Joshua Nassari ana wakati mgumu sana kushinda ubunge Arumeru kutokana na mila zao

Ili kujihalalishia uungwaji mkono miongoni mwa jamii za Wameru na Wamasai Chadema wameamua kuonyesha picha mbalimbali za Nassari wakidai anaombewa baraka na kina mama wa jimbo hilo.

Huku wengine wakiwa wamevalishwa mavazi ya CCM na skafu za CCM, ni za kupanga zinazolenga kujenga tu imani na matumaini kwa watu walioko nje ya jimbo hilo kuwa mgombea huyu anapendwa.

Mila za watu wa Arumeru ni tofauti sana na maeneo mengine.



Hivi wewe ni mmeru wa wapi? Naomba unijibu kilugha - KIMERU ili niamini kuwa wewe ni meru na unayajua usemayo.
 
Wapi nimekanusa hilo? Ni kweli uwa anaishi Marekani anakuja Tanzania kwenye Chaguzi tu za Ubunge na Bavicha..una lingine?

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 kushindwa na Jeremiah Sumari, unajua Nassari alikuwa wapi?
Duhh!.......kama maneno yako ni kweli basi mtoto huyu ni Kiboko kuliko Kiboko mwenyewe!.....yaani anakwenda Marekani kama kariakoo??
 
Mkuu Kimbunga,
Hawa jamaa hawataki kukubali mila na desturi zetu kama bado zina nafasi kubwa sana katika siasa zetu.

Mkuu nimeongea na mzee Lekeyeiya, wa Ngarananyuki anasema kiongozi wetu mkuu wa kimila, awe jamii ya Wamasai au ya Wameru, anapozungumza, anachoagiza inabidi sote tumtii, vingenevyo yule asiyetii anatengwa na yanaweza kumpata makubwa.

Kitendo cha kutuletea mtoto wetu ili atuongoze ni dharau kubwa kwetu.

Anasema kwa uchungu siasa zinataka kutuchafulia mila zetu na desturi ili alikubariki hata kidogo.
Acha propaganda ukweli ni kwamba uongozi wa kimila unaheshimika na utabaki kuwa wa kimila, ubunge sio uongozi wa kimila ndio maana utakuta nyadhifa za kisiasa zinapata viongozi ambao kimila isingewezekana, jiulize kwani uongozi kisiasa ni ubunge tu? Mbona kuna madiwani, wenyeviti, makatibu na wajumbe wa vijiji vijana ambao hawajaoa na kuolewa? Kwanini hoja hiyo ionekane ina umuhimu kwenye nafasi ya ubunge tu na sio nyinginezo? Jibu ni rahisi tu "HIZO NI PROPAGANDA ZA MAGAMBA", tuzipuuze tusonge mbele.. hao wazee unao wadahili hakika ni wale waliopata kofia, t-shirts, pilau nk.
 
Hivi wewe ni mmeru wa wapi? Naomba unijibu kilugha - KIMERU ili niamini kuwa wewe ni meru na unayajua usemayo.

Ulimbo,
Nikijibu Kimeru ndio utayakubali haya maneno yangu? Hata mie na wasiwasi kama wewe ni Mmeru kweli hujui mila na desturi za Arumeru.
 
Ulimbo,
Nikijibu Kimeru ndio utayakubali haya maneno yangu? Hata mie na wasiwasi kama wewe ni Mmeru kweli hujui mila na desturi za Arumeru.


Ndo maanake. Ugumu uko wapi. Kama wewe ni mkweli, nijibu tu kimeru.
 
Tusubiri matokeo mkuu...hagombei uongozi wa kila kuwaongoza hao wazee, bali kuongoza jamii yenye rika zote.
 
Hakuna cha washii wala laigwanani labda magamba wachakachue kura tena vijana walivyo jipanga kuchakachua nongwa!
 
Kiko wapi? Wakati mgumu my foot! wameshindwa hata kuchakchua. Ondoa sera za ko za ndotoni hapa, tunaangalia reality. Shame on you kwa kuwadhalilisha wazee wa Kimeru.
 
Wanabodi,
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa wakazi wa Arumeru Mashariki wanasema mgombea wa Chadema Joshua Nassari, nafasi yake ya kuchukuwa kiti cha ubunge ni ndogo sana.

Katika mila zao Wamasai na Wameru hazitofautiani sana. Wazee wa kimila wamesikitishwa sana na kitendo cha Chadema kuwaletea mtoto ili awaongoze.

Wanasema Nassari, bado mtoto analelewa na wazazi wake, hana mke hana mtoto, hatuwezi kumpima hata kwa uongozi wa familia yake, anawezaje kuongoza wazee!

Wanasema Nassari mwenyewe anajua mila na desturi zetu Wameru, haziruhusu watoto kushiriki vikao vya wazee.

Nassari anajitetea kuwa mbona wengine hawajaoa kina David Silinde, Zitto Kabwe, Joseph Mbilinyi, John Mnyika.

Wazee wakamwambia hawa wote wana mila na desturi zao, inawezekana baadhi yao hawana hata mila moja.

Hiyo haiwezi kuhalalisha sisi tuvunje mila zetu kwa kuongozwa na watoto wadogo ambao wanalelewa na baba na mama.

Hizo mila desturi za Wameru na Wamasai ndio limekuwa tatizo kubwa kwa Jossua Nassari kushinda ubunge.
Duh! watu kwa mbwembwe.
 
Back
Top Bottom