Jose Mourinho Wa FC Porto yupo wapi??

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Tukizungumzia jina La Jose Mourinho katika ulimwengu wa Soka Linaheshima yake ila kama vile kwa Sasa Limeanza kushuka Thamani.

Mourinho wa Fc Porto Ya msimu wa 2003-2004 ni Tofauti kabisa na huyu wa Sasa wa Manchester United,Mourinho wa Fc Porto alikua ni Mourinho Mpambanaji ndani ya dk 90 zote.

Akiwa wa Vijana wakali kama vile Kijana kutoka nchi Ya Mandela BENNY MCCARTHY,na wengineo akina Deco,Ricardo Calvaro,Maniche...nk Alibeba Kombe la Ulaya(UEFA) msimu wa 2003-2004 kwa fainali kumfunga Monaco jumla ya goli 3-0

Katika fainali hizo Mourinho alifanikiwa kuwafunga miamba wa Soka wa ulimwengu Manchester united katika hatua ya 16 bora na timu nyingine nyingi kama vile olymp lyon,deportivo la coruna...nk.

Mourinho wa Fc port alikua mpambanaji haswa asiyekata tamaa mwenye uchu wa kushinda kila mchezo,

Ila huyu Mourinho wa sasa Akizungukwa na Vijana aina ya Akina Fellaini,Pogba,Herrera,De gea,Baily,Rojo,Carrick,Rooney...nk amekua tofauti ile hali ya upambanaji imepungua sana akitishiwa hata na timu ndogo,

Mourinho wa Leo anamiliki mpira bila Magoli ila Mourinho wa Porto alikua hana umiliki wa Mpira ila alikua na Magoli ya kutosha na roho ya upambanaji hadi mwisho.

JE Mourinho wa Sasa Amekubali Mazingira kumbadilisha na kuanza kumiliki zaidi badala ya kufunga na kupoteza hali ya Upambanaji? Au Mbinu za Kimpira zimebadilika?
 
We jamaa,kutengeneza kikosi ni kazi kubwa,nacho mpendea Mourinho ni kwamba hapendi dharau,atatengeneza kikosi ambacho hakijawah kutokea united,something like a machine,we xubir dilisha la usajiri lijalo,He s a special one 4 a reason
 
Pogba ndio anasuka kikosi hapo??

Unanunua gunia la mavi kwa £ za kutosha ukidaganywa ni Gold
 
Bado tena yule mourinho wa Inter Milan hajaonekana kabisa akizungukwa na Vijana wapambanaji,Cambiaso,Chivu,Etoo,Lucio,Zlatan...nk
 
I am sure atakuwa anasingizia "mizigo" ya Mzee wa Philosophy (Van Gaal) na Moyes. Ngoja tuone msimu ujao akishanunua players wengine watatu. Ila asifanye makosa yaleyale ya kutupa fedha nyingi kwa watu kama Pogba
 
Pogba ndio anasuka kikosi hapo??

Unanunua gunia la mavi kwa £ za kutosha ukidaganywa ni Gold
Hahahaa unataka pogba afanyaje sasa? Afunge goli 20 ndo utamkubali? Huo sio wajibu wake uwanjani, majukumu makuu ya kiungo uwanjani,ni kuchezesha timu,ku defence, ku creat chances za magoli,ku assist,sasa tafuta takwimu united iko nyuma ya Liverpool tuu kwa ku create chances za magoli,hiyo inamaanisha tatizo ni strikers,ndo maana mourinho anakuambia Chicharito angekuepo united msimu huu angefikisha goals 20+ kwa chances ambazo united wame create hata kama angekua anatokea bench kucheza dk 10 au 20 za mwisho
 
Yes hata mi natamani kijana chicharito arudi OT. Van gal sin hamu nae aliuza dimaria akauza v.persie akauza chicharito na wengine kibao bila ujinga wa mwandishi wa story Van gal naamini man u ingekuwa pale juuu.
But ngoja usajili wa msimu wa joto uanze ndipo tutajua moto wa man u
 
Van gaal alikua na mpango wa kutushusha daraja,napenda sana kupiga story na Wazungu tunapokutana hasa za kisoka kama anapenda mpira,nikamgusia kuhusu Kocha X ambaye sasa yupo ligi kuu England baada ya kutoka Timu X akaniambia mpango wa yule kocha ilikua na kuiharibu kabisa Timu x kama vile alikua ametumwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom