Joseph Mbilinyi (Sugu), adaiwa kuonyesha ishara ya kidole cha kati kwa Wabunge wenzie

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
13407009_1531680686846344_4210700433527095187_n.png

Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu', amejikuta matatizoni baada ya kudaiwa kuwaonyesha wabunge wenzake ishara ya kidole cha kati ambacho hutafsiriwa kuwa ni tusi.

Mheshimiwa Sugu ametiwa matatani baada ya kuonyesha kidole hicho wakati akitoka bungeni, ambapo mbunge wa CCM Jacline Ngonyani aliomba Mwongozo.

Naibu spika alikili kutoliona , ila ameomba clip ya video ili kuangalia upya . na kama itabainika ilo ni alama ya tusi.
 
non verbal communication, lakini kila watu na utamaduni wao; kwa mfano sisi hapa Tanzania alama ya kumwambia mtu bye unampungia mkono nchi zingine alama hiyo hiyo unamwambia njoo pia sisi hapa TZ mtu akichokonoa pua sio tusi lakini kuna sehemu zingine mtu akichonoa pua watu wanatapika, mfano mwingine sisi hapa TZ mtu akijamba hadharani anaonekana "amepinda" kwingine unapongezwa na mifano mingine mingi tu. Sasa nirudi kwenye mada ni kweli kwamba hapa TZ hiyo alama ni matusi?!
 
We jamaa bwana! akili unazo ila unazitumia vbaya. kama umejua yote hayo bas unajua kuhusu Universal Symbols si et?
 
Si a sa kweli kweli, badala ya kujadili mambo ya msingi wanaanza kufuatilia vidole vimekaaje wakati wa kuongea ndani ya bunge 'ili mradi mtu awajibishwe!!.

But mwisho wa siku wana_CCM wabunge mjue mnawa_boost wenzenu na wanaonekana mashujaa hata kama wamefanya madudu. Shauli zenu
 
non verbal communication, lakini kila watu na utamaduni wao; kwa mfano sisi hapa Tanzania alama ya kumwambia mtu bye unampungia mkono nchi zingine alama hiyo hiyo unamwambia njoo pia sisi hapa TZ mtu akichokonoa pua sio tusi lakini kuna sehemu zingine mtu akichonoa pua watu wanatapika, mfano mwingine sisi hapa TZ mtu akijamba hadharani anaonekana "amepinda" kwingine unapongezwa na mifano mingine mingi tu. Sasa nirudi kwenye mada ni kweli kwamba hapa TZ hiyo alama ni matusi?!
Hapa mleta mada hujaweka vizuri ni kidole kipi kimetumika,maana kuna dole gumba ukiliweka katika mikao kama mitatu hivi linatoa ishara 3 tofauti,kuna kidole kidogo cha mwisho na kidole cha kati vyote vina namna ambayo inatoa ishara tofauti tofauti ikiwemo ya kutukana,ningeshauri ungeweka picha au mchoro ili tujadili vizuri.
 
Mheshimiwa Sugu ametiwa matatani baada ya kuonyesha kidole cha **** wakati akitoka bungeni, ambacho kimetafsiliwa ni tusi; ambapo mbunge wa ccm Jacline Ngonyani aliomba Mwongozo.

Naibu spika alikili kutoliona , ila ameomba clip ya video ili kuangalia upya . na kama itabainika ilo ni alama ya tusi
Jackline nani kakwambia kuwa hilo ni tusi? Amemuonyeshea nani? Nadhani huyu ni viti maalum! Hiyo kesi ataishinda tu!
 
Hivi maana ya kidole cha kati ni nini haswa? na hiyo maana imetafsiriwa wapi kisheria? (Kiuswahili sisi mwanaume ukimuoneshea mwanamke sio tusi unakua umesema ukweli kwa ishara kwamba anafanywa hicho kitendo)
 
mzee wa freedom kawapa dole la kati? Nadhani ni tuhuma tu haina uhakika ngoja tusubiri video clip tujue ukweli huenda alionyesha alama fulani kwa lugha ya viziwi sema wameshindwa tambua
 
Haya ndio alikuwa anasema Lema jana, maadili hakuna kuanzia ngazi ya famiia hadi kwenye jamii. Sasa kama mheshimiwa mbunge anaonyesha kidole cha kati ndani ya bunge unategemea kuwa na wananchi wa aina gani.
 
Back
Top Bottom