Joshua Nassari avuliwa Ubunge wa Arumeru Mashariki kwa “Utoro” Bungeni

Ngoja nisikie tokea upande wa pili.. Kama itakuwa kweli hakuhudhuria vikao hivyo mfululizo, wakati akijua wabunge wapinzani wanatafutiwa sababu ya kutimuliwa bungeni, basi anastahili hiyo adhabu.. Pia kama ni kweli ufanyike uchunguzi, pengine hujuma..

Ila bado naamini kuna figisu mahali..
 
Kama hajahudhuria vikao vyote hivyo bila sababu maalumu, nahisi alitaka kwenda kuunga mkono juhudi lakini akawa anaona aibu.

Sasa njia pekee ni kutokuhudhuria ili afukuzwe akaunge juhudi. Je mwenyekiti wake alikuwa na taarifa ya mbunge wake hasa ukizingatia ni kiongozi wa upinzani bungeni?

Haya hivyo hilo bunge kuhudhuria ni kukosa kazi maana ni bunge kibogoyo.
 
Hivi Lissu nae washamvua ubunge? maana spika anasema hajulikani alipo na hawana taarifa za wapi alipo tangu mwaka jana ndio maana wamemsitishia mshahara wake! hivi hili limekaaje? si wanasema anazurura? mbona hawamvui ubunge kama hoja yao ina ukweli?
 
hizo kanuni nasari hakuzijua? spika hana utaratibu na ofisi yake kuwauliza wabunge walipo?
je kuna watoro wangapi? tunaopmba spika awe muwazi ili an wananchi tujue watoro wengine ama kama hawapo bungeni waliko atuineshe inawezwekana wanadanganya tu
 
Alienda kusoma au kufanya mapenzi na akina dada?, kwanini mda wote huo asihudhurie hata kikao cha katikati tu ili kuvuruga mfululizo wa utoro wake.

Pesa zetu za kodi zinawafanya watoroke waende kutembea ng'ambo alafu wanatuletea kiswa-english bungeni.......walaaniwe!!
 
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua nassari anadaiwa kuvuliwa ubunge kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa kuhudhuria mikutano mitatu ya bunge, jambo ambalo ni kinyume na sheria na taratibu za Bunge.

Nafasi yake imebaki wazi.

View attachment 1045633

UPDATE:

JamiiForums imemtafuta Mbunge huyo ambaye amesema hana taarifa rasmi naye ameona taarifa zikisambaa mitandaoni.

Aidha, ameifahamisha JamiiForums kuwa mapema Januari (tarehe 29) mwaka huu aliwasiliana na Ofisi ya Spika na kueleza juu ya kushindwa kuhudhuria vikao vya Bunge.

Sehemu ya Barua yake kwa Spika inasomeka:

Dear Mr. Speaker.

REF: PARLIAMENT PROCEEDINGS

I am writing to keep your esteemed office informed that, I amregrettably unable to attend the currently ongoing Bunge proceedings because of circumstances beyond my reach.


For quite sometimes now, I have been attending my significant other who is receiving medical attention outside the country. The good news is, she managed to give birth to a healthy baby girl two days ago.

However, her medical specialists have advised that they will need to closely monitor her progress for couple of weeks before we can make our way back to the country.

I reiterate my desire to attend the upcoming sessions as scheduled upon my return.


All my Best,

Joshua Nassari (MP)

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungana wa Tanzania, Job Ndugai amemuandika barua, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Semistocles Kaijage kuwa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa sasa liko wazi kufuatia, Mbunge wake Joshua Nasari ( CHADEMA) kushindwa kuhudhuria mikutano mitatu mfululizo na hivyo kupoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge.View attachment 1045634View attachment 1045635

Sent using Jamii Forums mobile app

......Mheshimiwa joshua nassari si ndio aliemwambia JIWE wabadilishane nafasi
""Jiwe awe mbunge halafu joshua nassari awe raisi kama ubunge ni kazi nyepesi""

Kamati ya roho mbaya......!!? Karma

Km hujaelewa utakomaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom