Joseph Mbilinyi (Sugu) amtaka Rais Magufuli asafiri Nje ya Nchi ajifunze kwa wenzake

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,903
2,884
Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia CHADEMA Joseph Mbilinyi amemshangaa mh Rais John Magufuli kwa kitendo chake cha kutokusafiri nje ya nchi, akichangia bungeni mbunge huyo alisema haiwezekani Rais abaki amejifungia Dar badala yake anapaswa kusafiri nje ya nchi ili kwenda kujifunza kwa marais wenzie.

Maoni
Je, hii ni mwendelezo wa viongozi wa CHADEMA kubadili gia angani!?
 
mbunge wa mbeya mjini kupitia chadema mh joseph mbilinyi amemshangaa mh rais john magufuli kwa kitendo chake cha kutokusafiri nje ya nchi akichangia bungeni mbunge huyo alisema haiwezekani rais abaki amejifungia dar badala yake anapaswa kusafiri nje ya nchi ili kwenda kujifunza kwa marais wenzie. je hii ni mwendelezo wa viongozi wa chadema kubadili gia angani!?

Mmmmh, hatari sana hii, kwani rais hajawah kwenda nje ya nchi?
 
Wakisafiri makelele wasipo safiri makelele binadamu anataka nini haswa?

Sisi sio kisiwa....Ukishirikiana na wenzio ndipo nao watashirikiana nawe...Wewe baba hupendi kwenda kwa mwenzio na unapiga marufuku unategemea nani atakuja kwako....
 
Ukweli Chadema wanatuchanganya, wao ndio waliotupa mchanganuo wa safari za Rais, wametuonesha jinsi gani zinavyokuwa mzigo kwa taifa!, Rais Magufuli ameelewa somo, anajaribu kupunguza gharama za safari kwa kutumia wasaidizi wake. Sugu anakuja na hoja kwann Rais hataki kusafiri nje ya nchi. Nashauri Mh. James Mbatia na Joseph Mbilinyi wafanyiwe mdahalo kuhusu safari rais kama kuna umuhimu kusafiri au laa!
 
Rais aliyetoka alisafiri na kumekuwa na kelele upande wa ukawa, naona ndo point ya uliyemnukuu.

Alipigiwa kelele kwasababu hakufanya kwa kipimo....lakini sio ndio kukataa kabisa kusafiri...Ushirikiano na Viongozi wenzako ndipo utapata mawazo mbali mbali
 
Kamilisha habari ili ueleweke .kamilisha ujmbe kamili uliokuwa kwenye hoja take, mmeondoa binge live ili tuishi kwamajungu na uzushi .
 
maswali ya msingi ya kujiuliza ni haya:-
a) kwa kutokwenda kujifunza huko nchi inapata faida gani?
b) kwa kutokwenda kujifunza huko nchi inapata hasara gani?
c) akienda twapaata hasara gani?
d) je ipo njia mbadala ya yeye kujifunza mbali na kusafiri?
e) njia hizo zinachangamoto zipi?
f) zinafaida gani?
 
Tatizo ni kuwa Kikwete aliamia NJE kabisa. Kwa miaka 10, miaka 5 alikuwa nje ya Tanzania.

Inaweza kuwa kama USA yaani kwa mwaka Rais ana idadi ya safari za nje na hawezi kuzidisha. Ila pia ni LAZIMA asafiri.

Bush Jr alikuwa na safari 48 tu nje ya USA kwa miaka 8. Hizo zote Kikwete alimaliza kwa nusu mwaka mmoja tu.

Wakisafiri makelele wasipo safiri makelele binadamu anataka nini haswa?
 
maswali ya msingi ya kujiuliza ni haya:-
a) kwa kutokwenda kujifunza huko nchi inapata faida gani?
b) kwa kutokwenda kujifunza huko nchi inapata hasara gani?
c) akienda twapaata hasara gani?
d) je ipo njia mbadala ya yeye kujifunza mbali na kusafiri?
e) njia hizo zinachangamoto zipi?
f) zinafaida gani?

Acha ya rais hata wewe raia wa kawaida usipo jichanganya na wengine kuna hasara yake kama unafanya biashara ya kusaka pesa....SOMA ADVANTAGES ZA INTERNATIONAL TRADE TUU JAPO KWA UCHACHE ZITAKUSAIDIA.
 
Ukweli Chadema wanatuchanganya, wao ndio waliotupa mchanganuo wa safari za Rais, wametuonesha jinsi gani zinavyokuwa mzigo kwa taifa!, Rais Magufuli ameelewa somo, anajaribu kupunguza gharama za safari kwa kutumia wasaidizi wake. Sugu anakuja na hoja kwann Rais hataki kusafiri nje ya nchi. Nashauri Mh. James Mbatia na Joseph Mbilinyi wafanyiwe mdahalo kuhusu safari rais kama kuna umuhimu kusafiri au laa!

CHADEMA wamezoea maisha ya 'uchapati' wanageuka geuka kila kukicha. Wamesahau walivyojigamba kuwa Magufuli anatekeleza sera zao? sasa leo Sugu anaongea nini? Ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu nzuri.
 
Back
Top Bottom