Joto kali mwilini ila kipima joto kinaonyesha chini ya 37 Centigrade

Carina

Senior Member
Jan 4, 2011
190
65
Wadau salama huku.

Mwanangu ana miaka 3 na nusu, inatokea mara kwa mara (kama mara 2 hivi ndani ya miezi 4) anakuwa na moto sana mwilini. Ukimpima kwa ile thermometer joto linaonekana la kawaida tu ( yaani chini ya 37 Centigrade zinazotakiwa).

Nikimpeleka Hispitali (Aga Khan) wanasema ni infection tu ya kawaida. Anapewa madawa anakunywa inaisha ila hii hali inajirudia tena baadaye labda baada ya miezi miwili au mitatu.

Sasa msaada kujua ni kitu gani hiki?

Pili naulizia ni ipi Hospitali nzuri sana kwa watoto kwa hapa Dar es Salaam.

Tatu, namsikia sana Dr. Amir ambae yupo Kariakoo. Naomba kujua anapatikana vipi hasa hasa siku z weekend (Jumamosi na Jumapili) na jee anapokea kadi za bima ya afya.

Nne, ukiondoa Dr. Amir ni nani mwingine dr mzuri wa watoto Kwa Dar?

Asante naomba kuwasilisha.
 
Itakuwa malaria sugu labda maana watoto maskini unamuona anaumwa lakini baada ya muda anacheza
Kampime malaria please
 
Pole sana chief, Dr Amir yuko vizuri sana...pia kuna Dr mmoja yupo pale clinic ya UDSM anaitwa Dr Chacha pia weekends anakuwaga Quality center kwny health center ya TMJ kama sikosei,

Nilikua na mtumia sana huyo na Dr Amir miaka kama mitano iliyopita ss sijui kama bado yupo uende ukamcheki.
 
Wameshahama mule
 
Nashukuru sana Chief. Huwa anakubali bima za afya au ni Cash Cash
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom