Joseph Selasini aomba Mahakama imuongeze muda kesi ya kumlipa Mbatia Tsh. Bil 3

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,366
8,101
Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bara, Joseph Selasinametoa ombi hilo katika Mahakama Kuu, Masjala kwa maelezo kuwa bado anakamilisha nyaraka za utetezi.

Katika ya msingi namba 184/2022, Mbatia anaiomba Mahakama itamke kuwa tuhuma alizozitoa Selasini dhidi yake ni za uongo, na hivyo imwamuru amuombe radhi hadharani na kumlipa fidia ya Tsh. Bilioni 3.

Jaji Obadia Bwegoge ameahirisha kesi hadi Januari 17, 2023 kwaajili ya kusikiliza maombi ya Selasini na kuamua kama sababu za kuomba kuongezewa muda ni za msingi.
1669726226065.png

====================

Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi (Bara), Joseph Selasin ameiomba Mahakama Kuu Masjala Kuu, imuongezea muda ili aweze kuwasilishwa nyaraka za utetezi.

Selasini amefunguliwa kesi mahakamani hapo na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia akimtaka amlipe Sh3 bilioni kwa madai amemdhalilisha.

Maombi hayo madogo namba 541/22 yamewasilishwa mahakamani hapo leo Jumanne Novemba 29, 2022 na Wakili wa utetezi, Hassan Mkwanya mbele ya Jaji Obadia Bwegoge.

Wakili Mkwanya amedai Novemba 23, 2022 alipokea maelekezo ya kumwakilisha Selasini ambapo ilikuwa ni nje ya muda unaotakiwa kuwasilisha utetezi kisheria.

"Nilipoangalia nilikuta siku 21 za kuwasilisha utetezi kisheria zimepita, tukaona tuwasilishe maombi ya kuongezewa muda kwaajili ya kuleta utetezi," alidai Wakili Makwanya.

Wakili wa Mbatia, Hurdson Mchau alidai siku 21 zimeisha tangu Novemba 18 na Wakili wa utetezi alipata taarifa hiyo Novemba 23, hata nakala ya maombi hawajaiona na kuiomba mahakama kupanga tarehe ya karibu ili kuona maombi hayo yana sababu za msingi.

Hata hivyo, Jaji Bwegoge ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 17, 2023 kwaajili ya kusikiliza maombi ya Selasini kama sababu za kuomba kuongezewa muda ni za msingi au la.

Katika kesi hiyo ya msingi namba 184/2022, Mbatia anaiomba mahakama itamke kuwa tuhuma alizozitoa Selasini dhidi yake ni za uwongo, imwamuru amuombe radhi hadharani na kisha amlipe fidia ya Sh3 bilioni.

MWANANCHI
 
Hii Selasini hatoboi kabisa. Makosa ya wakili/uzembe wa kutozingatia muda si sababu ya msingi kutofika mahakamani tarehe iliyopangwa.... si utetezi wenye mashiko.....

soma hii:
Counsel submitted that, applicant and his counsel ought to know that there was change of the law. In short, he submitted that both applicant and his counsel were negligent. He cited the case of Kambona Charles v. Elizabeth Charles, Civil Application No. 529/17 of 2019, CAT (unreported) wherein the Court of Appeal held that a mistake made by a party’s advocate through negligence or lack of diligence cannot constitute a ground for condonation of delay. C
 
Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bara, Joseph Selasinametoa ombi hilo katika Mahakama Kuu, Masjala kwa maelezo kuwa bado anakamilisha nyaraka za utetezi.

Katika ya msingi namba 184/2022, Mbatia anaiomba Mahakama itamke kuwa tuhuma alizozitoa Selasini dhidi yake ni za uongo, na hivyo imwamuru amuombe radhi hadharani na kumlipa fidia ya Tsh. Bilioni 3.

Jaji Obadia Bwegoge ameahirisha kesi hadi Januari 17, 2023 kwaajili ya kusikiliza maombi ya Selasini na kuamua kama sababu za kuomba kuongezewa muda ni za msingi.
View attachment 2430834
====================

Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi (Bara), Joseph Selasin ameiomba Mahakama Kuu Masjala Kuu, imuongezea muda ili aweze kuwasilishwa nyaraka za utetezi.

Selasini amefunguliwa kesi mahakamani hapo na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia akimtaka amlipe Sh3 bilioni kwa madai amemdhalilisha.

Maombi hayo madogo namba 541/22 yamewasilishwa mahakamani hapo leo Jumanne Novemba 29, 2022 na Wakili wa utetezi, Hassan Mkwanya mbele ya Jaji Obadia Bwegoge.

Wakili Mkwanya amedai Novemba 23, 2022 alipokea maelekezo ya kumwakilisha Selasini ambapo ilikuwa ni nje ya muda unaotakiwa kuwasilisha utetezi kisheria.

"Nilipoangalia nilikuta siku 21 za kuwasilisha utetezi kisheria zimepita, tukaona tuwasilishe maombi ya kuongezewa muda kwaajili ya kuleta utetezi," alidai Wakili Makwanya.

Wakili wa Mbatia, Hurdson Mchau alidai siku 21 zimeisha tangu Novemba 18 na Wakili wa utetezi alipata taarifa hiyo Novemba 23, hata nakala ya maombi hawajaiona na kuiomba mahakama kupanga tarehe ya karibu ili kuona maombi hayo yana sababu za msingi.

Hata hivyo, Jaji Bwegoge ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 17, 2023 kwaajili ya kusikiliza maombi ya Selasini kama sababu za kuomba kuongezewa muda ni za msingi au la.

Katika kesi hiyo ya msingi namba 184/2022, Mbatia anaiomba mahakama itamke kuwa tuhuma alizozitoa Selasini dhidi yake ni za uwongo, imwamuru amuombe radhi hadharani na kisha amlipe fidia ya Sh3 bilioni.

MWANANCHI
Kuna mtu amekenua hapo hadi kero
 
Hii kesi itaamuliwa migombani mahakamani n sehemu ya kushikishana adabu yaan ukijidai mjanja tunamaliza Ila watakutana December hii watakaa migombani itachinjwa mbuzi na Mambo yataisha
 
Back
Top Bottom