Jombi, Jambazi aliyetisha wa Kimataifa aliyeishi Tanzania

Kipindi kirefu tumekuwa tukijifunza na kusoma habari za Majambaz toka Mataifa ya nje. Nikakumbuka hapo nyuma nchini mwetu alikuwepo jambaz mbabe wa kimataifa katika jiji la mbeya aliyeitwa jombi.

Miaka ya 80s mimi na wazaz wangu tulikuwa tumeingia tanzania na kutua mkoa wa mbeya tukitokea nchini Zambia. Toka miaka hiyo Mbeya ulikuwa ni mkoa wenye baridi na wenye utamaduni wa kipekee sana. Ulikuwa ni mkoa ambao walipenda watu kuishi KIBABE. kuna mitaa ilikuwa huwez pita bila kusumbuliwa hata na watoto wadogo ikiwa wanakuona umlaini.

Ubabe ulitawala hata club kama utaenda na mrembo ilhali wewe huna ubavu utanyang'anywa na wenye mbavu imara. Ndio kipindi nawaona watemi wa ngumi,karate na kungfu akina shetani,daud n.k. ilikuwa wanafahamika hata wakipita mtaani kwa mienendo ya mikogo ukakamavu na sugu mikononi mwao sabab ya mazoezi.

Alikuweo Jambaz maarufu mkoani humo ambaye alikuwa ni Jambaz wa kimataifa. Zambia walimfaham, South africa na nchini mwake Tanzania. Alifahamika mpaka na Rais. Jina la mwanzo aliitwa Said la kati nmelisahau ila al maarufu alikuwa JOMBI. alikuwa Tajiri na Mbabe hasa.

Alikuwa na matukio mengi moja wapo. Ni lile linalosemekana alienda iba gari south afrika ya aliyekuwa mkuu wa polisi wa kituo flan huko south afrika.kaburu. inasemekana Jombi alikuwa akibishana na wenzie kuhusu utaalamu wake na ubabe wa kuiba. Akawaambia wampe mwezi mmoja awaletee gari ana ya benz toka south afrika kutoka kwa kaburu mmoja kiongozi. Wanasema alisafiri akaenda zambia na baadaye south afrika.

Alikuwa ni mzungumzaji mzuri sana wa kiingereza alifanikiwa kujenga ukaribu na kaburu huyo kwa namna ambayo hakutaka kuwaambia wenzie akiamini wangeweza kwenda kuitumia. Na ndani ya week 3 alirudi akiwa na gari ambayo haielewek aliipataje lakini aliweza onesha kibao cha namba na documents mbalimbal za mmiliki wa gari lile.

Jombi alikuwa na watu wake wazee wa kazi ambao wengi walikuwa walimheshimu na kumwongopa sana. Kuna habari nying zilikuja kusemwa nao baada ya kifo chake. Wanasema alikuwa anaweza mkata mtu na kisu shingo halaf akalamba damu kwenye kisu akifurahia utamu wake au kuchanganya ubongo na damu kisha kunywa.

Mija ya style zake za ujambaz ilikuwa ni kuwajulisha wahusika anakotaka enda kuiba kuwa anakuja siku flan wamwekee pesa. Tukio moja inasemekana aliwah kumwambia tajiri mmoja burushi aliyekuwa na magari ya kusafirisha mzigo kuwa ataenda ijumaa jioni kuchukua pesa kias flan kikubwa sana hivyo amkusanyie asipeleke bank ikiwa anataka kuishi yeye na familia yake.

Yule tajiri aliwataarifu polisi ambao siku ya tukio waliweka ulinzi mkali sana...siku ya tukio polisi wakiwa lindoni alikuja mama mmoja wa kinyakyusa amejifunika nguo.nying kutokana na baridi ila alionekana na i mnene na alivaa viatu chachacha au saa nanr utanikoma.vilikuwa ni viatu maarufu miaka hiyo. Akiwa na kikapu amepeba mahindi na matunda alitembea taratibu akichechemea na kumfuata polisi mmoja kumuuliza kuna nini pale mbona wamezunguka nyumba.polisi alimjibu kuwa kuna jambaz alisema angeenda fanya uhalifu pale hivyo wanalinda nyumba yule mama akaanza kutetemeka na kusema alileta ule mzigo kama vipi basi ye arud polisi aupeleke mzigo ndani. Polisi alikumbuka aliambiwa asitoke lindon hata kwa sekunde.kwa kuona kero pia akamwambia mama ingia peleka.

Yule mama akatembea kuingia ndani...akiwa ndani inasemwa alienda mpaka sebulen na kukuta yule burushi na mkewe wamekaa na watoto wao wametulia.kabla hawajamuuliza we nani alitoa bastola mbili na kuwaoneshea wanyamaze.alimwambia yule.mzee akalete pesa kabla hajaua familia yote.

Yule burushi aliishiwa nguvu akaenda chukua pesa akaleta na jombi inasemekana alimpiga risasi ya pajani kuwa siku nyingine akiambiwa aandae pesa bas aandae pesa na si mapolisi.

Haukusika mlioa maana bastola ilikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti. Basi Jombi akawachukua na kuwaziba midomo kwa matambala na kuwafunga kamba mikononi akaondoka. Akapita kuwaaga askari na kuwatakia ulinzi mwema. Kama mama mzee safari hii akiwa amebeba kikapu ambacho kimefunikwa tu khanga...mlinzi mmoja akamwarakisha aondke kabla jambaz hajafika.mama yule mwenye saut ya kukwaruza akaaga akaondoka zake.ilipofika saa mbili polisi mmoja aliingia ndan baada ya kuona muda umeenda na taa hazijawashwa. Hakukuta watu sebulen aliona alama ya damu akaifuatilia na kukuta inampeleka hadi chumba kimoja huko aliwakuta wamefungwa. ...........

polisi waliwajulisha makao makuu na haraka upepelezi ukaanza. kiuhalisia walikua na uhakika kuwa mhusika ni Jombi lakini walikosa ushahidi.walipoenda kwake walipewa ushahidi na familia nzima kuwa jombi siku hiyo hakutoka nyumban.alikuwa ameamka na kufanya shughuli zake nying hapo nyumban na baadaye kurudi ndani mpaka alipokuja kutembelewa na wageni ambao ni rafiki zake.muda huo wanaosema alienda kufanya huo uhalifu alikuwa sebulen wanapiga story na wenzie.jombi akaachwa huru.

kuna habari nyingi sana kuhusiania jambazi huyu ambaye inasemekana alikuwa na uwezo wa kupotea chumban. kuna tukio linasimuliwa na waliokuwa wafanyakazi wake pale nyumbani kuwa alishawah kuzungukwa nyumban kwake na maaskari wakawa wana ongea naye chumban amejifungia wakimtaka afungue mlango. alipogoma wakasema wanavunja..walipovunja hawakumkuta mtu yeyote ndani. hawaelewi alipotelea wapi na kwa mazingira gani.hakukuwa na malngo mwingine mle ndani na waliserach nyumba nzima pasipo mafanikio.

rais alikuwa akifaham habari za jombi na hata wakuu wengi wa polisi.walikuwa wanshindwa wamkamate kwa makosa gani. alikuwa ameua watu wengi sana kwa namna ambayo ilikuwa ngumu kupata ushahidi na wakati flan watu waliogopa kutoa ushahidi. kuna jamaa mmoja nimemsoma sehemu moja humu ndani anasema yeye alishuhudia kaka yake akiuawa na jombi mbele ya macho yake. anasema kaka yake aliibiwa gari na alijua kuwa aliyeiba ni jombi akaamua kwenda nyumban kwa jombi yeye na mdgo wake akiwepo. ingawa alishaonywa mapema kuwa asiende.wanasema alienda kwa jombi. na alikaribishwa ndani akaonana naye na kutoa madai yake. huyu mdogo mtu anasema jombi alichomoa bastola na kumpiga risasi kaka yake palepale alianguka na kufariki.

walishtuka wakachukua mwili na kuondoka.watu waliwashauri wasihangaike kwenda polisi jamaa alikuwa vizuri amejipanga tayari kwa lolote. huyu bwna anasema kuwa waliishia kuomboleza na kumzika kaka yao kwa majonzi mazito sana. kama atapitia thread hii nadhani atatoa ushahidi.

jombi alisumbua kipindi chote cha rais wa awamu ya pili alikuja kukamatwa kipindi cha mkapa na miaka hiyo mkuu wa mkoa wa mbeya alikuwa laurent sanya. huyu alionekana kuwa mwiba mchungu sana kwa jombi. kosa alilolifanya jombi lilikuwa ni kwenda kumwibia mama mmoja wa kizungu ambaye alikuwa mke wa mkurugenzi wa mradi wa maji wa danida. baada ya kuiba pia walimbaka mama yule kwa ukatili mkubwa sana. yule mama aliamua kujiua kutokana na kitendo kile. mradi ule ulikuwa mkubwa sana na ulisababisha danida kwa kitendo kile wasitishe ule mradi. suala hili lilikuwa na athari kubwa sana hivyo alikamatwa ingawa ulikosekana ushahidi . kwa amri ya rais aliwekwa ndani inasemekana pasipo mashtaka. detention. maana kulikosekana ushahidi wa yeye kuhusika na mashahidi kulikuwa hamna ingawa ni yeye alihusika.rais mkapa alilazimisha awekwe ndani......

Aliitwa Abinara.
Jamaa alikuwa na mke na watoto wazuri sana. Mke alikuwa mpole na mstaarabu sana.
Bila kuweka na Tunyande, Ali na Ali, Kisangani ....
Habari za huyu mtu zilikuwa mbaya.
Alikufa kifo cha aina gani na maziko yake yalikuwaje?
Mali aliyodhurumu bado yapo?
Familia yake ina maisha gani sasa?
Waliokuwa wakiishi naye kama majirani wanasema alikuwa mtu a waaina gani? Niliwahi kusikia ilikuwa wakati hajasafiri, alikesha usiku kucha katika suti nyeusi anapatrol mtaani kwake akilinda watu wasibughudhiwe. Sijui kama ni kweli. Wengine walisema alikuwa akilinda vikkosi vyake visiwekewe vikwazo. Unaelewa nini juu ya haya?
 
Alikuwa anaitwa Kipagati huyu naye ana story zilizoshiba nadhani tutapata muda wa kumjadili alikamatwa kwenye mtego wa polisi baada ya kusogezewa demu mkali na baadaye jamaa akaingia mkenge hadi kuandaa harusi ambako alikamatwa madhabahuni ingawa pia alikurupuka lakini haikumsaidia ndiyo ikawa mwisho wake
Huyu kiplgat alikuwa wa mtu wa kutoka Iringa na haswa ndio tunaweza sema alikuwa baba lao.hadi vitabu vya historia vilimwandika.nitawaletea Uzi wake
 
Nakuunga mkono,mimi pia nimegundua kua kuna chumvi ndani ya hii story



Ubabe ulitawala hata club kama utaenda na mrembo ilhali wewe huna ubavu

Je ni club ipi ilikuwepo mbeya miaka hiyo ya 80s..?
Wewe ukiambiwa club unaelewaje
 
Alaf jamaa kang'ang'ania story ya nyokaa JCB, wakati ni chindoman ambaye naye ashajipaga aka ya Jombii
 
Stori za majambazi sugu siku hizi zimepungua sio kama hapo zamani, hii inamaanisha nini ni kwamba sahivi jeshi la polisi wameimarika kiulinzi, kiuweledi na kitechnohama.
 
acha kumfananisha jombii na vitu vya kijinga,huko Arusha kwenyewe alishakuja na akalamba hela nyingi tu na vito vya dhahabu,we unaongelea vijambazi vya 2000 hapo kalale.
Hebu acha ukuda basi! Yaani watu wasio na hatia wameuawa na huyo Jombi halafu wewe unamtetea?? Shame!
 
Hebu acha ukuda basi! Yaani watu wasio na hatia wameuawa na huyo Jombi halafu wewe unamtetea?? Shame!
Nimemtetea wapi?we mpuuzi ukimquote mtu soma alichoandika vizuri.
Maisha yangu utotoni Jombi alikua na bibi pale mtaani kwetu,Alikua binadamu tu jioni baada ya kupiga umafia anarudi kwa bibi yake pale mtaani analelewa tu.
Nazungumzia 80s,
sijui ulikua wapi
Tukio la mwisho Jombi kafanya ni huko Ar alipora wazungu madini na wakamkamata porini huko akitoroka.
Kipindi cha BM akapigwa miaka mingi tu .
 
Stori za jombi nimezisikia Sana enzi hizo nakaa mbeya 1995 maeneo ya mbeya retco katika ya mabatini na stendi ya zamanj
 
Hakuna jambazi aliyewahi kusumbua nchi kama nyokaa wa Arusha.

Alipigwa risasi 3 Sakina bar Arusha miaka ya 90 mwanzoni tena walimtegea mwanamke akamwekea dawa kwenye pombe.

Ila bado maaskari ilichukua muda mrefu kwenda kuchukua maiti yake kwa kumuogopa wakifikiri yupo hai.

Karate yeye, ubabe yeye, machale yeye.

Ametungiwa wimbo na Watengwa inaitwa "Story ya nyokaa"
Nyokaa amemsumbua nani sasa wewe. Nyokaa tulikuwa tunakaa nae mtaani Sakina White Rose juu, mbele ya kwa marehemu Sedekia. Acha mastory ya uongo. Kuua watu wawili watatu ndo kusumbua? Na tena hakuuawa Sakina bar miaka ya 90, aliuawa mbele ya nyumba alikuwa amepanga hiyo mitaa ya kwa Sedekia miaka ya 2000. Mtu aliuawa kizembe vile kwa kupigwa roba na Eliya Baunsa, askari wakammalizia na risasi ndo wakusumbua watu? Punguza fix master...
 
Porojo hizo za vijiweni. Kama alikuwepo alikuwa ni jambazi tu.

Hizo za "bulushi" ndiyo kabisa uongo. Labda huwajuwi mabulushi wewe.

Bulushi umpelekee habari unaenda kumwibia aite polisi? Au akae anakusubiri?

Si kweli.
Inaonekana unawajua sana " mabwana" zako wabulushi
 
Ni dharau kubwa sana kumfananisha Jombi na vibaka wa Arusha.

Huu uzi ulikuja kutupa historia ya matukio ya ujambazi Mbeya wala sio kusifia ujambazi au kusema nani zaidi.

Ila ukweli utabaki kuwa mafaili ya Jombi yalifika hadi Ikulu kwa Mkapa.
 
Back
Top Bottom