Joto kuzidi mwilini

briz

JF-Expert Member
May 8, 2013
4,275
19,109
Habari zenu wanaJF na madoc.

Naombeni mnisaidie hili kama ni tatizo, Mara nyingi joto la mwili wangu huwa linakua kubwa na sa nyingine mpaka wakati wa baridi. mtu ukinigusa unaweza kudhani naumwa lakini sivyo, kuna kipindi nilienda hospitali ila sikufanyiwa hata vipimo nikaambiwa ndo damu yangu ilivyo sasa nashindwa kuelewa ni kivipi?
 
Kupunguza Joto la mwili kunywa Juisi ya Ukwaju mkuu briz

[h=3]FAIDA ZA JUISI YA UKWAJU.[/h]

Tunda la Ukwaju.
Tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.





Juisi ya Ukwaju.

NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU.

Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarkets

  • andaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu
  • baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni
  • uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu
  • ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe
  • andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe
  • weka sukari kwa kiasi unachopendelea
  • pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste
  • weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa

FAIDA YA JUISI YA UKWAJU.


  1. Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)
  2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"
  3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo
  4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni
  5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa
  6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)
  7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)
  8. Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo
  9. Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda
  10. Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

NB: Ikiwa ukwaju na asali havikudhuru, basi changanya hivyo viwili ili kupata faida maradufu!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom