Wanabodi,
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa wakazi wa Arumeru Mashariki wanasema mgombea wa Chadema Joshua Nassari, nafasi yake ya kuchukuwa kiti cha ubunge ni ndogo sana.
Katika mila zao Wamasai na Wameru hazitofautiani sana. Wazee wa kimila wamesikitishwa sana na kitendo cha Chadema kuwaletea mtoto ili awaongoze.
Wanasema Nassari, bado mtoto analelewa na wazazi wake, hana mke hana mtoto, hatuwezi kumpima hata kwa uongozi wa familia yake, anawezaje kuongoza wazee!
Wanasema Nassari mwenyewe anajua mila na desturi zetu Wameru, haziruhusu watoto kushiriki vikao vya wazee.
Nassari anajitetea kuwa mbona wengine hawajaoa kina David Silinde, Zitto Kabwe, Joseph Mbilinyi, John Mnyika.
Wazee wakamwambia hawa wote wana mila na desturi zao, inawezekana baadhi yao hawana hata mila moja.
Hiyo haiwezi kuhalalisha sisi tuvunje mila zetu kwa kuongozwa na watoto wadogo ambao wanalelewa na baba na mama.
Hizo mila desturi za Wameru na Wamasai ndio limekuwa tatizo kubwa kwa Jossua Nassari kushinda ubunge.
Kama umri ni kigezo Nassari asingepata wingi wa kura aliopata 2010 na pia kura hazipigwi na wazee peke yao bali wanajimbo wote walioandikishwa ambao ni vijana kwa asilimia kubwa sana.......1/04/2012 itadhibitisha