Naomba msaada kwa developers wanaofanya kazi na Joomla. Kwa sasa kuna kazi naifanyia majaribio kwenye localhost(xampp) natumia joomla 1.5, Je, kuna madhara yoyote kwenye frontend template kama nta upgrade kutoka joomla 1.5 kwenda joomla 1.7?
Mabadiriko front end hakuna ila unatakiwa kuzingatia mambo je Components, Plugins, modules na Templates zipo compatible na joomla 1.7? Unaweza anza kujiuliza sasa tupo joomla 2.5.1 je kuna extension ambayo bado ipo 1.5? Naweza sema ndio. Kwa mfano component kubwa kabisa kwa ajili ya Comment kwenye joomla(jcomment) bado hawana inayokidhi 2.5, Joomfish vilevile..
Hivyo basi, kama kila kitu kipo compatible, usiwe na wasi hakuna kitakachotokea.
Ila kumbuka BACKUP BACKUP BACKUP, chochote kinaweza tokea kipindi unaupgrade, kama upgrade isiyokamilika, databe error nk, Akeeba Backup ipo kwa ajili yako. Kwa msaada wa kiufundi zaidi unaweza wasiliana na Dudumizi Solutions
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.