Uchaguzi 2020 Joseph Selasini, aviangukia vyama kuwasamehe vijana walioshindwa kura za maoni baada ya kuvihama vyama vyao

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Mbunge wa Rombo aliyemaliza muda wake Joseph Selasini, ameviomba vyama vyote nchini kuhakikisha vinawapokea vijana wote waliohama vyao vyao na kuhamia vyama vingine lakini wakashindwa kwenye kura za maoni kwa kuwa walishaonesha wanao uwezo wa kufanya kazi.

Selasini ametoa kauli hiyo hii leo Agosti 7, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi na kuongeza kuwa vijana hao wanapashwa kuwapokea na kisha kuwalea na kuwarekebisha kwenye makosa yao na kuwapa nafasi za uongozi.

"Naviomba vyama vyote, chama changu cha NCCR-Mageuzi, CCM, CHADEMA tusiwatupe vijana, hata vijana ambao walihama kutoka CHADEMA kwenda CCM wakaenda kushindwa kwenye kura za maoni, tunajua vijana wanavyotangatanga hata katika kutafuta uchumba, wanatafuta fursa fungueni milango hao vijana warudi waweze, kufanya kazi ya Watanzania" amesema Selasini.

CC: Lijualikali.
 
Huyu mzee ni mpumbavu aliyepindukia. Mods nisameheni. Kwa iyo siasa zinazobeba hatma ya maisha yetu watanzania yeye anataka tuzichukulie kama fursa za kimaisha?????

Huyu mtu bora aliondoka Chama makini chadema. Kwa akili hizi anastahili kuwepo huko NCCR au CCM ambako watu wanachukulia hatma za maisha zetu kama fursa zao za kiuchumi.

Kanipa hasira sana. Ndo mana nchi hii hatuendelei kwa kweli. Akili kama hizi hazitakiwi kabisa kuwepo kwenye kada ya uongozi
 
Back
Top Bottom