KWELI Jokofu likiachwa milango wazi huku limewashwa halidumu kwa muda mrefu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Hivi ni kweli kuwa jokofu likiwa 'switched on' huku milango yake ikiwa wazi, hupelekea kuharibika ndani ya muda mfupi wa matumizi?

1683178205259.png
 
Tunachokijua
Jokofu (friji) ni Kifaa cha kielektroniki kilichoundwa mahususi kwa ajili ya kutengeneza ubaridi au barafu. Kifaa hiki kwa asilimia kubwa hutegemea nishati ya umeme katika kutekeleza kazi yake iliyokusudiwa. Jokofu zipo za aina na ukubwa tofauti tofauti. Wataalamu wanaeleza kuwa ukubwa wa friji unaanzia nchi 24 mpaka 40.

Je, Jokofu (Friji) likiachwa milango wazi huku limewashwa halidumu kwa muda mrefu?
Jamiiforums imepitia ripoti za kuaminika za wataalamu wa vifaa vya kilelektroniki ambao wanafafanua mambo yafuatayo:

Kampuni za Croma Unboxed na Asian Kitchen wanakubaliana kwamba kuacha mlango wa friji wazi kuna athari kubwa na kunaweza kupelekea kifaa hicho kupata shida nyingi na hatimaye kufa mapema.

Wataalamu hawa wanafafanua kuwa jokofu linapoachwa wazi wakati limewashwa huruhusu hewa ya nje kuingia ndani ya jokofu na kusababisha joto ndani ya jokofu kuongezeka, hii hupelekea friji lako kutumia nguvu ya ziada na umeme mwingi kudumisha joto lake. Hivyo, kutokana na hali hii friji likiachwa wazi kwa siku nyingi huchochea vifaa vyake hasa Kompresa kufa mapema na hatimaye friji kufa.

Pili, wataalamu wanabainisha kuwa kuacha friji wazi kuna athari pia kwenye chakula au bidhaa zinazowekwa ndani yake. Hewa ya nje inayoingia ndani ya jokofu ina unyevu ambao unaweza kuzidisha unyevu uliopo ndani ya jokofu. Hii inaweza kusababisha vijidudu na bakteria kuongezeka ndani ya jokofu na hivyo kusababisha chakula kuharibika mapema.

Zaidi ya hayo, Wataalamu hawa wanaeleza kuwa kuacha friji wazi kunaweza kupelekea kuongezeka kwa bili ya umeme kutokana na friji kutumia nishati ya ziada ili kudumisha joto lake la kawaida.

Hivyo ili kuhakikisha jokofu lako linadumu na kuepusha madhara yote yaliyofafanuliwa JamiiForums inaona ni vyema kufunga majokofu yetu ipasavyo.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom