Joshua Nassari timiza ahadi yako ya kushusha bei ya sukari Arumeru Masharaki

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wana JF.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari alitoa ahadi kwa wananchi wa Arumeru Mashariki wakimachagua kuwa mbunge wao atashusha bei ya sukari, ni vizuri angeanza na hili la Sukari na wabunge wengine waige mfano kwake.
 
THUBUTU, wenye uwezo wa kutekeleza hiyo AHADI ni CCM tu!
Itamtokea puani labda CCM wamsaidie!
 
Mkinichagua Nitajenga Flyover ubungo, Mwenge,Tazara na Chang'ombe kuondoa foleni.. JE AMEJENGA?Mkinichagua Ntajenga machinga Komplex zingine Tano... JE AMEJENGA?Mkinichagua nitaleta maisha bora kwa kila Mtanzania.... JE AMELETA?Toa kwa Boriti kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako.Waweza kuongezea zingine ....
 
Wana JF.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari alitoa ahadi kwa wananchi wa Arumeru Mashariki wakimachagua kuwa mbunge wao atashusha bei ya sukari, ni vizuri angeanza na hili la Sukari na wabunge wengine waige mfano kwake.

Sukari siyo kero ya wana Arumeru Mashariki kama wewe siyo GAMBA.
Maji ndicho kilio kikubwa kwa wapiga kura hao, kama ulikuwa unafuatilia kampeini za wagombea.
kama aliahidi kupunguza bei ya Sukari itawezekana, maana jimbo lilikuwa CCM miaka 50 yenye dhiki kuu. Nassari MB kaapishwa leo hii unaleta zako zisizo na maana. Mbona Magamba yamekaukia migogoni mwenu tangu siku tisini mpaka sasa mwaka wa pili hata moja hamjalivua au haikuwa ahadi, soma maoni ya wana JF kuhusu maisha bora yaliyohaidiwa na meli pamoja na viwanja vya ndege. Au wewe ni miongoni mwa wale wanaofikiria kutumia....................................Acha ushabiki uchwara.
 
Ahadi alitoa, likini zina kipaumbele, Bei ya sukari ni mfumo ambao wasimamizi wake ni ccm chini ya meya wa Arusha na Mkuu wa Mkoa/Wilaya. Mpeni muda, na tumuunge mkono kufanikisha aliyoahidi
 
Wana JF.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari alitoa ahadi kwa wananchi wa Arumeru Mashariki wakimachagua kuwa mbunge wao atashusha bei ya sukari, ni vizuri angeanza na hili la Sukari na wabunge wengine waige mfano kwake.
Dah! kila mwananchi angekuwa sensitive kama ww tungekuwa mbali
 
Wana JF.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari alitoa ahadi kwa wananchi wa Arumeru Mashariki wakimachagua kuwa mbunge wao atashusha bei ya sukari, ni vizuri angeanza na hili la Sukari na wabunge wengine waige mfano kwake.

Mara hii? Hata ajamaliza siku hata moja bungeni? Umetumwa na sioi?
 
Pia aliahidi atashusha ushuru wa soko, arumeru
Matatizo ya msingi ya wameru ni Maji, Aridhi yote hayo yameanza kufanyiwa kazi hata kabla haja apishwa ....swala la ushuru na ile barabra inayofungwa kila inapo fika saa 12 ni swala dogo sana....na kuhakikishia kama Nassari akienda sokoni akawaambia wafanya biashara msilipe kodi 1000 lipeni 500 au akiamua kuwaambia vunjeni lile gate linalofungwa ili wananchi wasipiti kwenye barabra husika basi wananchi watafanya hivyo....Nassari tumuache afanye kazi zake kwani hata kwenye halimashauri hajaingia bado kiherehre cha nini kwanini hamzikumbuki ahadi za Kikwete....
 
Wana JF.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari alitoa ahadi kwa wananchi wa Arumeru Mashariki wakimachagua kuwa mbunge wao atashusha bei ya sukari, ni vizuri angeanza na hili la Sukari na wabunge wengine waige mfano kwake.
Nasikia alitoa ahadi ya kumuoa Halima lakini katika hali ya kushangaza ameamua kukuoa wewe vipi uko tayari....
 
Tuache ushabiki wa kizandiki hapa, suala la kushusha bei ya sukari, na mengine yanayofanana na hayo ni matokeo ya kufanya restrycturing ya mfumo mzima wa serikali. Kwa mfano, kule Karatu imewezekana baadhi ya mambo kupunguza mzigo kwa wananchi kwa sababu halmashauri inaongozwa na Chadema, kwa hiyo wanaweza kufanya maamuzi ya kumsaidia mwananchi kwa yale yaliyo ndani ya uwezo wao. Kuhusu Arumeru, haiwezekani leo hii Nassari akajiamulia tuu over night kufanya kitu kama hicho, kinahitaji muda na tuombe next election apate madiwani wengi sana ili waongoze halmashauri.
Acheni mawazo mgando.
 
Ndo kwanza kaapishwa na kuwa mbunge halali kwa mujibu wa sheria mmeshaanza kumfatafata, mbona hamlalamiki kuwachimbia visima? Mambo ni step kwa step
 
Wana JF.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari alitoa ahadi kwa wananchi wa Arumeru Mashariki wakimachagua kuwa mbunge wao atashusha bei ya sukari, ni vizuri angeanza na hili la Sukari na wabunge wengine waige mfano kwake.

Acha kumtengenezea kijana ahadi za uongo wewe, alitoa time frame? ulimsikia? mimi nilimsikia alisema atawakilisha matatizo ya wana-Arumeru Bungeni likiwamo suala la mfumuko wa hatari wa upandaji wa bidhaa ikiwamo sukari ili sirikali ichukue hatua za makusudi. Wana-Arumeru wana akili timamu na msimamo mzuri, anagesema kitu ambacho wanajua hakitekelezeki wasingemchagua kwa kishindo.
 
Back
Top Bottom