Joseph Justine Mkurugenzi wa CasfetaTayomi Amefariki

ThinkPad

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,844
230
WanaJF nimepokea taarifa hizi za msiba wa ndugu yetu na mtumishi aliye kuwa na wito kwa vijana Mchungaji joseph Justine.
Mchngaji Justin amefariki tarehe moja mwezi watisa na msiba huu umegusa watu wengi sana hakuna Mwana Casfeta yeyote ambaye hakufahamu mchango wa Mchungaji Justin katika hudama za wanafunzi na wanavyuoni katika kuendeleza michakato ya maadili nakukulia katika wokovu ukiwa kijana.

Safari kaimaliza kavipiga vita vilivyo imara na atimae bwana kamwita,bwana ametwaa na bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe.
Mungu ailaze maalapema mbinguni amina.
 
Asante kwa taarifa. Namkumbuka huyu ndugu, alikuwa mwalimu wa Wanafunzi waliookoka na wakati huo hakuwa Mchungaji wakati niko Azani Sec miaka ya mwishoni ya 80 na mwanzoni mwa 1990.

BWANA alitoa BWANA ametwaa, Jina lake lihimidie; Heri Wafu wafao katika BWANA, naam wapate kupumzika. Vita amevipiga, mwendo ameumaliza.
 
RIP Pastor Justine, poleni CASFETA na jumuiya ya wanafunzi kwa kuondokewa na mwalimu mzuri wa mambo ya kiroho.
 
Asante kwa taarifa. Namkumbuka huyu ndugu, alikuwa mwalimu wa Wanafunzi waliookoka na wakati huo hakuwa Mchungaji wakati niko Azani Sec miaka ya mwishoni ya 80 na mwanzoni mwa 1990.

BWANA alitoa BWANA ametwaa, Jina lake lihimidie; Heri Wafu wafao katika BWANA, naam wapate kupumzika. Vita amevipiga, mwendo ameumaliza.


Nikweli, amefariki akiwa mchungaji baada yakuwa mwalim wawanafunzi kwakitambo huduma yake ilikuwa kubwa na kuongezeka,ndio akawa na cheo cha uchungaji mpaka alipo fikwa na mauti.
 
Hatuna shaka kwa mema aliyoyafanya kwa kuchunga Kondoo wa Bwana basi alijitayarishia kiwanja huko 'heaven' hatuna wasi wasi, lakini mwamuzi ni God mwenyewe.
Tuko pamoja na wote waliogushwa na msiba huo. Amen
 
Amen. simfahamu huyu mtumishi wa Mungu, lakini tutakutana kwenye mji wa utukufu.
Liimidiwe jina la Mungu mkuu.
 
"Heri wafu wafao katika Bwana Mungu tangu sasa,wapate kupumzika baada ya taabu zao kwa kuwa matendo yao yafuatana nao".
Poleni,ndugu,marafiki,maaskofu,mitume,manabii na familia ya Mchunga kondoo wa Mungu, kwa kuwa Mwenyezi amemuita mtumishi wake Justine ktk ulimwengu ule usioonekana kwa macho.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom