Joseph Mbiliyi (Sugu) awaumbua CHADEMA, akiri walichelewa Uwanjani kumuaga Mzee Mkapa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,313
2,000
1.PNG

Leo, ilikuwa ni siku ya kuuaga Kitaifa mwili wa Rais wa Awamu ya 3, Benjamin Mkapa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar na viongozi mbalimbali walikuwa wakienda kutoa salamu zao za mwisho

Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe walienda uwanjani hapo na baadaye kudai kuwa walizuiwa kuingia Uwanjani kwa ajili ya kuuaga mwili wa Mkapa

Katika Ufafanuzi wao CHADEMA huku wakiitaka Serikali itoe ufafanuzi kwa kuzuiwa kwao wamedai wao wamefuata ratiba waliyopelekewa ikionesha tarehe, muda, siku tukio na muhusika

Hata hivyo, Jana Msemaji wa Serikali aliweka bayana ratiba ya kufika uwanjani hapo ambapo Serikali iliwataka Viongozi wote wa Kitaifa na Viongozi wa Kisiasa kufika katika Uwanja wa Karimjee na kuacha magari yao hapo kukiwa na gari maalum la kuwapeleka uwanjani ambapo la mwisho liliondoka saa 1:30 asubuhi
 

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
5,283
2,000
Itifaki ipo na Duniani Kote kuna Utaratibu..sijui Kwann chadema kila mara wanajiwekea kitanzi wenyewe.

Mkuu Wa nchi ameshaingia kwa usalama sio sawa nyie chadema kuingia baada ya Rais..Sio Heshima na pia sio sawa...

Lawama kila mara ila mmechemka sana
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,288
2,000
Hapo hakuna cha kitanzi wala nini, nyinyi mbona alipo pigwa risasi mh Lissu hamkwenda kumjulia hali pale Nairobi?

Kumbe mkuki ni kwa nguruwe siyo? Mkianza wenzenu wanamaliza! Wacheni kulia lia
Itifaki ipo na Duniani Kote kuna Utaratibu..sijui Kwann chadema kila mara wanajiwekea kitanzi wenyewe
.Mkuu Wa nchi ameshaingia kwa usalama sio sawa nyie chadema kuingia baada ya Rais..Sio Heshima na pia sio sawa...

Lawama kila mara ila mmechemka sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom