Joseph Selasini wa CHADEMA aondolewa uongozi Kanisa Katoliki DAR

Greenwhich

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
1,337
968
Pamoja na Joseph Selasini Mbunge wa CHADEMA-Rombo kuchaguliwa kwa kishindo na waumini wa Kanisa Katoliki Dar kuwa Kiongozi wa Baraza la Walei Jimbo kuu la Dar uongozi wa Jimbo hilo umemuondoa kwenye nafasi hiyo.

Habari kutoka ndani ya Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar zinasema kuondolewa huko kwa Selasini ni ili kukabiliana na maadui wa Kanisa hilo wanaopita huku na huko kulichafua.

Vyanzo vya habari vinasema kuondolewa huko kwa Selasini ni sawa na kuua ndege wawili kwa jiwe moja.Hii ni kwa sababu kuna maadui wa kanisa Katoliki wanaolichafua Kanisa Katoliki kwamba linaunga mkono chama cha CHADEMA na pia kuna maadui wa Chama cha CHADEMA wanaopita huku na huko kwamba chama hicho kinafuata itikadi ya Kikristo.

Uongozi wa Jimbo umewaomba radhi sana waumini wake kwamba ingawa wanampenda sana Selasini lakini kwa vile yeye ni kiongozi wa juu wa CHADEMA imebidi aondolewe uongozi wa Kanisa ili maadui wasipate cha kusema.
 
Kwa nn wasinge mshauri mpema asigombee kuliko kusubiri mpaka uchaguzi?
 
Yeye kasema nini sababu ya kuondolewa kwake?

Mkuu kanisa katoliki huwa halipendi waongo ,na kama unakumbuka huyu Selasini ni kati ya wabunge waliosema uongo bungeni kuhusu sakata la kamati ya iliyikuwa ya nishati na madini.
 
Kanisa katoliki halina kugombea nafasi hizo ila ni kura za sili kwa yeyote unayemuona anfaa kati ya wajumbe ndiyo zimeangukia kwake. kanisa huwa linamwondoa yeyote hata kama angekuwa ccm na yupo ngazi za juu kwa sababu asije akatumia vibaya jukwaa la dini akaligeuza la siasa
 
Tusi tafune maneno hakuna m2 mwenhe akili timam asie jua kwamba cdm nichama cha kanisa anae bisha anyoshe kidole
 
Sioni tatizo la kuwa kiongozi wa walei,
na kuwa mbunge wa cdm.

they have been threatened by small minds with parochial way of outlook who could do nothing rather than calling it christian lobby,thus to avoid such allegations,the church decided to do so.
 
Tusi tafune maneno hakuna m2 mwenhe akili timam asie jua kwamba cdm nichama cha kanisa anae bisha anyoshe kidole

Ni wenye mtazamo fulani tu ndiwo wanaoihusisha CHADEMA na Kanisa, na watu wa aina hiyo ni vigumu kuwahusisha na akili timamu.
 
ngoja ningoje mama wa upako na mbunge wa kuteuliwa mchungaji rwakatare aje atie neno
 
I dought...mleta mada atakuwa na lake jambo.Kama Selasin kaondolewa uongozi basi ni kwa kushindwa kwa kura kitu ambacho ni cha kawaida kwenye uchaguzi wowote, otherwise Kanisa Katoliki haliwezi kumpokonya mtu uongozi kwa sababu za kiasa kwani Uongozi ni karama toka kwa Mungu na moja ya mapaji saba ya roho mtakatifu ambaye kwake kanisa katoliki linaamini pia.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom