Greenwhich
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,337
- 968
Pamoja na Joseph Selasini Mbunge wa CHADEMA-Rombo kuchaguliwa kwa kishindo na waumini wa Kanisa Katoliki Dar kuwa Kiongozi wa Baraza la Walei Jimbo kuu la Dar uongozi wa Jimbo hilo umemuondoa kwenye nafasi hiyo.
Habari kutoka ndani ya Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar zinasema kuondolewa huko kwa Selasini ni ili kukabiliana na maadui wa Kanisa hilo wanaopita huku na huko kulichafua.
Vyanzo vya habari vinasema kuondolewa huko kwa Selasini ni sawa na kuua ndege wawili kwa jiwe moja.Hii ni kwa sababu kuna maadui wa kanisa Katoliki wanaolichafua Kanisa Katoliki kwamba linaunga mkono chama cha CHADEMA na pia kuna maadui wa Chama cha CHADEMA wanaopita huku na huko kwamba chama hicho kinafuata itikadi ya Kikristo.
Uongozi wa Jimbo umewaomba radhi sana waumini wake kwamba ingawa wanampenda sana Selasini lakini kwa vile yeye ni kiongozi wa juu wa CHADEMA imebidi aondolewe uongozi wa Kanisa ili maadui wasipate cha kusema.