Joseph Selasini: Katibu Mwenezi NCCR-Mageuzi ajiunga na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joseph Selasini: Katibu Mwenezi NCCR-Mageuzi ajiunga na CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ben Saanane, Aug 26, 2009.

 1. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Katika tukio jingine, Dk Slaa jana alimkabidhi kadi ya uanachama wa Chadema aliyekuwa katibu wa itikadi na uenezi wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini.

  Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hiyo, Selasini alisema, ameamua kufanya hivyo ili kuendeleza mapambano ya kisiasa kupitia chama hicho ambacho alisema kimeonekana kuwa na nia ya dhati kuwafikia wananchi.
  Alisema kuhamia kwake Chadema kutampa fursa ya kuwania ubunge wa jimbo la Rombo kama chama kitampitisha ili aweze kupambana na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Basil Mramba.

  Source:Mwananchi

  NB:Nia yake CHADEMA ni hiyo tu? Basi ni rahisi sana kwa mamluki kujipenyeza ndani ya chama.
   
 2. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ben,
  Kwasasa nia ya upinzani na watanganyika wote kwa ujumla ni kuwang'oa mafisadi popote pale walipo kwa nanmna yeyote ile!! naamini bw. Selasini ni mtu makini na ana uwezo na mbinu kali za kumng'oa Basil. Tatizo lilikuwa ni kule NCCR ambako mambo yalikuwa hayajakaa mswano! huyu bwana ni moto sana uliza wanaomfahamu watakwambia!
  Amani.
   
 3. M

  Mpingo1 Member

  #3
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama nitakuwa nimekosea, naomba mnisahihishe.

  Nadhani huyu ni ndugu wa Dr. Masumbuko Lamwai na ni watoto wa Mzee Selasini ambaye ni diwani wa Shimbi (Rombo) ambayo ni kata ya Mr. Mramba.

  Katika mazingira hayo, sina uhakika kama kijana ameamua kupambana na wazee wake, au ni dalili kwamba wazee wamesema siasa sasa basi! Huko nyuma, mzee Selasini alikuwa akiwaambia wanae wanaweza kuwa wanasiasa huko waliko lakini sio wakienda Rombo.......
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Daily News; Tuesday,October 16, 2007 @00:03


  [​IMG]
  "Sikujua wito wangu ni upi kati ya utumishi wa kanisa kama padri au shughuli nyingine za kijamii zikuwemo siasa, kwa sababu tangu utoto mimi nilikuwa natumika kanisani kama mtumishi na hata shule nilizosoma kuanzia ngazi ya sekondari ni Seminari na nilimaliza masomo yote ya upadri ndipo nikatafakari na kuona nina wito tofauti na huo nikamuomba Askofu wangu aniruhusu niende duniani", ni kauli ya Joseph Selasini ambaye hivi sasa ni Katibu Mwenezi wa Chama cha NCCR-Mageuzi.  Selasini ni mtoto wa tano kuzaliwa katika familia ya watoto 11, wakiwemo wa kike saba na wakiume wanne, alizaliwa Juni 4, mwaka 1958 Rombo-Mkuu mkoani Kilimanjaro ambapo elimu yake ya msingi alisoma katika shule tatu tofauti kufuatana na mazingira za kazi ya baba yake alivyokuwa akihamishwa.  Mwanasiasa huyo ambaye kwa mtu wa kawaida anaweza kushangaa jinsi alivyofanya uamuzi wake wa kuacha utumishi wa kanisa na kuingia kwenye masuala ya siasa, kwa kuwa kwa historia yake amelelewa kwenye maadili ya kikanisa zaidi yenye matendo ya kiroho kuliko matendo ya kidunia na mambo ya siasa kwenye majukwaa.
  Akizungumza na Mwandishi wa Makala haya kwenye mahojiano maalumu kuhusu uamuzi wake wa kujihusisha na masuala ya siasa na dini kwa pamoja hivi sasa, Selasini anasema yeye kwake haoni shida kutumikia kanisa lake na kuwa mwanasiasa kwa kuwa anaamini kuwa hata mwanasiasa ni mmoja wa viumbe vya Mungu ilimradi siasa inayofanywa iwe ni kwa manufaa ya umma na Taifa badala ya kuwafarakanisha wananchi.  "Mimi kwangu sioni tabu kwanza ya kuamua kufanya mambo mengine tofauti na utumishi niliokulia tangu awali yaani upadri, ingawa nilisoma masomo yote na kufikia ngazi ya kuwa padri, lakini niliona wito wangu sio huo nikamuomba Askofu wangu Marehemu James Sangu wa Jimbo la Mbeya kwa wakati huo, aniruhusu nitafute utaratibu mwingine wa maisha yangu nje ya upadri naye alikubali nikaondoka",anasema Selasini.  Anasema alianza kujihusisha na masuala ya siasa mwaka 1990, kipindi hicho akifanya kazi katika Benki ya Nyumba nchini (THB), na anakumbuka kuwa siku moja alitembelewa na Marehemu Kassim Haidari Maguto ambaye alimwambia kuwa ameelekezwa na kaka yake Masumbuko Lamwai aje kumuomba (Selasini ) kujiunga kwenye vuguvugu la mageuzi ambalo tayari lilikuwa limeshanza na lilikuwa likiongozwa na wana mageuzi 15.
  Anasema baada ya kuletewa ujumbe huo, wa kuombwa kujiunga kwenye harakati za kuleta mageuzi alikubali na wakati huo wana mageuzi hao 15 baadhi yao ni pamoja na Chifu Abdalah Fundikira, Mabere Marando, Prince Bagenda, Mashaka Chimoto,Ndimala Tegambwage, James Mbatia, Anton Komu, James Mapalala na Christopher Mtikila.  Selasini anaendelea kusema mageuzi hayo ni yale ya kuishinikiza serikali kufanya mabadiliko kwenye sheria zake mbalimbali zinazokandamiza, pia kufanya mabadiliko ya Katiba ya nchi ili kuruhusu kuwepo na mfumo wa vyama vingi vya siasa, kuwa na vyama huru vya wafanyakazi, kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa na kuondoa Jeshi kwenye masuala ya kisiasa .  Anasema harakati hizo zilifanikiwa kwa kiasi ambapo Juni mwaka 1991, walifanya mkutano wa kitaifa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo walitoa tamko kuhusiana na madai hayo na Kamati hiyo ya wana mageuzi ilijulikana kama Kamati ya Kitaifa ya Mabadiliko ya Kikatiba (NCCR), na kuwa serikali ilisikia madai yao na kupitisha sheria ya kuanzishwa kwa vyama vingi.  Selasini ambaye ni baba wa watoto wanne ana mke mmoja wa ndoa na wanaishi Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na anasema kuwa baada ya kuundwa kwa sheria ya vyama vingi mwaka 1992, Kamati hiyo ya NCCR iligawanyika ambapo Mtikila aliondoka na kwenda kuanzisha chama chake Democratic Party (DP), na Fundikira kuanzisha chake cha (UMD), ambapo Mabere Marandu pamoja na hao wana mageuzi waliongezea jina la Kamati hiyo na kukifanya chama cha NCCR-Mageuzi ambacho kilikuwa chini ya Mwenyekiti Mabere na Katibu wake Prince Bagenda.  Anasema mwaka 1993, NCCR-Mageuzi ilizaliwa rasmi na yeye kuwa Katibu wa Vijana ambapo James Mbatia alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kundi hilo na mwaka 1995 Mwenyekiti wa sasa wa chama cha TLP, Augustine Mrema alijiunga na chama hicho na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti na yeye kuwa Msaidizi wake, ambapo mwaka 1997 hadi 2000 alichaguliwa kuwa Afisa Utawala wa chama na baadaye kuwa Katibu Mwenezi Taifa wa chama hicho nafasi anayoishikilia hadi leo.  Akizungumzia maisha yake kabla ya siasa, Selasini anasema alianza shule ya msingi Mkuu Extended iliyoko wilayani Rombo mwaka 1969 ambapo alisoma hadi dasara la pili, na wakati huo baba yake alikuwa mkuu wa shule hiyo na aliteuliwa kwenda kuwa Afisa Tawala wa Elimu ya Watu Wazima wilayani Kilosa ambapo aliondoka naye na kwenda kusoma darasa la tatu na la nne katika Shule ya Mazinyungu mkoani Morogoro.  "Hata hivyo sikumaliza darasa la saba shuleni hapo, kwani baba alipata tena promosheni ya kwenda kuwa Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya, na tulihama naye na mimi nikaenda kusoma Shule ya Msingi Majengo katika Manispaa ya Mbeya ambapo nilimaliza darasa la saba na kuchaguliwa kujiunga na shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya, lakini kwa kuwa nilipenda kutumikia kanisani niliomba kujiunga na seminari hivyo nikachaguliwa kwenda Seminari ya Kaengesa iliyopo mkoani Rukwa", anasema Selasini.  Anasema alisoma kwa miaka minne hadi mwaka 1979 ambapo alipomaliza yeye na wenzake waliandaliwa kwa mafunzo ya mwaka mmoja katika kituo cha Katandala wilayani Sumbawanga mjini ili baadaye waende kusoma Filosofia ya upadri.  Baada ya kumaliza masomo hayo baadhi yao walichaguliwa kuendelea na masomo ya Filosofia na wengine akiwamo yeye kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita ambapo walipelekwa Seminari ya Itaga mkoani Tabora, ambapo alisoma
  masomo ya Historia, Jiografia na Uchumi (HGE).  "Nakumbuka wenzangu tuliomaliza nao kidato cha nne na kusoma mwaka wa maandalizi lakini na wakati wa kugawanywa wao waliendelea na masomo ya filosofia na mimi kwenda kidato cha tano leo hii wao ni mapadri wakiwemo Father Athur Mwakasagule aliyepo Mbeya, Deo Katumbu (Sumbawanga),Vitus Sichalwe yeye yuko Barza la Maaskofu Kurasini jijini hapa(TEC) na wengine wengi", anasema Selasini.  Hakuishia hapo kwani ndoto yake bado haijatafsiriwa ili kujua ni nini wito wake, na mwaka 1982 alikwenda Jeshi la kujenga Taifa kwenye kambi ya Magange mkoani Tabora ambapo baada ya kumaliza alijiunga na seminari ya Kibosho kwa masomo ya miaka miwili ya Filosofia ya upadri.  Anasema alipomaliza alirejea jijini na kujiunga na Seminari ya Segerea ambako alisoma theolijia kwa miaka mingine mitatu na alipomaliza alijitafiti na kuona ana wito mwingine tofauti na upadri hivyo akaomba aondoke na kwenda kufanya mambo mengine nje ya utumishi kama padri.  "Safari yangu ikaanza ya kwenda duniani kutumikia wananchi na Taifa langu na sio tena kanisa kama mtumishi kwa nafasi ya upadri, kwani mwaka 1988 niliajiriwa katika Benki ya Nyumba (THB)kama Karani wa Hesabu za Mikopo ambapo mwaka uliofuata niliteuliwa kuwa Afisa Utumishi daraja la kwanza na pia kadri miaka ilivyokwenda nilipandishwa cheo na kuwa Meneja Utawala na Uendeshaji",anasema Selasini.  Anasema mwaka 1993, alibadilishwa kazi na kuwa Afisa Miliki Mwandamizi wa Estate za benki hiyo na mwaka uliofuata benki ilifilisiwa na yeye kujiajiri kama mjasiriamali na kipindi hicho ndipo aliamua kuoa na kipindi hicho kabla ya benki kufilisiwa alikuwa tayari ameshaanza kujihusisha na masuala ya siasa baada ya kuombwa na mwanamageuzi.
  Selasini anamalizia kwa kusema pamoja na kupenda siasa bado anatumikia kanisa lake kwa kujihusisha na mambo mbalimbali katika Parokea yake ya Pugu ambapo ni Mwenyekiti wa Parokia hiyo na pia ni Makamu Mwenyekiti wa Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kuwa katika siasa anachukia uongo unaotolewa na baadhi ya wanasiasa kwa mtindo wa propaganda ambao unaharibu sifa na majina ya wanasiasa wengine, na kuomba tabia hiyo iachwe kwani taifa ni la kila mmoja kulitumikia kwa nafasi yake ili kuleta maendeleo na sio kulibomoa.


  NB: Sasa hiyo ndiyo CV yake! Akipambana na Mramba huyu,si Itakua ni sawa na Mramba kupita bila kupingwa?Sasa hivi tunahitaji kuwa na wabunge ambao wana upeo mkubwa katika mabadiliko ya kiuchumi na si kupiga siasa tu....huku tunakoelekea kama tutakua na wabunge wa aina hii tutaweza vipi kushindana na Nchi nyingine zinazokua kiuchumi kama Kenya,south Africa,Ghana au kufikia walikofikia South Korea na Singapore?CHADEMA lengo letu ni kutoa mawazo mbadala,na uongozi mbadala.Nashangaa kuona mtu ambaye ana experience ya uanamageuzi hadi kupewa cheo cha juu ndani ya NCCR-Mageuzi leo anatoa malengo mafupi namna hii ya kuwania ubunge tu. Ametekeleza haki yake ya kikatiba kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa but,CHADEMA as a serious party inabidi kuwa makini linapotokea suala la wanachama mashuhuri kama huyu mzee kuweka malengo mafupi.Hata hivyo Umri wake pia litakua suala lingine,Mramba anahitaji Serious Challenge kutoka kwa kijana ambae akili inachemka.Ndiyo maana Mnyika aliweza kumkimbiza Vibaya Keenja kwenye jimbo la Ubungo 2005,au Zitto kule Kigoma kaskazini. Mh.Joseph Selasini au wadau wengine mnakaribishwa kwenye mjadala
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mkuu Heshima Mbele...

  Ingawa mimi mwenyewe sijui ila kwa kuifahamu Rombo...sithani kama Mzee Salasini ni mzazi wa Dr M. Lamwai. Sina sababu nyingine yenye nguvu zaidi ya kuona majina yao ya Ukoo hayafanani..!!

  Hata hivyo, kumshinda Mramba Rombo ni kazi sana kwa sababu miaka ya karibuni kumekuwa na pilika pilika za kujenga barabara kule, maji na umeme vimefika maeneo mengi. Ukiweka hayo mapoja na ukweli kuwa Mramba atakuwa bado ana hela za ufisadi, huyo mpinzani wake aje na nguvu za ziada.
   
 6. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ndio huyu Joseph mdogo wa Masumbuko alisomea upadri pale Kaengesa seminari Sumbawanga! Siku zote yeye na baba huwa hawapikiki chungu kimoja katika mambo ya siasa. Baba ni CCM damu na yeye ni mpinzani damu!
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280

  Ndiyo maana nikasema hapa CHADEMA inabidi kuwa makini sana,isije kuwa ni dili la kupunguza upinzani kwa Mramba next year.

  Pia huyu mzee umri wake umeenda sana.Utaona huyu jamaa katika kura za maoni akibwagwa halafu mwingine akipitishwa basi atahamia CCM kabisa akisubria kum-replace mramba akistaafu ili nae aingie kama mzee wa makamo.Tanzania haiwezi kwenda hivyo,baba yake ni diwani katika kata ya Mramba,na Ninavyomjua mramba ni mtu wa kutumia hela kuwatuliza madiwani kwanza.Sasa baba yake kama ameshafikia hatua ya kumkataza kuwa mwanasiasa Rombo unadhani Mramba akicheza na Rupia itakuaje? Infact,Mramba anatakiwa kukimbizwa na vijana tu? Huyu jamaa anatia wasiwasi,malengo yake ni ubunge tu? Unajua Mramba anatakiwa kukimbizwa na vijana kwani mtaji wake ni campaign timu ya opposition Rombo haipigi kampeni ya Nyumba kwa Nyumba,na tusisahauMramba amekua kwenye kampeni tangu alipochaguliwa 2005,hapa ndipo linapokuja suala la umuhimu wa vijana wachangamfu na wasomi kupambana na Mramba kwa kampeni
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280

  Mkuu Yebo Yebo,

  Umeongea point,Ili kupambana na Mramba pale Rombo kunahitajika kampeni ya Nyumba kwa nyumba.Najua uzoefo wa Mramba na MBA yake mpaka sasa hivi atakua anfanya SWOT Analysis. Pia huyu mzee sidhani kama anawaelewa watu wa Rombo Kama Mramba kwa kuwa hajakaa nao sana,kama alitoka huko akiwa std 3 unategemea nini?

  Pia Baba yake huyu jamaa atakua kikwazo kikubwa sana kama Mramba akishupalia Propaganda na pesa hapo,najua anaweza sema mbona Dr.Slaa ni CHADEMA na Mkewe ni CCM? Hii ni kesi tofauti coz nawajua sana wananchi wa Rombo


  Halafu suala lingine inabidi Rombo iwe na Mbunge atakaeweza kutunga miradi na kutafuta funds for the Big Projects kama za Mramba na aweze kuwashawishi wapiga kura kama kweli aneweza kufanya kazi ya aina hiyo.Ikumbukwe Jimbo la Rombo lilikuwa na mbunge kutoka CHADEMA mwaka 1995-2000 likiongozwa na Justine Alfred Salakana. Lakini jamaa hakufanya anything watu wakasema heri Mramba na wengine heri Leonce Silayo Ngalai aliyekuja kufariki dunia mwishoni mwa miaka ya 90' na alikua mpinzani mkubwa wa salakana kwa wakati huo ktk kambi ya upinzani huku kwa upande wa CCM akiwepo Mrambaaliyebwagwa na Salakana.

  Mkapa alimpa Mramba ukuu wa mkoa wa Mbeya na 2000 ilipofika akagombea,lakini salakana hakugombea.

  Leo hii salakana ni Mwanchama wa CCM.Sasa tunapoangalia historia ya jimbo la Rombo kwa kweli inabidi CHADEMA tuwe makini na tusirudie tena makosa.Mramba anahitaji mbinu kali na mtu anaeifahamu Rombo kuchuana nae ili kurudisha hilo jimbo.

  Ni bora kuangalia msimamo wa mtu,nia yake,uwezo wake kiuongozi na kitaaluma na ufahamu wakewa masuala makubwa na ya muhimu dunia ili tuwe na raslimali watu makini katika kukuza uchumi wa nchi yetu,pia katika taifa letu kuna tatizo la allocation of resources.Hili tatizo limechangiwa sana kutokana na wabunge wetu ku-endorse budget iliyo na mapungufu ktk allocation of resources.

  So,mbunge awe na uwezo wa kujenga hoja za kiuchumi na kijamii zaidi kuliko za kisia ili tupige hatua kwa haraka.Now CHADEMA we have to be serious on this kama kweli tunatoa uongozi mbadala au tuna-represent an alternative views(mwazo mbadala
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Joseph Selasini, welcome home!
   
 10. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ben,
  Kwa mtazamo wangu naona kabisa bado una zile hisia za kizamani za nani mkali kati ya NCCR na CHADEMA. Hisia hizo ndizo zilizorudisha upinzani nyuma kwa miaka mingi! hivi unataka kila mbunge awe na CV ya aina gani? kwani CV ya mwenyekiti Freeman ikoje?.

  IMHO Joseph Selasini anao uwezo na uzoefu mkubwa sana wa kukabiliana na mikikimikiki ya dizaini za akina Basil na pia kuwaletea maendeleo wana Rombo bila kutumia pesa za kifisadi ama kufanya upendeleo kwenye bajeti yetu kama alivyokuwa akifanya Basil.

  Kumbuka safari hii Rombo hatutaki kuishia tu kutoa serious challenge kama ulivyosema Mnyika kwa Keenja bali tunataka ushindi kamili!!

  Mwisho naomba uthibitishie jamvi kama Basil bado ataruhusiwa kugombea ubunge pamoja na kesi zinazomkabili!
  Amani.
   
 11. M

  Mpingo1 Member

  #11
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thanks for clarifications. Ninamfahamu vizuri huyu mzee na jinsi asivyopikika chungu kimoja na wanae kwa sababu za kisiasa. Dr. Lamwai aliamua kunyoosha mikono na kurudi kundini!......

  Tusubiri tuone siasa za Rombo zitakavyoendelea.........
   
 12. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu mbona unasoma katiba kwa haraka, Basil hajahukumiwa na hivyo katiba inamruhusu kugombea ubunge. Soma ibara ya 67 ya katiba ya Jamhuri.
   
 13. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wanasiasa wanaokimbia vyama kwa sababu wanataka kugombea vyeo ni wa kuogopa sana.
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ndahani hunielewi,

  Suala langu ni kuwa na mgombea mwenye malengo mafupi ya Ubunge tu,hivi leo hii akigombea halafu akabwagwa na akakimbilia chama kingine au akaenda CCM kwa baba yake CHADEMA kama taasisi ya kisiasa wataonekanaje? Mgombea mwingine katika uchaguzi utakaofuatwa atakua ktk hali gani?Wananchi wataweza kumchukulia yeye au Chama serious kweli? Lazima tuwe na malengo mapana.

  Sina tatizo kama hilo ulilotaja mkuu,eti kwamba nani zaidi kati ya CHADEMA na CCM? Hapana,mbona sikupinga ujio wa Mwita Mwikabe aliekua mwenye kiti UVCCM Tanga? Mbona sikumpinga Lwakatare anetoka CUF tena chama kikubwa chenye nguvu karibia sawa na CHADEMA na mtu aliekua katibu mkuu wa CUF upande wa Bara kujiunga na CHADEMA?

  Ni kwa kuwa nimeona malengo mafupi ya kutaka madaraka,kumbuka haya ndiyo yanayoufanya upinzani usikue hapa Tanzania


  Na mwisho kabisa ndugu yangu,sina uwezo wa kuthibitisha kama Mramba atagombea ama laa,lakini nimekua nikitumia Mramba kama kigezo cha kumpima prospective candidate wa Jimbo la Rombo ili Mramba akiamua kugombea basi upinzani uwe na mgombea imara bila kujali mramba atashinda ama la,manake Si lengo letu kumtoa mramba pale Rombo tu.

  Pia,katika kuangalia vikwazo ni bora ufanye overestimation ya tatizo ili ukikuta ni dogo uweze kuli-solve haraka kuliko kuli-underestimate kisha uaibike.Tumia kipimo kama cha Mramba ili asipogombea ushindi uwe wa kimbuka,pia akigombea tusidhalilishwe.

  Pia umesema tunahitaji ushindi kamili,nimetoa mfano wa Zitto na Mnyika but you have chosen to pick one ukaacha mwingine.....Lengo ni kuchukuua ubunge Rombo na pia kuwa na mbunge makini sio kuishia kuwa mwanaharakati tu wa sisa za ndani lakini ikifikia kipindi kama cha bajeti unashindwa uelekeze wapi hizo harakati zako.Angalao tuwe na wabunge makini kama wa South korea,au Japan.Wabunge wenye mbinu za kuendeleza jimbo kiuchumi na kijamii.Uliza tena mkuu,pia asante
   
 15. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #15
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Yaani mtu anachukua kadi tu na kuulipukia ubunge,je ni juzi juzi tu ameona chadema kina sera nzuri kama kweli ni mwanaharakati makini?

  Pia wanasiasa wa aina hii wanaweza kukiweka CHAMA pabaya sana huko baadaye.Huyo anataka kubebwa na kazi zilizofanywa na wabunge machachari wenye malengo marefu na CHADEMA wakati huo akitega tu pembeni.Huyo nina mashaka san na nia yake au dhamira safi ya kuwakomboa au kuwasadia wananchi wa Rombo na pia commitment in achieving party's long term objectives unless we so Desperate to that level.Thanks na maoni tu!
   
 16. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sawa kaka,
  Je na CCM wata-risk kumruhusu/kumpitisha?. Pia kumbuka kuna system yao mpya ktk uchaguzi ujao. i.e, wagombea watakua wanazunguka jimbo zima wakiwa-pamoja huku wakikutana na kukampeni mbele ya wanachama/wapiga KULA wao wote ana kwa ana!!. Pamoja na Basil kujulikana kwa kiburi chake safari hii sidhani kama atathubutu kuchukua hiyo fomu! ni kama vile kufungulia mapipa ya minyoo na uozo!
  Kwa kifupi Basil hata iwe vipi hatagombea na kama akigombea hatashinda..
   
 17. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280

  Mkuu Mpingo, kwa ufahamu wangu mzee Selasini ni diwani wa kata ya Makiidi na sio Shimbi, ila ni kweli Selasini na Dk Lamwai ni watoto wa mzee Roman Selasini ambaye ni diwani kwa tiketi ya CCM. DK Lamwai kama mjuavyo mambo yalimzidia ikabidi arudishe majeshi CCM. Sasa ndo kabaki mdogo mtu so itakuwa ni mmoja kwa wawili.
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Aug 26, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu sasa hapo tupo ukurasa mmoja,

  Ila kwa jimbo la Rombo mramba anawajua sana,na nilikua nimechukizwa na ile kasumba ya watu wa Rombo kumpitisha mramba ndani ya CCM bila kupingwa,nilipokua naingia university 2005 nikashuhudia hawa jamaa jinsi mramba alivyokua akiwa manipulate,nikajua kiboko yake sasa ni hoja na uwaelewe vizuri wananchi wa Rombo na kampeni kali ya nyumba kwa nyumba tu.I'm out
   
 19. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani huyu Selasini mdogo hawezi kupambana na Mramba, kwa sababu yeye Mramba anapimwa kwa bara bara tu ambayo inajengwa sasa kwa kiwango cha lami, sijui imefikia wapi.

  Pili, wananchi wanaijua political dynasty ya the Selasinis, so kama ni mabadiliko kwanza watapenda wapate mtu mpya kabisa kutoka sehemu nyingine mwenye uwezo wa kuwashawishi watu kama ulivosema, kwa hoja tofauti na ikibidi hoja zenye uwezekano mkubwa wa kuwa tangible.
   
 20. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mbona tuko pamoja mkuu!
  Ondoa hofu, kumbuka tunamzungumzia mtu ambaye kwa muda wake wote wa kisiasa amekuwa akipambana na CCM na amekuwa akifanya hivyo akiwasaidia wagombea Urais na ubunge mbalimbali wa vyama vya upinzani japokuwa si kwa kupitia medium ya CHADEMA.

  Kwa mantiki hiyo basi sioni tatizo kama leo hii akiamua yeye mwenyewe kugombea ubunge japo kwa kupitia mgongo wa CHADEMA! bw. Selasini hana nia ya kuua upinzani ama kuja-kuidhoofisha CHADEMA.

  Kama CHADEMA watatoa mgombea mwingine mwenye sifa na uwezo wa kumng'oa Basil basi apitishwe!

  Je una hakika gani kama bw. Selasini atashindwa kuwaletea maendeleo wana-Rombo kama ulivyosema, nakunukuu: "ikifikia kipindi kama cha bajeti unashindwa uelekeze wapi hizo harakati zako."

  Mi nadhani ni vyema CCM ikaangushwa Rombo kwanza, alafu nyie wana-Rombo wenye ujuzi na utaalam mtamsaidia mbunge wenu kuleta maendeleo kwa pamojah!

  NB: Mara nyingi watu wenye nyadhIfa ama sifa kubwa wanapohama/hamia chama kingine huwa ni strategic move ya chama husika haswa kipindi cha uchaguzi kinapokaribia kwa hiyo basi usijeshangaa siku moja ukaambiwa kwamba ni wazee wa CHADEMA ndio waliomua-approach bw.Selasini ili aje agombee na wala sio vice versa!

  Amani
   
Loading...