Joseph Kusaga ateuliwa Mwenyekiti Kamati ya Kuongoza kamati ya Kupendekeza vazi la Taifa

ANASTAHILI, clouds walianza zamani sana kusapoti vazi la taifa

pamoja na upupu wa kisiasa wa clouds, jamaa pia wanastahili nishani ya kujitolea hasa kwenye maafa ... si mafuriko, mabomu nk

nimemnyonga mnyonge na haki yake nimempa


Kiswahili bana!
Ukimnyonga si atakufa,kwa hiyo hiyo haki ataipatia ahera?
 
Concept nzima kwamba vazi la taifa litapatikana kwa kamati linachekesha. Cultural totalitalianism.
 
ANASTAHILI, clouds walianza zamani sana kusapoti vazi la taifa

pamoja na upupu wa kisiasa wa clouds, jamaa pia wanastahili nishani ya kujitolea hasa kwenye maafa ... si mafuriko, mabomu nk

nimemnyonga mnyonge na haki yake nimempa

Clouds ni redio ya CCM wewe. unafikiri magamba hawanaakili kukubali redio uhuru ife hivihivi?
 
joseph sio kila kazi za kuteuliwa zinakubaliwa uunaryuhusiwa kuktaa
mwisho tutashindwa kukutofautisha kati ya HASHIM LUNDENGA NA KASHFA ZAKE NA CLOUDS NA JOSEPH KUSAGA
WATCHOUT BR
 
Hilo vazi la taifa litakuwa la size gani; XL, XXL, L au M? Halafu nani atakuwa analivaa, rais? Mbona mnanichanganya?
 
Tumethubutu usanii tumeuweza na sasa tunasonga mbele na usanii wetu....Zidumu fikra za wasanii wa magamba!!! Zidumu!!!!!
 
Ufisadi mwingine at work. Watakuja na vazi la ajabu ajabu tu hawa kwa sababu ufisadi umeshawaathiri.

Masauni

Nashukuru umeliona hili, lakini ufisadi wenyewe hauko kwenye suala la kubuni vazi la ajabu ajabu.

Tangu lini mtu ambaye alikuwa DJ ambaye shughuli zake zote maisha yake yote ni MUZIKI akapewa kazi ya kuongoza kamati ya kubuni VAZI la Taifa? Badala ya uongozi kupewa mtu ambaye amebobea kwenye fani, kama vile akina Merinyo na Ailinda Sawe (Afrika Sana) au hata Asia Idarous, na wengineo kama Vida Mahimbo, ambao wote ni wabunifu, waongoze kamati, wafanye utafiti wao, anapewa DJ aliyebobea kwa sababu tu anaweza KUINUNUA nafasi hiyo?

Joe anajua kwamba "gia" ya muziki siku hizi haina mashiko, ndio maana anajaribu kujiingiza kwenye mambo ya kitamaduni zaidi, ili aonekane naye MDAU!

Ngojeni, wadau husika watawasusia! ITADODA!
 
Hongera zake.

Naamini WanaJF wana nafasi kubwa kushiriki kwa njia moja au nyingine katika zoezi hili kuhakikisha kuwa vazi linalochaguliwa litakuwa "limeenda shule."
 
Kwa mtazamo wangu vazi la Taifa huwa linatokea tu,baada ya majaribio mengi yasiyo rasmi uku mtaani..yani ni kama vile sasa tupo kwenye mahabara tunachanganya kemikali mwisho wa siku tunalipata kutoka kwa watu sio kamati...mfano mzuri Nigeria.

Kuteua watu wachache tena wasiobobea kwenye hiyo tasnia ni kupeana ulaji tu kama wa studio na majengo ya wasanii vya JK.

Kwaio wakishalipata ndio kinafuata nini?
 
Joe anafaa sababu ni successful entrepreneur, wengine ni wataalam ktk fani kuanzisha biashara na kusimama hii ni watu wachache sana.
Wangapi wanaweza vumilia michano mnayotoa wakati hata viduka hamna ila mnatomboka tu.
 
Kwa mtazamo wangu vazi la Taifa huwa linatokea tu,baada ya majaribio mengi yasiyo rasmi uku mtaani..yani ni kama vile sasa tupo kwenye mahabara tunachanganya kemikali mwisho wa siku tunalipata kutoka kwa watu sio kamati...mfano mzuri Nigeria.

Kuteua watu wachache tena wasiobobea kwenye hiyo tasnia ni kupeana ulaji tu kama wa studio na majengo ya wasanii vya JK.

Kwaio wakishalipata ndio kinafuata nini?

Thank you.

My sentiments exactly. Hayo mambo ya utamaduni wa kuwa engineered na kamati za kiserikali yatatuletea propaganda tu, matokeo yake mnaweza kuambiwa vazi la taifa liwe la kijani, tena lina alama ya jembe na nyundo.

Totalitalian bs and propaganda.
 
Tumbiri ndugu yangu hamna kitu kama hicho, tuwe na vitu vya msingi vya kusubiri kuliko kitu kama hicho eti vazi la taifa!
Hebu jipe tafakari utekelezaji wake utakuwaje??
Katika namna kiswahili tu kinaelekea kutushinda katika kuwa na msimamo wa kukisimami kama kweli "Lugha ya Taifa"
Ah hebu turudini kwenye mjadala wa KATIBA hawa mapoyoyo wasituyumbishe kwa mambo ya kijingajinga ha


jG umeongea ukweli TANZANIA tuna challenges nyingi zaidi ya hilo vazi la taifa, alafu me sioni mantinki ya vazi la taifa zaidi ni moja ya njia ya kutengeneza ufisadi tuu. Shule hazina facilities za kutosha, hospital wagonjwa wanalala chini na hakuna dawa sasa hilo vazi la taifa mimi mtu wa kijijini litanisaidiaje? viongozi wetu ni wavivu wa kufikiri na hilo ndolinalotutesa sana hapo wanamtengenezea mamilioni Kusaga ya kifisadi.
 
Msishangae uteuzi huu. Aliyeufanya yaani Nchimba naye hovyo kama Clouds. Shame on you!
 
Kwanini hawataki kuchukua kile kimao alichokuwa anavaa mwalimu[ kisichokuwa na COLLAR] kiwe ndio vazi la taifa kwa wanaume? Wanawake wavae vitenge na vilemba!! Tukifanya hivyo tutapunguza gharama na njia ya wakina Nchimbi kufisadi hela zetu!
 
Kwanini hawataki kuchukua kile kimao alichokuwa anavaa mwalimu[ kisichokuwa na COLLAR] kiwe ndio vazi la taifa kwa wanaume? Wanawake wavae vitenge na vilemba!! Tukifanya hivyo tutapunguza gharama na njia ya wakina Nchimbi kufisadi hela zetu!

Ushasema Ki-Mao, vazi la taifa la Watanzania ku copy kutoka Mao ni ukoloni mamboleo wa kiutamaduni.

Vazi la taifa la Watanzania litatokana na wananchi wa Tanzania, na wananchi pia wanaweza kuamua kwamba kuwa na vazi la taifa si muhimu vilevile.

Huwezi kuwa na vazi la taifa kabla ya kuwa na an indigeneous textile industry.

Serikali iache kukazania kuunda kamati za ku design vazi la taifa na iangalie kuweka mazingira mazuri ya kuendeleza a local textile industry, utaona watu wenyewe wanakuja na style zao organically na zinazopendwa sana automatically zitakuwa vazi la taifa bila kamati.

Kwani kuna kamati gani ilikaa na kusema khanga/ vitenge ni vazi zuri?
 
Hii kamati ni ya kujitolea ama inagharirmiwa na serikali? Hebu wekeni wazi

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Vazi la taifa! So what? Waziri anakaa anaamua kuunda kamati ya kutafuta upuuzi! Tumekosa ya kufanya? Tusimjadili Kusaga bali umuhimu wa hilo vazi! Subiri msikie mabilioni yatakayotumika while Sewahaji panatisha!
 
Back
Top Bottom