Joshua Nassari akanusha kufyatua risasi jana kwenye uchaguzi wa madiwani Daraja II Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joshua Nassari akanusha kufyatua risasi jana kwenye uchaguzi wa madiwani Daraja II Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kitu Kizito, Oct 29, 2012.

 1. Kitu Kizito

  Kitu Kizito JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mh Joshua Nassari amekanusha tarifa zilizoandikwa na magazeti ya Uhuru na Habari Leo kuwa jana alifyatua risasi na kuzua tafrani katika uchaguzi wa kumtafuta Diwani wa Kata ya Daraja Mbili ya Jijini Arusha uliofanyika jana.

  Nassari ameyasema hayo leo jioni wakati akihutubia kuzindua Kampeni nyingine za chama chake kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa kwa ajili ya Halmashauri ndogo ya Mji wa Usa River unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya Novemba 4, 2012.

  Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na watu wengi, umefanyika katika viwanja vya Ngaresero Usa-River. Mbali na Nassari, kiongozi mwingine wa Chama aliyehudhuria alikuwa Henry Kileo, kutoka CHADEMA Kanda ya Kinondoni.

  Nassari amedai kuwa yeye alikuwa Wakala Mkuu Kata ya Bangata, na kwamba ameshazungumza na OCD kuhusiana na taarifa hizo. Amedai kuwa mtu aliyefyatua risasi ni Mwenyekiti wa UVCCM, Godwin Mwalusamba na kwamba Polisi walimuweka ndani na kuandika maelezo yake...lakini anashangaa kuambiwa ni yeye!!

  DSCN5946.JPG Sehemu ya watu waliojitokeza leo kwenye mkutano wa Ngaresero jioni ya leo. Nassari yuko jukwaani
  DSCN5929.JPG Nassari akihutubia mkutanoni hapo
  DSCN5906.JPG
  Henry Kileo nae akizungumza katika mkutano huo
   
 2. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,971
  Likes Received: 37,531
  Trophy Points: 280
  Chadema hakuna kulala mpaka kieleweke.

  Matokeo ya udiwani iwe chachu kwani hata hizo kata mlizoongeza ni matunda ya m4c.

  Hakuna kurudi nyuma.

  Muongeze mbinu na mikakati ya ushindi.Hii ndio kazi iliyobaki.
   
 3. F

  FRANK MICHAEL Senior Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tena eti gazeti la uhuru wapuuzi kweli, jana Nassari tulikua naye Bangata.[SUB][/SUB]
   
 4. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Naipongeza cdm,kata 5 si mchezo..
   
 5. n

  ngurati JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo sasa! Kuna haja ya kuyasusia Kabisa Uhuru na habari Leo kwa upotoshwaji mkubwa.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Mwanzo wa ngoma lele, leo inafyatuliwa tu, kesho inafyatuliwa kwa mtu.

  Hatuwezi kushangaa kwa mwendo huu.
   
 7. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Polisi walikuwepo daraja 2 na aliyefyatua risasi walimwona. Hizi propaganda kwenye maswala technical na obvious kama haya ni upuuzi kabisa!
   
 8. washa

  washa JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 476
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Hivi mbona magazeti haya hayafungiwi?, lakini pia ninahamu ya kusikia kauli ya tendwa juu ya vurugu katika uchaguzi wa uvccm!
   
 9. b

  blueray JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Habari Leo na Uhuru ni moja ya viwanda vya kuzalisha uongo, hata wanachama wenyewe wa CCM wanaboreka na uongo uliokithiri wamagazeti haya. Ukitaka kujua uongo chunguza taarifa ya tukio moja hasa likiwa la kisiasa, magazeti yote habari na ujumbe wa taarifa husika ni sawa lakini ni Habari Leo tu na Uhuru wanaripoti tofauti!
   
 10. Medical Dictionary

  Medical Dictionary JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,053
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  mwanahalisi ilifungiwa kutokana na kuripoti ukweli ambao ulithibithishwa na mhusika(dr ulimboka),jambo leo na habari leo yameripoti uongo kwanini nayo yasifungiwe..?
   
 11. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kwa nini wanazushia upinzani kwa nini wasijizushie wenyewe maana ndio wamilikaji wa bunduki kila kona
   
 12. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yanafungiwa tu yale ya nayo toataarifa muhimu na zaukweli lakini magazeti ya udaku ya ccm hayafungiwi mkuu ila siku zinakuja hawa watakuwa rupango ili kueleza kwa nini walikuwa wanapotosha ukweli
   
 13. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kumbe tuhuma nyingi wanazoshutumiwa wapinzani si za kweli, wanabambikiwa ili watu tuamini kuwa wapinzani wanaleta vurugu. Kama haya magazeti (Uhuru na Habari leo) yasipofungiwa basi hatutakuwa na imani tena na wanaosimamia sheria za nchi hii. Pia itatufanya tuamini kuwa Mwanahalisi limefungiwa kutokana na kuripoti ukweli ambao serikali haikuupenda. Nabaki kujiuliza, hivi hii serikali ni ya watu milioni nne tu ambao ni wanachama wa CCM?
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Aina ya waandishi wa Habari Leo na Uhuru ni aina ya waandishi wanaojulikana kama makanjanja.

  Wala sishangai aina ya upotoshaji wanaoufanya kwa maslahi ya bwana wao.
   
 15. K

  Keil JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni jukumu la Bwana Joshua Nassari na CHADEMA kuyashitaki hayo magazeti kwa kuandika habari za uongo ambazo zina athiri CHADEMA na Mbunge mwenyewe.

  CHADEMA siku zote kimekuwa kikishutumiwa kwamba ni chama cha wafanya fujo. Iwapo Nassari na CHADEMA watakaa kimya, watu wa nje ya eneo la tukio na hasa ile mikoa ambayo inalishwa kasa kirahisi wataendelea kuamini kwamba ni kweli CHADEMA ni chama cha wafanya fujo na ndio maana hata Mbunge wake alifyatua risasi kwenye uchaguzi.

  Habari kama hiyo ni kashfa kwa CHADEMA na pia ni kashfa kwa Nassari na kwamba inaweza kukigharimu chama kupoteza imani imani kwa wapiga kura na/au Mbunge wake kupoteza ubunge kwa kutochaguliwa kwa sababu ya habari hizo ambazo ni za kupikwa au zenye lengo la kukichafua chama au Bwana Nassari.

  Watu wakisubiri serikali iyafungie magazeti hayo, hilo haliwezi kutokea hata siku moja. Muhimu ni Nassari mwenyewe kwa kushirikiana na CHADEMA wayashitaki magazeti husika au wayatake magazeti yaombe radhi kwa kuandika habari za kizushi.
   
 16. LENGIO

  LENGIO JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 1,032
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Wanafuata maelekezo ya kilaza nepi nauye.
   
Loading...