Joshua Nassari amkurupusha mwenyekiti wa kijiji CCM Monduli akigawa rushwa

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,820
1,195
Tumemkuta katibu wa tawi la CCM kijiji cha Naiti, anaitwa Peniel Olodi akikusanya shahada za kupigia kura za wananchi wa kata ya Makuyuni hii ni sehemu ya daftari la majina na namba za shahada zao. Wanchukua shahada za wapiga kura wenye mwelekeo wa upinzani, kisha wanawapa fedha na kubaki na shahada zao. Hii inaonyesha jinsi gani CCM na Lowassa wapo hoi.

SOURCE:- Josh Nassari.
 

Attachments

eumb

Senior Member
Apr 2, 2012
149
0
Haya wale wanaobisha kuwa hakuna uhuni unafanyika kwenye chaguzi wabishe tena na hili! Duh, sijui lini tutafika kwenye demokrasia ya kweli!!??
 

Arushaone

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
14,922
2,000
Hizo ni siasa chafu. Wako wapi tume ya uchaguzi wakiondoe CCM kwenye uchaguzi husika? Wapi msajili wa vyama vya siasa atoe tamko?
 

mamseri

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
685
250
Yamekuwa hayo tena? Mbona Lowasa alisema hana wasiwasi na hiyo kata? Kumbe kelele za bure sasa ushahidi umekamatwa. Atulie anyolewe
 

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
0
Huyo kada wa CCM ilitakiwa kwanza apate kichapo kizuri tu kabla ya hatua nyingine kufuata.
 

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
325
0
Huyu dogo mpga kelele akaweke mambo sawa jimbon na nyumban kwao kwanza aache ukanjanja kna mbowe,zito wanamake yeye anarukaruka tu huyu mjinga
 

kalokolaVIII

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
397
195
Mheshimiwa Nassari,
salamu kwako na wapiganaji wengine mnaopambana kuikomboa Tanzania kutoka katika makucha ya mkoloni mweusi.
Kila wakati wa uchaguzi nimekuwa nikisoma haya matukio ya wenyeviti wa vijiji,mabalozi wa nyumba 10, na makada mbalimbali wa CCM kukutwa/kukamatwa wakikusanya shahada za wapiga kura - kwa maoni yangu haitoshi kukimbizana nao kwasababu wewe unamkamata mmoja lakini 9 wanakukimbia kwa maana ya kuwa haufanikiwi kuwafichua na mbaya zaidi hata huyo unayemfichua hakuna kinachomtokea from a legal point of view. sasa swali la kujiuliza - NINI KIFANYIKE??? Kwa mtazamao wangu umefika wakati CHADEMA kama CHAMA kianze mapambano ya ku-introduce kwenye penal code ya Tanzania kosa la kukutwa na shahada ya kura ambayo si "mali" yako na adhabu yake ilinganishwe na UBAKAJI - hakuna cha faini wala nini - maana huu kwa uhakika ni UBAKAJI WA DEMOKRASIA.
Anzeni kulipigania hilo na tunataka kuona kama CCM watasema kuwa si kosa kukusanya shahada za kura - hawatoweza kulitetea hilo hata kidogo. Nawasilisha!!!
 

kababu

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,538
1,250
Huyu nayee mkatamigomba anaweza kitu kweli, wameru bwana, wanakatakata miomba, huko monduli hamna migomba bwana nassary, rudi tu nyumbani kwani hapo unapoteza mda na fedha nyingi,
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,510
2,000
Tutumie Biometric katika chaguzi,tuone kama CCM wataweza nunua macho na vidole vya watu!!!CCM wanaudhi basi tuu ndiyo maana naseam kuwatoa ccm madarakani kwa kura ni ndoto,jamaa wezi sana hawa!Chaguzi mbili za urais wameiba Zanzibar wazi wazi unategemea nini
 

Deshmo

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
4,778
2,000
Huyu nayee mkatamigomba anaweza kitu kweli, wameru bwana, wanakatakata miomba, huko monduli hamna migomba bwana nassary, rudi tu nyumbani kwani hapo unapoteza mda na fedha nyingi,
Darasa la 7,posho buku 7
 

Gefu

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
6,945
1,500
...tuwekeeni picha ya huyo mtu akiwa ameshapendeza rangi nyekundu tafadhali...
 

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,053
2,000
Hizo ni siasa chafu. Wako wapi tume ya uchaguzi wakiondoe CCM kwenye uchaguzi husika? Wapi msajili wa vyama vya siasa atoe tamko?
Mkuu msajili wa vyama anapata kiwewe tu pale anaposikia CDM wamefanya jambo fulani. ccm kwao imehalalishwa hata kuua...

Kitaeleweka mwaka huu!
 

maphie

Senior Member
Jul 28, 2011
174
0
Nashangaa watu mnaomponda nassary na kabila lake! Kimsingi kwa mtu ambaye anaijua historia uhuru wa Tanganyika anaweza kujua mchango wa wameru katika harakati za uhuru; hawa ni watu kwanza kabisa kutoka Tanganyika kufika umoja wa mataifa kudai uhuru mwaka 1954! Anachofanya Nasari ni kuendeleza harakati hicho kwa kuwaondolea watanzania huyu mkoloni mweusi(ccm). Viva cdm, viva Nasari! Kamat mwizi popote pale alipo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom