Joseph Warioba aeleza sababu zilizoilazimisha serikali kufuta Mahakama ya Kadhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joseph Warioba aeleza sababu zilizoilazimisha serikali kufuta Mahakama ya Kadhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Oct 13, 2009.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Mahakama ya Kadhi

  “Mahakama ya Kadhi, ina historia ndefu, tumekuwa tukiizungumza tangu 1971, siyo kwa msingi wa kidini, ni kwa msingi wa kitaifa. Labda turudi nyuma, tulipopata uhuru tulikuwa na mikondo tofauti ya Mahakama.

  Kulikuwa na Mahakama za kawaida, inatoka Mahakama hii unakata rufaa Mahakama ya juu, lakini pia ilikuwapo Mahakama ya natives unatoka kwenye baraza la chifu, unakwenda kwa DC, PC unakwenda kwa Gavana.

  Sisi tulipopata uhuru tukasema hapana, lazima tuwe na mfumo mmoja wa Mahakama. Kwa hiyo mwaka 1963 ilipitishwa sheria ya Mahakama - Magistrate Court Act, ndiyo ilianzisha mfumo mmoja waMahakama tukasema Mtanzania kama anatafuta haki anatumia utaratibu ule ule.

  Baada ya hapo tukaanza kuona sheria fulani fulani zinabagua, tuzibadili, tukaendelea. Ilipofika mwaka 1971 kuna sheria moja ambayo tulitaka tuitengeneze kwa ajili ya Watanzania wote, Sheria ya Ndoa. Serikali ilikuwa inakuja na sheria, basically ambayo inatambua ndoa ya mke mmoja.

  Ilipata upinzani mkubwa sana, mkubwa sana, Mnanka (Kiongozi wa kitaifa enzi hizo kutoka Musoma) alikuwa mmoja wa viongozi waliopinga kwa nguvu sana. Kwa hiyo, sheria hiyo ilipata upinzani kutoka kwa sheria za kimila na kiislamu. Waislamu wakasema kwa imani yao wanaweza kuoa mpaka wanawake wanne, wa mila wakasema idadi inategemea na uwezo wako.

  Kwa sababu ya upinzani ule, serikali ikaona kweli hapa hatuwezi kuleta sheria moja ambayo ni lazima ibane kila mmoja, ikasema basi, Serikali itakuwa na sheria yake, na hiyo inapokwenda kufunga ndoa kwenye ofisi ya serikali unaweza kutamka pale kama hiyo ndoa ni ya mke mmoja au zaidi ya mmoja, kwa hiyo sheria ikatambua jamii nzima.

  Lakini pia serikali ikasema tutatambua ndoa zote ambazo zinafungwa kihalali, iwe ya kimila, kikristo, kiislamu, kihindu, ya bahai, ikasema tunazitambua, ikifungwa ndoa kwa utaratibu huo ni halali nchini, tunachojitaji tu ni kwamba, baada ya kufunga ndoa hiyo njoo usajili, kwa hiyo suala la kusajili likawa la wote, na hakuna pingamizi, na talaka ikawa hivyo hivyo.

  Nakumbuka Wakristo, na hasa Wakatoliki hawakukubaliana na hili la talaka, kwamba umeoa, mmefunga ndoa kanisani mnaishi…kisha hampatani unakwenda mahakamani kuvunja ndoa hiyo. Wakristo wakasema haiwezekani, kama umefunga ndoa kikristo kuivunja ni kwa utaratibu wa kikristo, serikali ikasema hapana kwa sababu walitaka kwenye sheria iseme ndoa ya kikristo haiwezi kuvunjwa mahakamani.

  Serikali ikasema hapana, tunatengeneza sheria ambayo itatumiwa na kila mtu hatuwezi kusema hivyo, lakini hatuwazuii kuendelea na sheria zenu huko, kwa hiyo kama mtu ameoa kanisani kisha baadaye amekwenda akapata talaka mahakamani ninyi bado mna uwezo wenu wa kumwadhibu kwa sheria zenu huko na mpaka leo hii.

  Mkatoliki, ukifunga ndoa katoliki kisha ukaivunja mahakamani kanisa halitambui na litakuadhibu na kwa muumini hili si dogo, kuna watu ambao wamefunga ndoa na wametoa talaka, kanisa halikutambua wakataka kuoa tena ikabidi wafuate utaratibu wa dini kupata kibali.

  Lakini tulikubaliana kwa hilo. Baada tu ya sheria ya ndoa, tukataka tulete sheria ya mirathi lakini hii ndiyo haikuwezekana kabisa kwa sababu hizo hizo. Sheria ya mila wakapinga wakasema sisi tuna utaratibu wetu wa mirathi, Waislamu wakapinga tuna taratibu zetu, nadhani mara tatu Serikali ikajaribu.

  Mara ya kwanza, ilikuwa chini ya Mzee Kawawa, wakati ule 1971, masuala ya sheria yalikuwa chini ya Ofisi ya Makamu, haikuwa Wizara kamili. Kwa hiyo, Mzee Kawawa ndiye aliyepeleka pendekezo la kwanza, likakataliwa.

  Akaja Waziri Manning, mimi nikiwa Mwanasheria Mkuu wake, tukateua consultant (Mshauri mwelekezi) Profesa Weston, atufanyie utafiti alete mapendekezo tunawezaje kuwa na sheria ya mirathi, akatuletea tukapeleka ikakataliwa.

  Baadaye mimi nikawa Waziri wa Sheria nikasema ngoja nijaribu kuifufua tena, nikaenda kupata mawaidha kwa Mzee Kawawa, akaniambia Joseph hili utaliweza?...mimi nilishindwa, Waziri Manning akashindwa. Akasema haya mambo ambayo msingi wake ni imani na utamaduni si mambo ya kuharakisha, lazima itoke ridhaa kwa jamii yenyewe serikali iache.

  Lakini, wakati wote huo tuliendesha mambo haya kwa sura ya kitaifa ya umoja, hakukuwa kwamba wakati tunazungumza, waislamu wanasema hivi na wakristo wanasema hivi. Na wakati wote, Waislamu walikuwa wanasema sisi masuala ya mirathi yanaongozwa na Quran, na wanasema chombo kinachohusika ni Mahakama ya Kadhi, hawa wa mila wanasema taratibu zao, kwa hiyo tuliyatazama haya kwa msingi wa utaifa, miaka yote hiyo, hapakuwapo na mkwaruzano kwa misingi ya dini.

  Juzi juzi hapa, nimeangalia majadiliano ndani ya Bunge, akisimama mkristo anapinga Mahakama ya Kadhi, akisimama mwislamu anaunga mkono. Limekuwa ni suala la kidini, badala ya kuangalia katika mfumo wetu wa kitaifa unashughulikia masuala hayo kwa njia zipi. Sasa baada ya hapo imekuja waraka na mwongozo.”
   
 2. M

  MkuyuMkubwa Member

  #2
  Oct 13, 2009
  Joined: Sep 27, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM itekeleze tu ahadi yake ya kuanzisha mahakama ya kadhi. ndio maana ya ilani, na ndio siasa.....ukiahidi unatekeleza...ihukumiwe kwa ahadi zake. sio inaahidi kwenye ilani afu baadae inataka mjadala wa kitaifa wakati imekwisha ahidi
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu, Samahani lakini bado sijaelewa hizo sababu zilizopelekea kuvunjwa kwa mahakama ya kadhi. Tafadhali nieleweshe!
   
 4. October

  October JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hata kama walichoahidi hakina tija kwa taifa? Kama waisilamu wanataka Kadhi kwanini wasianzishe wenyewe? kwanini wanataka kadhi alipwe kwa kodi za wasio waisilamu?
   
 5. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa kifupi anachosema Warioba ni kwamba Mahakama na Kadhi pamoja na ile ya Natives zilivunjwa ili kutoa haki sawa kwa watanzania bila kubagua rangi, dini au jinsia. Ikabaki mfumo huu tulionao kwa sasa. Lakini hapo hapo mambo fulani fulani hususan ya kidini yaliachwa yaendeshwe kidini. Brilliant!!
   
Loading...