Joseph Selasini asema tatizo la CHADEMA ukiwa na mawazo tofauti unaitwa 'Snitch', Msaliti, Usalama, unatumika na mwisho, unataka kuhama

Selasini aliyasema hayo jana baada ya kuhojiwa na Mwandishi wa Mwananchi aliyetaka kujua kuhusu tetesi kuwa anataka kutimkia CCM.

Selasini alikuwa akihojiwa kuhusiana na kujiuzulu kwake kukaimu nafasi ya Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

"Unajua Selasini amekaimu nafasi hiyo kwa maneno tangu Lissu alipokuwa na ule mkasa. Unajua kama Mbowe angeiandikia barua ofisi ya Bunge kumtambua ina maana Selasini angepata stahiki za mnadhimu kama vile posho ya kila mwezi, nyumba na ofisi.

Lakini Selasini alipokuwa anakwenda kudai, anaambiwa hakuna barua ya utambulisho na Selasini kamwambia mara kadhaa Mbowe aiandikie barua ofisi ya Bunge lakini hakufanya hivyo. Alisema mmoja wa Wabunge wa CHADEMA aliyeomba hifadhi ya jina lake"

Chanzo: Mwananchi

Pia soma

i. News Alert: - Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ajiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni

ii. Mbowe amshangaa Selasini kujiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Upinzani Bungeni, asema sababu alizotoa hazina mashiko
Huwezi hama kama huna pa kwenda,akachukue dau tu.Hao mamluki waende ccm jamaa akawape teuzi watazitumia kuibomoa ccm
 
Augustine Moshi,
ruhusuni siasa muone nguvu ya chadema , acheni propaganda za kichovu
Nguvu ya Chadema ilitokana na kupigia kelele ufisadi. You (we, as I supported Chadema wholeheartedly and made financial contribution) lost that when we dumped Slaa and embraced the person we had identified as the personification of corruption.

We have lost the plot, I am afraid.
 
Ujinga ajizi ya njaa

Unapotaka kuhama nenda kwa amani hiyo ndiyo hekima.

Unapoachia ngazi achia kwa hekima, adabu na busara. Tulia na ulinde heshima yako

Kubweka kama mbwa ni inshara ya mnafiki, muovu na asiye na staha

Unafiki ni kitu kibaya sana.
Acha ipenye vizuri
 
Nguvu ya Chadema ilitokana na kupigia kelele ufisadi. You (we, as I supported Chadema wholeheartedly and made financial contribution) lost that when we dumped Slaa and embraced the person we had identified as the personification of corruption.

We have lost the plot, I am afraid.
Where is Dr Slaa now ? namna Dr Slaa alivyojiunga na ccm ni namna ya kusikitisha sana ! ipo video nikikuonyesha utamsononekea sana , kurudi ccm ni kuondoa heshima yote aliyokuwa nayo
 
Suala sio mawazo tofauti bali hayo mawazo tofauti yana impact gani kwenye afya ya chama.

Wapo watu wengi wanaona kwa kuwa wana uhuru wa kutoa maoni na mawazo basi wanadhani kila wazo lao au maoni yao hata ya hovyo basi yanapaswa kupokelewa.

Ikiwa umeto maoni yako (inayoyaita tofauti) kati ya kundi la watu 100, wakakukatalia kwa hoja na wewe unataka kulazimisha basi sepa tu.

CHADEMA DAIMA.

Hivi nyie mbona mnalillia kila leo uhuru wa maoni wakati hamtaki kuonesha kwa vitendo huo uhuru wa maoni?


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hivi nyie mbona mnalillia kila leo uhuru wa maoni wakati hamtaki kuonesha kwa vitendo huo uhuru wa maoni?


Sent from my iPhone using Tapatalk

Kanywimwa uhuru upi ? Yeye sio chama kwamba akiropoka akubaliwe. Akigomewa anaehuka kuenda kusema hakuna haki.
 
makosa ya Mbowe yanapotetewa kqa nguvu zote.....
Hayo maslahi ameyafahamu leo,amekaa miaka miwili na ushee hajaandikiwa barua yakukaimu akaona sawa tu,sasa nikipi kimemsibu mpaka akaanza kulalama wakati miezi minne ijayo bunge litavunjwa kupisha uchaguzi.
Na kama kweli hajaandikiwa barua ya kukaimu iweje yeye anaandika barua ya kujiuzulu?.
Huyu ana lake jambo si bure.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom