Joshua Nassari: Maisha yangu yapo kwenye bonde la uvuli wa mauti - Maisha yangu yapo HATARINI Watesi wetu wananitafuta

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
"Maisha yangu yapo kwenye bonde la uvuli wa mauti, Maisha yangu yapo HATARINI. Watesi wetu wananitafuta

nasari.jpg

Nassari: Usalama wangu uko shakani


Siku tatu baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), kuibua tuhuma nzito dhidi ya viongozi wa serikali waliowashawishi madiwani wa chama hicho kujizulu na kuhamia CCM, mbunge huyo amesema maisha yake kwa sasa yako shakani.

“Usalama wangu kwa sasa upo shakani, watu wangu wa karibu, familia yangu na wale wote nilioshirikiana nao kutekeleza jambo hili wote hatuko salama,” alisema Nassari.

Mbunge huyo amesema hayo katika mahojiano maalum na gazeti hili jijini Dar es Salaam yaliyolenga kujua chanzo na mikakati aliyoitumia kufanikisha uchunguzi huo.

Jumapili iliyopita, Nassari na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) waliweka hadharani sehemu ya video inayowaonesha watu waliodai ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkurugenzi wa halmashauri hiyo na katibu tawala wa wilaya jinsi walivyopanga na kufanikisha madiwani hao kujizulu kisha kujiunga na CCM kwa lengo la kumuunga mkono Rais John Magufuli.

Katika mazungumzo yake, Nassari alisema: “Nimebadili mfumo wa maisha, kwa sasa natumia usafiri ambao hauna hadhi kabisa ya mbunge, kuna wakati napanda bodaboda, navaa miwani ili kujiziba watu wasinitambue, natafutwa na kuna mmoja ameshanitumia ujumbe.”

“…hata kuja huku (Dar es Salaam kutoka Arusha) nilitamani kupanda ndege lakini niliogopa, kwa kuwa kuanzia uwanja wa ndege ningejulikana, kwani kuna watu wao hivyo niliamua kutumia njia ya barabara tena kwa usafiri ambao huwezi kuamini anautumia mbunge na kama kungekuwa na usafiri wa bajaji kutoka Arusha ningeutumia,” aliongeza:

Nassari alisema: “Hata hizi simu zangu kwa sasa silali nazo najua wanaweza kuzifuatilia, jana nililala kwingine na simu zilichukuliwa na Halima Mdee (Mbunge wa Kawe-Chadema) na Bulaya (Ester Bulaya- Mbunge wa Bunda Mjini-Chadema).”

Alisema tangu suala hilo litokee, amekuwa akipokea ujumbe na kupigiwa simu na watu wake wa karibu wanaonyesha wasiwasi juu ya usalama wake.

“Kwa ushahidi huu, tumewavua nguo wateule na waliowateua kwa hiyo si jambo dogo kiusalama, mkuu wa wilaya ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, anaweza kukufanya lolote kwa hiyo lazima nichukue tahadhari,” alisema Nassari na kuongeza:

“Nilidhani Rais angekuwa tayari amewachukulia hatua wote waliohusika ili kupisha uchunguzi unaofanywa na Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa), kwani uchunguzi hauwezi kufanyika kwa watu ambao bado wako ofisini wanaweza kuuvuruga,” alisema

Nassari alisema ushihidi alioutoa Takukuru ikibainika ni wa uongo atakuwa tayari kuachia ubunge wake na ikitokea waliotuhumiwa wakaachwa atakuwa na wakati mgumu kuwatumikia wananchi wake wa Arumeru Mashariki.

“Maisha yangu yatakuwa hatarini endapo watumishi hawa wataendelea kuwepo ofisini ikizingatiwa kuwa ninapoishi na wanapoishi hao sio mbali na hakuna mahali pengine nina makazi zaidi ya Meru,”alisema.

Ushahidi anaouzungumzia Nassari aliukabidhi juzi Takukuru jijini Dar es Salaam na kuelezwa kwamba uchunguzi umekwisha kuanza.

Sabubu ya uchunguzi

Nassari alisema wakati akiwa masomoni nje ya nchi, alianza kupata taarifa ya madiwani katika jimbo lake wanajiuzulu na wote wakitoa sababu moja ya kwenda kumuunga mkono Rais Magufuli.

“Nilijiuliza nini kimetokea maana wote waliojiuzulu wote walitoa sababu moja, watu wakasema mbona mbunge hasemi au anahusika na yeye, mimi nikaamua kutafuta chanzo ili kupata ukweli na ndiyo njia hii nilioyotumia,” alisema Nassari

Kuhusu vifaa na jinsi alivyovitega alisema: “…siwezi kuweka mbinu hadharani, nilitumia mbinu za kijasusi, nikiweka wazi nitakuwa naharibu, itoshe tu kusema ni vifaa bora kabisa vya kisasa ambavyo vimefanikisha kupata ukweli na gharama ya vifaa hivi ni kama Sh 8 hadi 9 milioni.”

Alisema anashangaa mpaka sasa uchunguzi wa suala la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) haujakamilika kwani wakiruhusu wachunguzi wa kimataifa itafanikisha hilo.

“Unajua kwa teknolojia ya sasa, juu huko kuna satellite ambazo ukiwaruhusu wachunguzi wa nje, watafunga mitambo yao katika eneo hilo la Area D (mjini Dodoma) alipopigiwa Lissu risasi hizo na picha zitaonyesha tukio zima,” alisema Nassari na kuongeza:

“Hata mimi naweza kuwasaidia kuwaunganisha na hao wachunguzi, Serikali iruhusu wachunguzi wa nje ili kufanikisha hili na kupata ukweli.”

Aligusia msimamo wa Serikali uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwamba uchunguzi utafanywa na vyombo vya ndani na wanasubiri Lissu apone aweze kusaidia.

“Nilitegemea Mwigulu asingekuwapo ofisini mpaka sasa, anasema hadi Lissu apone, hivi kama Lissu angekufa uchunguzi usingefanyika, hii ni kauli ya waziri wa mambo ya ndani ambayo sidhani kama ilipaswa kuitoa,”
 
anatafutwa na nani? au anajihofia baada ya kurelease ile clip ya 2008 iliyopitwa na wakati wakashangiliwa na Bawacha? mwenzie juzi kazuga tairi za gari lake kufunguliwa ili apate ajali ila hizo ni kiki tu.
Clip ya 2008 lakini walionaswa na hiyo clip ya 2008 walikua secondary na wengine chuo. Akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa hata siku moja
 
Sikudhani wapiga propaganda wa CCM wameshindwa mbinu hadi kujifunua mioyo yao kuwa wanachuki kiasi cha kuua. Dracula. Ndiyo wanatabia ya dracula, hawana mbinu za kisiasa na mkakati. Mnatia aibu.

Ili msionekane ni kizazi kilichokosa malezi, rudini kwa wazee wale waliosoma Kivukoni mkawaulize wawafundishe mbinu.

Naamini hamjui kwanini Chigwiyemisi aliitwa Tingatinga. Nguvu yake ilikuwa wapi.
 
unazushia watu uongo wa kutunga video unategemea nini? eti wapinzani upinzani gani mnaoufanya nyie. naamini bado mtanyooka tu.

Chezea Africa eeehee???

Ni hivi hajazusha bali kasema ukweli na ukweli una kawaida ya kuuma. Hao waliosemwa wameumia kupita kiasi hivyo kwakuwa wako madarakani ndio wanataka kutumia nguvu yao kumdhuru. Lakini usidhani watu watakuwa waoga kama mnavyofikiri, ni lazima hali hii ikiendelea watu watachukua hatua na hamtaamini. Nakuhakikishia hakuna mtu unayeweza kumgandamiza akakuangalia kila siku, itafika siku watu watasema ifike mwisho. Na kwa huko Arusha hilo haliko mbali.
 
Back
Top Bottom