Joshua Nassari avuliwa Ubunge wa Arumeru Mashariki kwa “Utoro” Bungeni

At least means not exceed .Ikiandikwa"at least 3days ina maanisha siku zisizo zidi 3.
Na iwe ndani ya siku 7 tangu azaliwe mtoto.
Na hizo siku ni paid leave.
"Employment and Labour Relations Act 2004 provides for paid paternity leave of at least 3 days (in a leave cycle of 12 months) for a new father if this leave is taken within the 7 days of the birth of a child".

Kwa kiswahili mwajiri atakulipa kwa siku tatu za paternity leave ndani ya mwaka ukiamua kuchukua, lakini aina limit ya muda wa kukaa bila ya malipo.

Haya na wewe njoo na yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingawaje simfagilii Job a.k.a mzee kifimbo cheza ila Joshua anajua alichokifanya mikutano mitatu bila bila lazima kuna namna
 
Nimemkumbuka mzee Sitta rip kwa sababu alikuwa ni Spika wa speed na viwango na kiukweli alilibadilisha sana bunge.

Zama hizi za sayansi na teknolojia siyo lazima watu mjikusanye eneo moja ndio mjadala ufanyike, unaweza ukawepo utaratibu wa wabunge kutoa michango yao kwa njia za kielektonic na watalazimika kukusanyika pamoja pale tu panapokuwa na mambo ya muhimu ikiwemo kupitisha bajeti.

Angalia muhimili wa Mahakama kwa mfano, juzikati wamezindua mahakama inayotembea na hii yote ni katika kuongeza kasi na kuimarisha viwango vya Huduma.

Kuna wabunge yawezekana tangu waingie bungeni 2015 hawajawahi kutoa mchango wowote iwe wa kuongea au wa maandishi. Sasa wabunge wa aina hii wana tofauti gani na Nassari?....... Je, wachukuliwe hatua gani?

Ukienda Kenya bunge zima hukutana mara chache, vikao vyao vingi huviendesha kwa mtindo wa kamati na hii inatoa fursa kwa wabunge kufocus katika maeneo ambayo wako interested.

Nimalizie kwa kusema kuna wabunge ambao siyo wahudhuriaji wazuri bungeni lakini tembelea majimbo yao uone tofauti, hapo walikuwepo MO, RA na hata yule Ayiro wa Rorya.

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka.
Maendeleo hayana vyama!
 
Muongozo wa Bunge una madhaifu mengi.Spika Ndugai ni moja kati ya udhaifu wa bunge.Nadhani hilo ni wazo zuri mfano mtu kama Abood na waarabu wengi walio wabunge hawaongei saana bungeni achilia mbali kuhudhuria.
Kwa hiyo hilo ni wazo zuri lakin skype haitowezekana bungeni kutokana na uadui uliopo baina ya wabunge wa vyama.ccm wataanza kupiga kelele ili asisikike.Hii itatia tu hasira na mengineyo.Halafu.
moja kati ya udhaifu wa bunge la sasa ni kutanguliza uvyama yaani wabunge wanawaza serikali kuliko nchi/wananchi na maendeleo.Ndio maana hakuna ukosoaji kwa serikali hata upuuzi gani ufanyike.

kunatakiwa katiba ibadilike na itoe mwongozo mpya wa uendeshaji wa bunge na uchaguzi wa wawakilishi kwa ujumla.Ikibidi kila mkoa utoe mwakilishi 1 tu ambaye atakuwa ni strong.Hii nnaipenda.mfano kama Sugu angekuwa mbunge wa Mbeya nzima.mbeya ingekuwa imepiga hatua kubwa zaidi na uonevu wa serikali ungepungua maana ingeogopa kupoteza ushawishi mkoa mzima.pia siasa zingekuwa za kistaarabu zaidi na ujinga na utoto wa bungeni ungepungua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaaa haaa yericko kashukiwa na watu kule Instagram alijaribu kumtetea nasari watu wakawa wanakuja na maswali yenye akili ambayo hata yeye yericko yalimshinda, naona kapanic kuona nasari anatoa majibu mepesi mepesi kwa maswali mazito ambayo hata yeye yericko yalimshinda kiufupi dogo kaliuza jimbo kijasusi 😀😀😀
 
"Employment and Labour Relations Act 2004 provides for paid paternity leave of at least 3 days (in a leave cycle of 12 months) for a new father if this leave is taken within the 7 days of the birth of a child".

Kwa kiswahili mwajiri atakulipa kwa siku tatu za paternity leave ndani ya mwaka ukiamua kuchukua, lakini aina limit ya muda wa kukaa bila ya malipo.

Haya na wewe njoo na yako

Na hiyo Paternity Leave, unaomba kwa mwajiri wako muda gani na kwa utaratibu upi? Au unajiondokea zako baada ya miezi mitatu ndio unamtumia mwajiri BARUA PEPE kuwa your 'significant other' kapata mtoto? Tuelimishane.
 
Na hiyo Paternity Leave, unaomba kwa mwajiri wako muda gani na kwa utaratibu upi? Au unajiondokea zako baada ya miezi mitatu ndio unamtumia mwajiri BARUA PEPE kuwa your 'significant other' kapata mtoto? Tuelimishane.

34.-(1) During any leave cycle, an employee shall be entitled to-
(a) at least 3 days paid paternity leave if-
(i) the leave is taken within 7 days of the birth of a child; and
(ii) the employee is the father of the child;

(b) at least 4 days paid leave for any of the following reasons-
(i) the sickness or death of the employee's child;
(ii) the death of the employee's spouse, parent, grandparent, grandchild or sibling.

(2) Before paying an employee for leave under this section, an employer may require reasonable proof of the event prescribed in subsection (1).

(3) For the purpose of clarity-
(a) the 3 days referred to in subsection (1)(a) are the total number of days to which the employee is entitled irrespective of how many of the employee's children are born within the leave cycle;
(b) the 4 days referred to in subsection (1)(b) are the total number of days to which the employee is entitled irrespective of how many of the events prescribed in that paragraph occur within the leave cycle, but the employee may take more days as may be authorised by the employer for the event and other subsequent events within the same leave cycle provided that such extra days will be without pay.
........................................................................................................................................................................................................

Hiyo ni literal (rule) interpretation in general employment terms, nakushauri pitia sheria yote utaona sheria inatambua kuna watu wana mikataba tofauti na 8am-4pm ya kila siku na ivyo kuna application tofauti za kupata leaves and so forth but that still protect their literal rights of paternity.

Sasa mmbunge wajibu wake wa vikao ni seasonal na ombi la Nassari kwa mujibu wa maelezo ni days before bunge kuanza, kuna different approaches kwa taratibu zao walizojiwekea na kwa mujibu wa mmbunge husika amezifuata. Kesho ndio tutasikia zaidi upande wake.

https://www.ilo.org/dyn/natlex/docs/SERIAL/68319/66452/
 
Hii inavunjwa kwa sababu ya nguvu ya mtu mmoja kufanya teuzi na kumtoa yeyote kwa mamlaka yake kikatiba.
Anavunja katiba kikatiba sio vinginevyo.
Hivi unafikiri hata Mkuu wa Wajeda akiambiwa avae tisheti ya kijani hadharani atakataa ?
Kumbuka anayeweza kumwambia chochote ni mwenyekiti wa chama na mkuu wa nchi na ndiye anayeweza kwa usiku mmoja ukaamka ukajikuta una njaa mana anaweza akakupiga chini na akateua mwingine na akaunda safu ya kukuzibiti kwa namna yoyote.
Anateua wakuu wa Idara zote na vyombo vyote na mihimili yote.

Na nafasi zake za uteuzi zina maslahi manono ajabu.
Nani asiyependa maisha mazuri?

Nguvu kubwa na mamlaka makubwa yapo kwenye uteuzi ambao upo kikatiba.

Katiba ikimpunguzia madaraka ni lazima aifuate.
Kwa sasa hata Chama chake ni kidogo kwa mujibu wa Lipumba alieleza vizuri sana.
Nguvu kubwa na mamlaka makubwa kikatiba ndiyo silaha kubwa ya kufanya Lolote ukizingatia pia kuwa hashitakiwi.

Lakini pakiwa na Katiba inayompunguzia madaraka ya uteuzi, maamuzi bila bodi au chombo maalum cha kumshauri na awe analazimika kufuata ushauri huo wa Kitaalam .

Katiba yenye kuipa mihimili mingine Mamlaka ya kuisimamia na kujisimamia yenyewe bila kupanguliwa kirafiki na kindugu na mkubwa wa Taifa.

Bunge lenye mamlaka ya kuhoji teuzi zinye mashaka na kutoa maamuzi ya kuzitengua.

Hivi unafikiri kama wakuu wa dola wangekua wanapelekwa bungeni kujadiliwa na kueleza weledi wao na kuhojiwa kuna mtu angezembea kwenye kutoa haki.
Lakini kwa sasa anayemteua Mkurugenzi ndiye huyo huyo anayemteua Mkuu wa Wilaya, mkuu wa mkoa ,Das, Ras n.k watasimamiana VIPI kama sio kuwa na Common intention ya kichama tu lakini sio kiuwajibikaji na kiuadilifu wa kweli bila unafiki.

Anayemteua Mkuu wa Magereza ndiye huyo huyo anayemteua waziri wa mambo ya ndani .Watasimamiana vipi kama sio kumsikiliza Swahiba zaidi na kada zaidi na kumtoa anayeonekana hayupo kichama na kirafiki au kindugu.

Katiba ndio msingi wa mfumo . Mifumo mibovu inajipambanua kulingana na katiba
Na katiba iliyopo inajivunja yenyewe Kikatiba ndio maana kifungu kimoja kinatoa Haki kingine kinavunja bila kuathiri mamlaka ya mvunjaji.
Wakuu wa Wilaya wanavunja sana katiba kwa kuweka watu ndani masaa 48 kwa makosa yasiyo ya kijinai . Lakini hakuna wa kusema mana mtaule wao ana mamlaka makubwa kuliko chombo chochote duniani.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hili ndio tatizo la msingi kwenye katiba na watu wengi sana wamelilalamikia hili swala lazima lifanyiwe amendments kwa jinsi raisi anavyohodhi madaraka makubwa muda wake umeshapitwa.

Mara yakazuka madai ya katiba mpya from nowhere wakati iliyopo aina shida zozote, leo ukiwauliza wanaopiga kelele za katiba mpya iweje watakwambia sijui NEC, Jecha na mambo mengine ambayo hayana nguvu za kihoja kuleta katiba mpya, lakini hili la madaraka litawaumiza sana wapinzani na watanzania madaraka ya raisi lazima yapunguzwe.
 
Hili ndio tatizo la msingi kwenye katiba na watu wengi sana wamelilalamikia hili swala lazima lifanyiwe amendments kwa jinsi raisi anavyohodhi madaraka makubwa muda wake umeshapitwa.

Mara yakazuka madai ya katiba mpya from nowhere wakati iliyopo aina shida zozote, leo ukiwauliza wanaopiga kelele za katiba mpya iweje watakwambia sijui NEC, Jecha na mambo mengine ambayo hayana nguvu za kihoja kuleta katiba mpya, lakini hili la madaraka litawaumiza sana wapinzani na watanzania madaraka ya raisi lazima yapunguzwe.
Wanasiasa Wasio waadilifu wanapenda katiba inayowapa madaraka makubwa sana wakishaingia madarakani.
Kundi linalonufsika na teuzi za kutoka kwa mtu mmoja hawawezi kuleta katiba bora.

Kama JK angeweza kudhibiti wanasiasa waliovuruga mchakato wa Katiba ya Warioba Leo hii angekua ni Rais mstaafu Bora kabisa Duniani. Kitendo cha Kuwatumia makada wa chama Chake na wanachama wa vyama vya vingine na makada wao kwenye Bunge maalum kulinajisi mchakato wa Katiba mpya.
Bunge liligeuka kama bunge la kawaida la kujadili maslahi ya wanasiasa na vyama vyao badala ya maslahi ya nchi.

Mpaka sasa Katiba iliyopo ipo kwa ajili ya maslahi ya wanasiasa na vyama vyao hasa chama tawala lakini sio maslahi ya Nchi yenye watu wengi wasio na vyama.

Katiba imekua ni kwa ajili ya maslahi ya Chama sio vinginevyo ndio maana ni rahisi kumwona Msajili wa vyama akifanya kazi za Kusaidia Chama Tawala kushinda uchaguzi mdogo kama wa Diwani na Mbunge.
Ni Katiba ya kuwafanya makada wa chama Tawala wajipambanue kuwa wao wako juu ya sheria.

Kuna udhaifu mkubwa kwa sababu ya Kofia Mbili za Mwenyekiti kuzivaa kwa wakati mmoja.
Hata kwa Hali ya kawaida mtu akivaa kofia mbili kichwani atakua kituko au watu watahoji afya ya hiyo sehemu ilipovaliwa hizo kofia.

Kwa mtu mwadilifu kabisa kabisa hakuna haja ya kuwa na madaraka makubwa peke yake mana inampunguzia malumbano yasiyo na maana. Anaacha vyombo vyake vifanye kazi kwa kila kimoja kwa majukumu yake kamili.

Ukiwa na Tume ya maadili inayopatikana kwa misingi ya uwazi na wakahojiwa uadilifu wao bungeni. Wakapigiwa kura hakika uadilifu utasimamiwa kwenye sekta ya umma kwa nguvu kubwa.

Ukiwa na Wakuu wa vyombo vya usalama wanaopatikana kutokana na uadilifu na historia uliyopo wazi kiuadilifu ni rahisi kujenga uadilifu mana kila mmoja atakua anajua kuwa uadilifu utawapa fursa ya kusimamia mikoa na Wilaya na idara. Lakini mtu mmoja anateua tu hata shangazi zake walevi au wezi alimradi anajua kuwa watakua wanatumika kujenga himaya ya kichama na kimaslahi ya vyeo hakuna kinachobadilika zaidi ya kila mtu kutii ili ale kwa urefu wa kamba yake.

Ukiwa na Mhimili wa mahakama au Bunge lenye wakuu wa mihimili wanaopatikana kwa historia ya kutenda haki ni ukweli kuwa nchi itakwenda.
Sio jaji anachaguliwa kwa kutoa hukumu ya kumgandamiza mtu asiyependwa na mkubwa wa uteuzi .

Mtu aliyepiga mtu gongo la kichwani kwa lengo kuua kabisa hawezi kuwa mkuu wa mihimili wa Bunge mana angewekewa pingamizi na tume ya maadili kuwa mvunja sheria hawezi kusimamia mhimili wa kutunga sheria.

Kuna watunga sheria wengi sana wamepata uwakilisha wakati historia yao sio nzuri kabisa. Kuna wengine walikua wahalifu kabisa lakini hakuna Miiko ya uongozi iliyoko Kikatiba.
Hao hao wanawekwa kwenye Bunge maalum la katiba.

Wanasiasa hasa waliopo Bungeni na makada wa vyama kamwe hawatafikia muafaka wa kupatikana kwa katiba bora mana wanapigania maslahi yao na vyama vyao na sio Taifa.
Watabaki na mambo ya serikali Tatu na tume ya uchaguzi kuwa huru bila kupigania tume nyingine zinazowagusa wananchi moja kwa moja kama tume ya utumishi.
Tume ya Kupambana na Rushwa ,tume ya haki za binadamu,tume ya maadili n.k.

Mambo ya msingi kama afya na uhai havijadiliwi kwa upana badala yake watu wanapigana mitama kwa ajili ya serikali tatu au mbili. Wanasiasa wanapigania maslahi na vyeo tu na wapo tayari kwa lolote alimradi walete katiba inayowapa wao unafuu mkubwa wa maisha na kuwaweka mbali na mlango wa gereza.

Kama awamu hii ya Tano itajiweka mbali na ubinafsi wa wanasiasa basi tunaweza kupata katiba bora kabisa kabla ya Muda wake kuisha.
Katiba inayomfanya kila mtu ajione kuwa anawajibika kufuata sheria mana kila mtu atajiona amesimama kwa miguu yake.

Haiwezekani mtu ambaye ni kiongozi aseme hadharani kuwa Mimi ni mtu hatari sana nitaweza kukufanyia kitu kibaya hutanisahau . Huyu hajasimama kwa miguu yake. Amesimamia miguu ya mtu au yupo mgingoni kwa mtu. Anamwogopa alitemteua mana huyo huyo ndiye aliyeteua wakuu wa Tume ya maadili ,PCCB Polisi,tiss n.k. Hakuna wa kumzuia mwenzake na kumchunguza kama ilivyokua kwa Waziri kumchunguza mkuu wa mkoa wakati wote ni wateule wa mtu mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ndilo jambo mhimu kulijadili hapa, kuliko Nassari na wengine wasioelewa maana ya kuwa mwakilishi wa wananchi.
Kwa kuanzia ningeshukuru kusikia mbinu za ushindi wake akiwa CCM. Je, wananchi watakuwa wamemchagua kwa hiari yao, au kwa mbinu/kulazimishwa!

Mjadala kama huo ungekuwa wa manufa makubwa.

Nasari hastahili kupitishwa na Chama chochote kile kuwa mbunge mana ameshindwa kuwakilisha wananchi kwenye vikao vya Bunge.

Nitawashangaa CCM au Chadema kama watampa nafasi ya kugombea.
Huyu ni bora wale wanaounga mkono juhudi kuliko huyu anayeacha makisudi kuwawakilisha wananchi wake bungeni bila sababu za kueleweka.

Hawa wanasiasa wamelewa fedha. Ametumia jina na wadhifa wa ubunge kuomba na kupata misaada mingi na kujijenga haraka haraka kiuchumi.
Hospitali zetu zinajitahidi sana kutoa huduma bora kabisa ikishindikana hata Kenya lakini wanasiasa wamefikia mahali hata akijikata wakati wa kunyoa ndevu anakimbilia ulaya tena hata wakati wa vikao bila kujali kazi aliyopewa ya kuwakilisha wananchi.

Nasari asipewe tena jimbo lolote kwenye chama chochote. Kama anampango wa kukimbilia CCM nadhani wao kupitia kanuni ya bunge lao na spika wao wametuambia kuwa Dogo ameshindwa kuwakilisha wananchi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom