiyo wawafundishe mawakala watakaopendekezwa mbinu zote za kuhakikisha kuwa kura haziibwi. Mawakala wawe watu wanaoaminkia ambao hawawezi kushawishiwa kirahisi au kutishwa.

  Naomba na wengine mchangie mawazo zaidi au mpeleke mapendekezo yenu moja kwa moja kwa wahusika vyamani.
   
 3. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nakupinga kwenye Introduction yako...Kesi haijafungwa, kesi imefunguliwa...
   
 4. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2010
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  OBSERVERS WAMETOA RIPOTI KUWA ELECTION WAS FREE AND FAIR

  TUSINUNE KWA KUWA KURA ZA SLAA HAZIKUTOSHA, ni kwamba WA TZ WAMEMPA JK!:smile-big:


   
Loading...