Joseph Mungai, Frank Mwakalebela wahojiwa na TAKUKURU kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joseph Mungai, Frank Mwakalebela wahojiwa na TAKUKURU kwa rushwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pdidy, Jul 30, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,589
  Likes Received: 5,773
  Trophy Points: 280
  Kwa walioangalia TBC1 taarifa ya habari inaonekana TAKUKURU wameamua kudili na CCM....

  Huko iringa mwandishi wa TBC1 anasema Mh Mungai na Bw Frank Mwakalebela wamehojiwa baada ya kukutwa wakigawa cash live hadharani..habari zaidi zinasema kwa upande wa Mwakalebela alikuwa kwenye moja ya guest house ndipo walipowafata lakini bahati mbaya wapambe waliokuwa na hela waliruka ukuta na kuingia mitini.....na kubakia na baadhi ya wengine.

  Hakika inawezekana hawa jamaa tunawasifia lakini kwa mtindo huu waanaonekana wanafanya hivi ama kwa kujulikana wako kazini nikimaanisha inawezekana hakuna hata kesi moja watakayoshinda kwa style hii... Kama mmemsoma Mama Sitta amesema hakuna aliyemkuta anagawa hela. Kumkuta mtu na hela na bahasha sio dili akikawambia alikuwa anapanga kutoa kadi za mwaliko utasemaje?

  Hawa watu wawe makini wasijilazimishe kuwa "PWEZA" wakati hata harufu yake hawaijui wataishia kuonekana wapuuzi mbele ya watanzania, tusubiri
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Walimkosakosa Hosea sasa kaamua kuwaumbua, kazi wanayo!
   
 3. K

  Keil JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wala sijaona kama anawaumbua, sana sana Hoseah mwenyewe na watu wake ndio ambao wanaonyesha kwamba hawajui kazi ama wanafanya kazi kwa kukurupuka. Kati ya wagombea wote walioshikwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye atafikishwa mahakamani maana hawana ushahidi wa kuwafikisha mahakamani.

  Unakumbuka kesi ya Elisa Mollel na Lekule Laizer kwenye uchaguzi wa CCM mwaka 2007? Kesi iliishia kufutwa tu na ndio ukawa mwisho wa mchezo. Hapa naona TAKUKURU wako kwenye maigizo ili kuwazuga watanzania.
   
 4. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee unamzungumzia Frederick Mwakalebera yule boss wa zamani wa TFF au mwingine?? je unaamini chanzo chako kweli???
   
 5. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  typical of Mitanzania ni mila rushwa kusipo jitambua hapa sijui unafundisha kazi au? acheni malalamiko tuwaache TAKURURU wafanye kazi zao! au rushwa imakuwa mila na desturi zetu?
   
 6. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Tatizo wote walio kamatwa wamekutwa wanataka kutoa rushwa na sio kwamba wametoa rushwa.kwanini takukuru wasi subiri mpaka wahusika watoe rushwa ndio wawakamate hili wawe na kesi nzuri zaidi?
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kutaka ni tofauti na kujaribu ....hapa patamu!
  Kuna kosa la "kutaka"? ... yaani mens rea? Actus reus NI MUHIMU.....HATA KATIKA KUJARIBU LAZIMA WANGESUBIRI HADI TRANSACTION IANZE HATA KAMA HAIJAKAMILIKA...
  Pia inaonekana hawa wazito wanajiamini sana kama vile wako juu ya sheria! Loh!
   
 8. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,439
  Trophy Points: 280
  Macho tunayo tunaona, masikio tunayo tunasikia, tuchukue uamuzi kuwa chama hiki hakitufai
   
 9. m

  mrs kiwonyi New Member

  #9
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nafikiri takukuru wabadilishi jinsi ya kushughulikia ttizo la takrima katika uchaguzi.
  wote waliokamatwa kwa kweli hatujaona matokeo hasi ya kukamatwa kwao. hivyo nafikiri ili tuuone ueledi wao inapaswa kutoa mambo yenye matunda.
  pia nadhani navyo vyama katika ngazi zote watoe ushirikiano kwa takukuru, kwasababu hito ndio dawa ya kuwaondoa viongozi wasio waadilifu katika taifa.
  wote ni mashahidi uchaguzi wa UWT wote walioshinda asilimia kubwa ni wale waliokamatwa na takukuru, je hiyo ni ishara gani? ni swali kwa wana jamii wote
   
 10. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Moja huyu Mungai kwa kweli sasa awaachie 'wanyalukolo' wengine bado tu kuchoka.

  Pili we member inabidi uache kutumia majina kamili ya watu kama sio wewe mwenyewe SAMSONMFALILA hilo ni jina lako wewe au fujo tu. Utakuja kuwaletea watu matatizo wakija likizo zao huko bure kwa mambo ya kipuuzi.
   
 11. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Kesi ya ELISA MOLLEL na LEKULE LAIZER iliingiliwa na Mzee wa manywele (EL) lakini alikuwa amechelewa kwani alitaka hata press conference isifanyike lakini RBC wa Arusha aliitoa kabla ya Hosea hajatoa amri kwani manywele aliwasiliana naye!!! Kilichofuata baada ya hapo ni kuwanyonga TAKUKURU kwa kupitia DPP . Faili lilipofika kwake hakulirudisha na baadaye akasema hakuna kesi. Kwa kuwa PCCB ni tawi la CCM kama vilivyo vyombo vingine vya dola, basi DBC wa Arumeru na aliambulia uhamisho kwenda Tandahimba na RBC wake akapelekwa Manyara. Kazi kwisha hapo.....na hii imejirudia kwa RBC kilimanjaro na wengine watafuata........
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,589
  Likes Received: 5,773
  Trophy Points: 280
  mkuu naamini taarifa ya habari sasa kuamini chanzo ni wewe kuikubali tbc ama lah
   
 13. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2010
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Kwa Mungai hiyo ni njia ya pili. Kwanza alijaribu 'kumnunua' mpinzani wake wa karibu kwa kum-ahidi 'kumrudishia' gharama zake zote za uchaguzi na faida kidogo kama akijitoa kabla ya siku ya kura. Kwa ufupi nafahamu kuwa jamaa alimwambia atafikiria, lakini kwa wapambe wake amesema kuwa hatafanya hivyo, na anaendelea na uchaguzi. Naona Mungai kaona dalili kuwa jamaa hana mpango wa kujitoa na bado anamtoa jasho.

  Mungai amekuwa anamwaga fedha kama mchezo kwa kutumia hotel na mgahawa wake unaosimamiwa na dada yake na mtoto wa dada yake. Wajumbe wanaoenda pale kula au kulala badala ya wao kulipia, wao ndiyo wanalipwa kwa kula au kulala pale. Maajabu. Pia anamtumia mdogo wake anaitwa Kisauti, ambaye anajitutumua kuliko Mungai mwenyewe. Nadhani mwaka huu mambo ni magumu, japo anaweza kupita kwa al manusura sana.
   
 14. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kuna msemo "naming and shaming", sio lazima mtu afungwe lakini ile kumtaja kwenye vyombo vya habari kwa jambo ambalo sio jema basi linatosha kuwasababishia wengine kushindwa kufanya kitu kama kile.

  Mfano vile alivyosemwa DC wa Kigoma au Waziri Sitta ni mambo ya kutia aibu kwa vyeo vyao walivyo navyo.

  Ila hao wagombea wengine hawaamini kama wanaweza kukamatwa au wanajiamini sana?
   
 15. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  bitimkongwe
  aibu ni nini? wanasiasa wa kiafrika wana aibu? kumbuka ya Kibaki wa kenya, Mugabe wa Zimbabwe, Lowassa na Rostam wa Tanzania... na hata Kikwete mwenyewe... aliingiaje madarakani? Mishipa yao ya aibu ilishakatika wakati wa michezo ya utotoni...
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,589
  Likes Received: 5,773
  Trophy Points: 280
  lowasaa kasema juzi
  hotojutia richmond yeye aliamuru umeme uje hayo mengine ayamuhusu
  huyu ndie waziri tena ale mkuu kikwete una kazi ngoja tusubiri magubeli ya 2011 kazi kwako
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,589
  Likes Received: 5,773
  Trophy Points: 280
  Juma contena
  nahisi utoto ukikua utaacha hivi babako anaitwa mfalila unahisi mko wenyewe kwenye ukoo
  pole ama ulitaka kutuoyesha ni hodari wa mabox tukupokee kwa shangwe wakati wa likizo
  anyway tusubiri uchaguzi ndio niongee
   
 18. M

  Mutu JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ahaaaaaaaaaaaaaaaah
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,589
  Likes Received: 5,773
  Trophy Points: 280
  awa watroto wanaopelekwa nje kwa summer camp wanamatatizo kweli..wenzako tunakuja uko likizo tunarudi kwetu kijana sikulalamikii kubakia uko maana najua umesema swala la kurudi likizo kwa sam natumaini wewe ukirudi umefika else sam akutie kwenye hold 4
   
Loading...