Joto Hasira Serikali Moja, Mbili au Tatu Kwa Vizazi na Utaifa Faida na Hasara Zake nini?

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,838
2,000
Nikiwa ndani ya JF huwa ni dalasa tosha kwangu,napata shida sana,najiuliza na kutamani kujifunza na kuelewa hivi ili joto hasira la Muundo wa Serikali iwe moja, mbili au tatu nini faida au hasara ya msingi kwa vizazi [generation] au Utaifa [Nationalism].

Naomba nijuzwe mambo muhimu yafuatayo hapo chini, uenda maono [vision] yangu binafsi na ya zama za kizazi changu na utaifa wangu ukawa tofuati na watanzania wengi.

FAIDA NA HASARA YA SERIKALI
1: MOJA
2: MBILI
3: TATU

FAIDA NA HASARA
1: UTAIFA WA TANZANIA BARA [TANGANYIKA]
2: UTAIFA WA TANZANIA VISIWANI [ZANZIBAR].

Binafsi yangu naamini katika yafuatayo.
Naamini kwenye MUUNGANO,na muungano wa aina gani ninaoamini, naamini na ninatamani sana kama kutakuwepo na Muungano wa Serikali moja.

Na kama ni Plan ya Mungano na nikakutana na changamoto kisha nikatafuta plan B basi itakuwa ni Serikali Mbili ambayo nimezikuta zikiishi kwa mazoea.Na waswahili usema mazoe ujenga tabia na kikabila yangu tunasema TEMU YA MONTO ITANA LYOGHO..

Kwanini serikali mbili?.Moja nitazingatia UKWELI halisia kuwa nimezaliwa na kukuta kuna Tanzania Bara na Tanzania visiwani.Pili binafsi mimi si muumini wa tabia za mazoea kuwa MUUNGANO wetu ni lazima uwe COPY na KUPASTE kutoka kwenye aina fulani ya MUUNGANO Duniani.

Naamini kwenye Muungano UNIQUE unaozinangatia FAIDA kuu pande zote.Mengine ni changamoto [Challange] na TAIFA ni sura ya binadamu inaishi kwa matendo ya sura ya uwanadamu.Binadamu tunaishi kwa kuvumiliana na linapokuja sura ya Muungano wetu ni Muungano wa undungu.Kwa wale wanaotoka Pwani ya Tanzania kama Tanga, Bagamoyo, na Pwani pia wanaotoka nyika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Mwanza, Simiyu, Songea, Mbamba Bay au Kigoma wanajua nini umuhimu wa Zanzibar kwao, kwa kuwa maelfu ya wanandugu zao ni wazaliwa wa Zanzibar kwa damu.

Ebu nambie faida na hasara unazo ziona wewe!!!
 

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
2,670
2,000
Sioni umuhimu wowote wa kuungana na Zanzibar. Bora tungeungana na Malawi, Zambia, Burundi au Rwanda coz kungekuwa na faida kuliko Zanzibar ambayo hata kwa soko tu bado ni soko dogo kwa bidhaa zetu. Kifupi sio muumini wa muungano na wazenji, zaidi zaidi wanatuletea Usumbufu.
 

tpmazembe

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
2,469
1,225
Huu muungano naona kama umekaa kuridhishana tu wala sio kwa ajili ya maendeleo.huitaji kumaliza darasa la saba ili kuweza kujua serikali moja ndio suluhu na maendeleo ya taifa na kuwa na serikali za kikanda zenye magavanor ili kutunza tamaduni za maeneo tofauti katika taifa hili kubwa la Tanzania.

Muungano huu tunaoenda nao 2014 hauna tofauti na jumuiya ya afrika mashariki,maana hata afrika mashariki sasa kusafiri inakuhitaji kitambulisho tu kama uinavoenda kupanda boti kwenda tanganyika au visiwani,hata fedha tutakuwa nayo moja kama ilivyo eac.uraia utakuwa tofauti maana serikali zitakuwa tofauti na kila moja itaangalia maslahi ya watu wake.
 

Sabung'ori

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
2,118
2,000
...muungono tunaohita sasa ni wakiuchumi,hizo sababu nyingene kwa sasa zimepitwa na wakati...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom